Dk Kitila Mkumbo: Vijana wa BAVICHA wanahitaji kufundwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Kitila Mkumbo: Vijana wa BAVICHA wanahitaji kufundwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by n00b, May 24, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  Gazeti la Rai Mwema | Jumatano, 24 Mei 2012


  Malumbano baina ya Mwenyekiti wa BAVICHA na Makamu wake katika vyombo vya habari ni hatua ya kubalehe kisiasa, ambayo haipaswi kuwakatisha tamaa wapenzi wa mageuzi nchini. Bahati mbaya kubalehe huku kunaambatana na usumbufu na kero. Usumbufu na kero hizi zingekuwa za maana kama vijana hawa wangekuwa wanalumbana juu ya jambo la msingi la kifalsafa au kisera au kikanuni ndani ya chama na nchi. Bahati mbaya kwamba vijana hawa wanalumbana kwa jambo la kipuuzi. Ni upuuzi kulumbana juu ya kauli rejareja za Mbunge wa Maswa John Shibuda, mwanasiasa ambaye mbwembwe zake za kisiasa zinajulikana hata kabla hajahamia CHADEMA.

  Kwamba Shibuda ametangaza kugombea urais ndani ya kikao cha CCM haiwezi kuwa tatizo kwa sababu kimsingi kufanya hivyo hakuvunji kanuni yeyote ndani ya CHADEMA kwa sababu hakuna kanuni yeyote inayoelekeza muda na mahali mwafaka pa kutangaza nia ya kugombea urais. Mwanachama anapaswa kuongozwa na busara zake tu juu ya muda na mahali pa kutangaza nia yake. Sasa kama mwanachama wa CHADEMA hana busara kiasi cha kutangaza nia ya kugombea urais ndani ya kikao cha ‘mpinzani' wake CCM, na kama busara za mwanachama huyo ni finyu kiasi cha kumuomba mwenyekiti wa CCM ndiye awe meneja wa kampeni zake, kwa nini iwe tatizo kwa BAVICHA au CHADEMA?

  Hivyo, haikutarajiwa kwamba kuna mtu mwenye akili sawasawa ndani ya CHADEMA angemjibu Shibuda pale alipotamka, ndani ya kikao cha CCM, kwamba angegombea urais kupitia CHADEMA mwaka 2015. Kauli ya Shibuda haikustahili kupewa umakini wowote hasa kwa kitendo chake cha kusema kwamba Rais Kikwete ndiye angekuwa meneja wake wa Kampeni. Hili peke yake lilitosha kuonyesha kwamba kauli za Shibuda ni mwendelezo wa mbwembwe zake kisiasa zisizostahili kupewa uzito wowote ule. Hivyo, kwa Mwenyekiti wa BAVICHA kutoa tamko kali juu ya Shibuda ilikuwa sawa na mtu mwenye akili timamu kujaribu kumkimbiza kichaa aliyekimbia na nguo zake. Ni vizuri wanasiasa vijana wakaielewa kwa upana wake dhana ya uhuru wa maoni. Uhuru wa maoni ni pamoja na kukubali kusikia yale usiyoyapenda na kuyataka.

  Katika kujitutumua kisiasa, Makamu wa BAVICHA naye anatoa tamko la kumkana ‘bosi' wake, tena hadharani na nje ya viwanja vya chama. Madai ya makamu huyu wa BAVICHA ni kwamba hakuna kikao kilichoidhinisha tamko la Mwenyekiti wa BAVICHA kusema hayo aliyoyasema. Haya, na yeye tunamuuliza kikao gani cha BAVICHA kiliidhinisha yeye kumpinga mwenyekiti wake hadharani mbele ya waandishi wa habari? Je, makamu wa BAVICHA aliona ugumu gani kwenda kumshtaki mwenyekiti wake kwenye vikao vya BAVICHA na/au CHADEMA?

  Nafikiri vijana hawa wa BAVICHA wanahitaji kufundwa. Nawashauri viongozi wa CHADEMA kuchukua hatua muhimu za kuwafunda vijana wa BAVICHA ili ubalehe wao wa kisiasa upite bila madhara kwa chama. Kufundwa huko ni pamoja na kuwafundisha namna ya kufanya kazi na vyombo vya habari. Wanahitaji kuhariri matamko yao sawasawa, na kabla ya kuyatoa wapime athari za matamko yao kwa chama. Ukiona wewe ni kiongozi wa CHADEMA unatoa tamko na tamko hilo linapamba vichwa vya habari vya magazeti pinzani kwa chama chako kama vile Uhuru, ujue tamko lako limekiumiza chama.


  Laiti viongozi wa BAVICHA wangekuwa makini wangejizuia kutoa matamko yao. Mwenyekiti wa BAVICHA angekuwa makini angetafakari maana ya kauli yake kabla hajaitoa, na angedundua kwamba tafsiri pana ya kauli yake ni kutaka kuzuia baadhi ya wanachama wa CHADEMA kugombea urais. Naye makamu wake angekuwa makini angetambua kwamba kumpinga mwenyekiti wake hadharani ni kutangaza mgogoro ndani ya chama, na ilikuwa ni kucheza mikononi mwa wapinzani wa CHADEMA. Viongozi hawa wanapaswa kutambua kwamba katika mawasiliano muhimu siyo unachosema, bali kile ambacho hadhira inasikia. Kwenye tamko la Mwenyekiti wa BAVICHA hadhira walisikia kwamba baadhi ya wanachama wa CHADEMA hawaruhusiwi kutangaza kugombea urais, na walichosikia hadhira ya makamu wake ni kwamba kuna mgogoro ndani ya CHADEMA! Je, huu ndio ujumbe ambao viongozi hawa walitarajia kuufikisha?

  Msimamo wa CHADEMA dhidi ya kauli za Shibuda umekuwa ni ‘kumdharau' kwani, pamoja na kwamba zinasababisha usumbufu, kauli zake zimekuwa hazina madhara ya msingi kisiasa kwa chama. Hata hivyo kauli za Shibuda iliyoripotiwa katika moja ya magazeti ya Jumapili ni zaidi ya usumbufu. Kwamba viongozi wa CHADEMA wanamchukia Shibuda kwa sababu ni msukuma ni kukigombanisha chama na wapiga kura wa kanda ya ziwa. Huu sasa sio usumbufu tena bali ni uharibifu. Usumbufu unavumilika, lakini uharibifu hauwezi kuvumilika. Ni wazi kuwa Shibuda amepania kuiharibu CHADEMA. Kwa hivyo kuna haja ya kuangalia upya sera ya kumdharau Shibuda.

  Tukumbuke kwamba mambo yote haya yanatokea kipindi ambacho Waziri mwandamizi katika serikali ya CCM ameapa kuona CHADEMA inasambaratika ndani ya mwaka mmoja. Vijana wa BAVICHA yawapasa kuwa makini, vinginevyo wataonekana wapo katika mkakati wa kuisambaratisha CHADEMA. Tumewaonya!


  Dk Kitila Mkumbo ni Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
   
 2. ma2mbo

  ma2mbo JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 699
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  kitila mkumbo ndio mmoja ya anaewachochea alafu anaenda kujikosha....aya ni makovu ya uchaguzi wa bavicha.
   
 3. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hapo wanaanza kulumbana hata hawajafika mbali! wakishawekwa kwenye umate umate je?
   
 4. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,906
  Likes Received: 5,367
  Trophy Points: 280
  Anayetakiwa kufundwa ni yule pandikizi la CCM, Juliana sijui..
   
 5. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mi nakuunga mkono Dk. Kitila,

  Lakini pia naomba mkumbuke kuwa kauli za huyu mkimbizi wa siasa zinakera, zinafanya mtu ufukute joto la ndani, yani unajihisi upo kwenye tanuru, kwa sababu kila anachokifanya na kukisema kinaidhirisha jamii kwamba nia yake ni kuvuruga chama, na hili lipo wazi.

  Hata ukiaangalia utetezi wake akiongea kidogo tu anaanza kuingia kanda ya kaskazini against kanda ya ziwa, oooh wametumwa na viongozi wa juu oooh chama kinawenyewe... Yaani unaona kabisa nia ya jamaa sio njema hata kidogo.

  So sometimes tunatofautiana kwenye uvumilivu so siwezi kumkandia mwenyekiti wa BAVICHA straight lakini nawashangaa zaidi nyie wakuu kwa kitendo chenu cha kuyadharau maneno anayoyatoa huyu mkimbizi....chukueni hatua haraka tafadhali, siku si nyingi atatuvuruga.... Anajulikana kabisa ni shushushu toka enzi, sasa tuwe makini wakuu....
   
 6. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,172
  Likes Received: 1,256
  Trophy Points: 280
  Fukuzeni huyu msukuma mwenzangu. Tonvanvebhe ng'hana.
   
 7. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,209
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Dr Mkumbo unasemaje juu ya kauli ya Shibuda kwamba CCM bado ni chama imara na kinastahili kuendelea kutawala?

  Na je vipi kuhusu mambo mengine kama vile Shibuda kupinga msimamo wa kisera wa CDM kama suala la posho?

  Mimi naona mdharau mwiba.....

  Na Makamu Mwenyekiti ametoa tuhuma juu ya kitengo cha habari cha CHADEMA Makao makuu kwamba kinaingilia mambo ya vijana kupitia kwa Afisa Habari aliyeandaa tamko la Heche. Je, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi Mh. JJ Mnyika anasemaje? Au Afisa Habari ndugu Tumaini Makene anasemaje?

  Jambo jingine, tamko la Makamu M/kiti linaonekana kubeba agenda yenye hisia ya makundi ndani ya CHADEMA hasa ukiangalia wale waliomuunga mkono wazi au kwa kificho.

  Sisi wengine tupo mbali sana na CHADEMA lakini tunaona mambo kwa macho mawili, nina hakika waliomo ndani wanajua kinachoendelea. Katika mustakabali huu je, hakuna sababu ya kutilia maanani choko choko hizi zinazoendelea na hivyo kuendana na usemi wa wahenga.. usipoziba ufa...
   
 8. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Well said by Dr Kitila Mkumbo. Unastahili nafasi muhimu sana katika kujenga future ya nchi yetu mara tutakapowaondoa wakoloni weusi kupitia sanduku la kura hapo 2015
   
 9. K

  Konya JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 920
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kwa yaliyotokea nafikiri itakuwa ni funzo tosha viongozi wa bavicha na CHADEMA kwa ujumla
   
 10. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #10
  May 24, 2012
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Kivipi nawachochea? Najikosha kwa nani? Unaweza kufafanua kidogo ueleweke?
   
 11. F

  FJM JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hoja ya Shibuda kutangaza nia yake ya kugombea urais mbele ya NEC ya CCM si issue sana. Kwangu mimi shida ni haya maneno aliyosema mbele ya CCM

  "Muda wa vyama vya upinzani kukabidhiwa madaraka haujakifaka"

  Sasa kama muda haujafika yeye anagombea kupitia chama kipi?
   
 12. N

  Nabihu JF-Expert Member

  #12
  May 24, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  HECHE alikuwa anatafuta sifa kwa aliyempa nafasi hiyo Mbowe & Juliana alikuwa anataka kuipa heshima BAVICHA...

  ....waendelee kupata semina za CDU.
   
 13. mlaizer

  mlaizer JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  nakubaliana na maoni ya Dr. mkumbo,i doubt m/kiti na makamu wa BAVICHA hawaelewani...........
   
 14. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,209
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mkuu Dr afadhali upo hapa. Unaweza kuhusisha kile kilichotokea wakati wa uchaguzi wa Bavicha mpaka kufikia hatua ya Shibuda kuunda timu iliykutana usiku hotelini pale Magomeni. Nisingependa ueleze yaliyotokea hapa as naamini habari hizi zilikuwa confidential na zilishughuliwa vilivyo na kamati ya Marando, Profesa Safari na Christowaja Mtinda na hatimaye kuwaengua wale wote walioshiriki kwenye mpango wa kuweka mamluki. Nilikuwa najaribu tu kukumbushia haya ili msipuuze haya mambo vinginevyo Comrade Wassira anajua wanachofanya na kupitia vikundi vikundi hivi vya kina Mwampamba, Mchange na Juliana mtashindwa kutimiza ndoto za Watanzania. Tumewatahadharisha mapema
   
 15. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2012
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Dr. Kitila Mkumbo namkubali sana lakini kaniudhi sana. Kwanini hakugombea ubunge wa Africa Mashariki? Bado mpaka leo sijaelewa. Ana uwezo mkubwa wa kuona mbali tangia akiwa Mwenyekiti wa Kitivo cha Sayansi, alafu akawa Raisi wa DARUSO wakati huo DARUSO ikiwa DARUSO kweli kweli
   
 16. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #16
  May 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kwangu mimi shibuda ni komedian
   
 17. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  The Kitila Mkumbo niliyepata kumfahamu miaka yote ndiye huyu huyu hapa kwenye superb logical thinking and sound arguement WITHOUT PREJUDICE the least.

  Hebu kamtambue huyu rafiki yangu kuwa ni mtu wa ina gani kwa kupitia japo hicho kijipande hapo chini. Hakika Mkumbo kamaliza kila kitu kwa kuniibia mawazo yangu juu ya kiji-mzozo uchwara ndani ya BAVICHA - Vijana sasa elekezeni nguvu kwenye 'Vua Gamba' na ktu msiende huko anakowatafutia Mzee Shibuda - Mzee ambaye anazeeka vibaya baba yetu huyu:


  ... Kwamba Shibuda ametangaza kugombea urais ndani ya kikao cha CCM haiwezi kuwa tatizo kwa sababu kimsingi kufanya hivyo hakuvunji kanuni yeyote ndani ya CHADEMA kwa sababu hakuna kanuni yeyote inayoelekeza muda na mahali mwafaka pa kutangaza nia ya kugombea urais. Mwanachama anapaswa kuongozwa na busara zake tu juu ya muda na mahali pa kutangaza nia yake. Sasa kama mwanachama wa CHADEMA hana busara kiasi cha kutangaza nia ya kugombea urais ndani ya kikao cha ‘mpinzani’ wake CCM, na kama busara za mwanachama huyo ni finyu kiasi cha kumuomba mwenyekiti wa CCM ndiye awe meneja wa kampeni zake, kwa nini iwe tatizo kwa BAVICHA au CHADEMA? ....
   
 18. P

  Peres Member

  #18
  May 24, 2012
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naungana kabisa na Dr. Kitila! Hawa vijana wanahitaji kulelewa na kufundwa kisiasa juu ya nini cha kusema, wapi na wakati gani.
   
 19. S

  SIXPLANET Member

  #19
  May 24, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kutofautiana ni kujifunza kama walio tofautihana wanaweza kusikilizana.
  Na pia uvumilivu unamwisho, hakuna sababu ya kuwa na mtu anaye waludisha nyuma wakati sisi tunasonga, what is the cost and benefit of having shibuda?
   
 20. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #20
  May 24, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mkumbo, u have made my day
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...