Dk. Kigwangalla aagiza kufungwa chumba cha upasuaji cha Hospitali ya Sanitas ya Mikocheni

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,768
3,621
Naibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza kufungwa mara moja Chumba cha upasuaji cha hospitali ya Sanitas ya Mikocheni Jijini Dar es Salaam baada ya kubaini kuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo mfumo na ramani yake kimefungwa kwa kutokidhi vigezo vya kimataifa vya namna chumba hicho kinavyotakiwa kuwa.

Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo mapema jana Februari 29.2016, alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye hospitali hiyo majira ya saa nane na nusu mchana ambapo baada ya kutembelea hospitali nzima na kushuhudia namna ya utolewaji wa huduma, hakuridhishwa na hali aliyokutana nayo kwenye chumba hicho na kutoa maagizo kwa Msajili wa Hospitali Binafsi, Dkt. Pamela Sawa kufunga chumba hicho mpaka uongozi wa hospitali hiyo utakapofanya marekebisho ya mapungufu yaliyopo.

“Chumba cha upasuaji hakiko sawa, siwezi kuvumilia kuacha chumba hiki kiko chini ya kiwango cha kimataifa. Rekebisheni chumba hiki kwa kutumia mfumo wa ramani wa wizara,” alieleza Dkt. Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo kwa mmoja wa Ofisa wa Hospitali hiyo.

Aidha uongozi wa hospitali hiyo umepewa siku saba wawe wamewasilisha maelezo ya kutowalipa mishahara kwa kipindi cha miezi minne watumishi wake pamoja na jinsi wanavyoteketeza taka hatarishi za hospitali hiyo.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo alipata malalamiko kutoka kwa watumishi hao ambao wamelalamikia kukatwa kwa makato ya mafao pasipo kupelekwa mahali husika kwa zaidi ya miaka mitatu na nusu.

Dkt. Kigwangalla alivitaja viwango vya chumba cha upasuaji kuwa kinatakiwa chumba cha kubadilishia mavazi,kunawa mikono,sehemu ya alama maalum zenye rangi nyekundu, meza ya upasuaji, ukanda wa usafi, chumba cha mapunziko baada ya kutoka kwenye upasuaji na chumba cha kusafishia vifaa vya upasuaji na kuna mashine maalum kwa kuwa kila upasuaji una idadi ya vifaa vinavyotumika.

Aliongeza kuwa viwango hivi vinawekwa ili kuepuka maambukizi.

Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa hospitali hiyo, Bi. Gean Cabral alisema watarekebisha mapungufu yaliyobainika pamoja na kufanya yale yote waliyoagiziwa baada ya tukio hilo.

dk-hk-34.jpg
 
Na wawakumbuke wale mgambo wa ilala waliowalipa elfu 50 kwa mwezi badala ya 220,000/=. Lakini vile vile kuna matatizo mengi sana hospitali za serikali ukiondoa muhimbili na wala hawastuki. Madaktari wanafanya kazi katika mazingira magumu, vifaa tiba hakuna nk. HAPA KAZI TU
 
Kitu cha ajabu mawaziri wanapenda sana kuwa na waandishi wa habari ili habari zao zisikike lakini wananchi wanapotaka kujua kinachoendelea bungeni wanakuwa mbogo.
 
Hivi huyu jamaa mbona haji mikoani akajionea!
Yeye ni daktari anajua nini kilichopo huko mikoani na anajua nini Dr. Ulimboka alikuwa anagombea na yeye alikuwa anamuunga mkono Ulimboka leo kapewa shavu kasahau matatizo ya madaktari. This is not fair
 
Tunasema tena, Kigwangalla na Ummy wana dalili zote za kuwa mawaziri mzigo. Sekta ya afya ina changamoto lukuki lakini hadi sasa wawili hawa hawaonekani kuwa na mkakati wa maana. Kila kukicha ni story za kushtukiza na kuuza sura.
 
Kitu cha ajabu mawaziri wanapenda sana kuwa na waandishi wa habari ili habari zao zisikike lakini wananchi wanapotaka kujua kinachoendelea bungeni wanakuwa mbogo.
uhuru wa kupata habari ni haki ya msingi ya Mtanzania
na kufahamu serikali yake inafanya nn

thank AWAMU YA TANO KWA KUWEKA WAZI UHURU WA KUPATA HABARI

HIYO HOSPITALI NIMEIJUA SIFANYIWI OPERATION MPAKA KIGWANGALA ; HARUHUSU


MEDIA NI MHIMILI WA NNE WA NCHI.
BAAADA YA BUNGE, MAHAKAMA NA SERIKALI
 
wananiudhi sana hawa mawaziri....

Hivi job description yao ni Dar tu

Hasa huyu kigwangala...kutwa kuchwa kuhangaika na vi dispensary vya mtaani
dar ndio tz wewe. 10% ya watanzania wamebanana dar wengi wapo makorongoni aheri waliobaki vijijini
 
Hivi wale waganga na wakaguzi wakuu wa wilaya na mikoa wanafanya nini ........... Maana kama kila kitu hadi aje Rais au Waziri inamaa hawa haya hawayaoni .................
Na kwanini mnawaacha wakati hawafanyi kazi zao ....................
Kwa mtindo huu wa hadi wafike viongozi wa juu ndio wafanye maamuzi ya chini kabisa ina maana sisi wa Mbekenyera na Nanjilinji si tutafikiwa mwaka 2096. ............
 
uhuru wa kupata habari ni haki ya msingi ya Mtanzania
na kufahamu serikali yake inafanya nn

thank AWAMU YA TANO KWA KUWEKA WAZI UHURU WA KUPATA HABARI

HIYO HOSPITALI NIMEIJUA SIFANYIWI OPERATION MPAKA KIGWANGALA ; HARUHUSU


MEDIA NI MHIMILI WA NNE WA NCHI.
BAAADA YA BUNGE, MAHAKAMA NA SERIKALI
Mkuu hili mbn hukuliongelea akat tulivyonyimwa haki ya kupata habari za bunge live au ndo unafiki at its best
 
Back
Top Bottom