Dk Kitima: Ni nchi gani inayoweza kufanya uzembe kwenye ajira kama Tanzania?

Domy

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
4,700
1,086
Dr Charles kitima ambaye ni makamu mkuu wa chuo cha St augustine ameyasema hayo kwenye mahafali ya chuo hicho ambapo mgeni rasmi alikuwa mh John Magufuli.

Amesema kuna wahitimu wa course ya ualimu walihitimu mwezi wa saba mwaka 2012 mpaka sasa wako mtaani wakitafuta ajira wakati shule za kata hazina kabisa walimu,

ndipo akahoji ni nchi gani inayoweza kufanya uzembe wa aina hiyo duniani zaidi ya Tanzania?

Source:StarTV habari.
 
Ni mmoja wa wasomi ninaowakubali sana, si mnafki husema kile anachokiamini bila kupepesa macho!
 
Kama kaweza kusema hivyo basi huyu elimu yake ni ya ukweli inamsaidia na itasaidia kuikomboa Nchi yetu. BRAVO Dr wa ukweli umeonesha mfano.
 
Hakuna nchi inayoweza kufanya uzembe huu zaidi ya Tanzania chini ya chama cha mapinduzi.Magamba wameua viwanda,vilivyobinafsishwa wafanyakazi wengine wanatoka nje kwa kazi wanazoweza kuzifanya Watanzania.Bado serikali haina mkakati wa kuwalinda vijana kwenye ajira,tembelea international schools utawakuta Wakenya wanafundisha kiswahili.Vigogo wa Kenya wanawekeza kwenye miundombinu ya utalii kwa mvuto wa mlima kilimanjaro na kuajiri vijana wengi lakini Magamba wanaficha fedha uswisi.Nampongeza Dr.Charles Kitima kwa kuyasema yale ambayo wasomi (fake) wanashindwa kuyasema kwa kuihofia serikali ya ccm huku vijana wakizidi kusahaulika na kupata shida.
 
Ni mmoja wa wasomi ninaowakubali sana, si mnafki husema kile anachokiamini bila kupepesa macho!

inabidi Benson Bana afuate nyayo za huyu jamaa.msema kweli daima ni mpenzi wa MUNGU.baada ya kusema hayo nikamuangalia Magufuli alivyoshtuka hakutegemea kuchanwa live pale.
 
Hawa ndo watu walioelimika .Wanaoamini wanachokisema.Sio propaganda za kina Bana,wachumia tumbo.
 
Angekuwa ni wale wajinga wangefanya kazi ya kusifia, ukishaelimika hupaswi kupepesa macho kwa unafki jiamini unamwogopa nini bg up dkt kitima.
 
Hawa ndo watu walioelimika .Wanaoamini wanachokisema.Sio propaganda za kina Bana,wachumia tumbo.

Benson Bana alikuwa anaheshimika sana ila sasa watz wanamdharau sana kutokana na yeye mara nyingi kutetea upumbavu.
 
Hata angepanda juu ya mti au mlima akayasema hayo hawa manyang'au hawasikii la mhubiri wala muazini.
 
huyu dr ni moja ya academician ambao wako strong saana nchi hii kweli pamoja na utofauti wa itikadi za kidini mi namkubali saana
 
CCM imetuvurugia nchi yetu,kwa upumbavu wake haijali maslahi ya taifa lake.
 
free mind ndio chanzo cha mabadiliko vijana tufungue fikra zetu kutoka kwenye minyororo ya serikali isiyo na tija
 
Mh. Nape lifanyie kazi hili suala tunawahitaji walimu, inaeleweka wazi hapa kuna suala bajeti si vibaya lifanyiwa upendeleo maalumu.

Chama
Gongo la mboto DSM

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
CCM imetuvurugia nchi yetu,kwa upumbavu wake haijali maslahi ya taifa lake.

Nakataa kwenye hilo wapinzani ndio wametuharibia nchi macho na masikio yao ni kwenye ruzuku tu, kazi kubwa ya vyama vya upinzani ni kuipa changamoto kwenye mambo ya maendeleo hawa wetu zaidi ya ruzuku hawana jipya

Chama
Gongo la mboto DSM

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Nakataa kwenye hilo wapinzani ndio wametuharibia nchi macho na masikio yao ni kwenye ruzuku tu, kazi kubwa ya vyama vya upinzani ni kuipa changamoto kwenye mambo ya maendeleo hawa wetu zaidi ya ruzuku hawana jipyaChamaGongo la mboto DSMSent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
akili nyepesi kama zako (zilizojaa ccm) ndo zinazofanya watu tuichukie ccm. utawezaje kuzungumza kirahisi kiasi hiki kwa hoja nzito kama hii...! halafu mtz wa aina hii bado na yeye anauaminisha umma kuwa ni mzalendo? nitakuelewa zaidi kama utakuwa form 4 liver ila kama na wewe ni msomi wa degree na ni mzawa wa nchi hii basi utambue kabisa hujaelimika bado. yaani ni heri tuanze kupigana jaman inchi ikombolewe kama wanaotutawala ndo wana akili KIDUCHU namna hii.
 
Back
Top Bottom