Dk. Kigwangala hajui kwa nini watu wanataka katiba mpya

Shing'weng'we

New Member
Dec 10, 2010
3
0
"Many people are claiming and advocating for a new constitution, but most don't give reasons why? Why do you think we need a new constitution? or Major changes in the current constitution? What are the issues people?" Kutoka post yake kwenye facebook.
 
kayumba

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
653
72

Sishangai kwa post yake.
KWANINI: 1. Ni mbunge wa ccm, tumeona huko nyuma wabunge wa ccm walivyo kejeli honja za msingi kwa nchi yetu!
2. Ni mchanga kwenye siasa
3. Jinsi alivyopata nafasi ya kugombea kupitia ccm inamfanya asiwe kwenye nafasi nzuri ya kutao mchango wenye mawazo kinyume na mtizamo wa chama chake kwa sas
 
zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,006
3,667

He is asking very valid questions, let's be open minded and answer him why we need newer constitution, I say newer because ours is still new, not even 50 years old.

My reason: katiba sio msahafu unaweza badilishwa time yoyote ili mradi uwe kwa manufaa ya waTanzania wote.
 
Kiranga

Platinum Member
Jan 29, 2009
60,499
74,717
"Many people are claiming and advocating for a new constitution, but most don't give reasons why? Why do you think we need a new constitution? or Major changes in the current constitution? What are the issues people?" Kutoka post yake kwenye facebook.

Ingawa nishasema sana kwamba Kigwangala ni usurper / pretender, lakini kusema kwamba hajui sababu ya watu kutaka katiba mpya kwa sababu ya hiyo post ni kumpakazia.

Alichofanya mheshimiwa Dk. hapo juu ni kuchokoza mjadala, watu waseme wanataka katiba mpya kwa sababu gani. Hili ni tofauti kabisa na mtu kusema hajui kwa sababu gani watu wanataka katiba mpya.

Tusiwe kama waandishi wa magazeti ya udaku.
 
Gad ONEYA

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
2,633
168
Siamini kama anongea hivyo kwa sababu ya uchanga wake kwenye siasa! Anajua anachokifanya!
 
Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
11,294
20,189
.....but most don't give reasons why? Why do you think we need a new constitution? or Major changes in the current constitution? What are the issues people?.

Huyu jamaa hajasema kwamba hajui kwa nini wanataka katiba mpya. Anawauliza watu waseme issues ni zipi! kuna tofauti kubwa kati ya kutojua na kuuliza swali la ''kizushi'' ili kuchokoza mjadala. Nina uhakika Kigwangala anachokoza mjadala hapa.

Lakini maswali yake ni ya msingi. What are the issues?? unaweza kukuta tunapigia kelele vitu ''vichache'' mno ambavyo kumbe havihitaji katiba mpya bali mabadiriko kidogo.

Tunaweza kumjibu Kigangwala kwa kuanza kusema issue moja moja inayohitaji kuwekwa/kubadilishwa ndani ya Katiba
 
junior2008

JF-Expert Member
Apr 27, 2009
528
42
"Many people are claiming and advocating for a new constitution, but most don't give reasons why? Why do you think we need a new constitution? or Major changes in the current constitution? What are the issues people?" Kutoka post yake kwenye facebook.

Huyu ni kilaza mkubwa! Kwanza anakubali watu wengi wanataka katiba mpya ila anasema walio wengi hawatowi sababu, kwahiyo kuna wachache wanatoa sababu! Kama haelewi sababu mpaka sasa ama ni mpumbavu na anayetuthibitishia kwamba ubunge aliyopewa na CCM (baada ya kumwengua Hussein Bashe)hana uwezo nao au ni mwendelezo wa kujibembeleza kwa mabosi wake! Madai ya katiba mpya hayajaanza leo wala jana ni ya muda mrefu, CHADEMA wameyafufua tu. Kama viongozi maarufu ndani ya CCM kama vile Mkapa, Jaji Bomani, Jaji Manento na Balozi Mbita na viongozi mbalimbali wa dini wanaona umuhimu wa katiba mpya na wanatoa sababu basi Kigwangala ni kilaza asiyestahili kuwa mbunge!!!
 
Buyengwa

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,175
10,366
The issues: 1. Madaraka ya rais ni makubwa mno hususani katika uteuzi wa viongozi wa nafasi nyeti. 2. Wateule wote wa rais wanapaswa waidhinishwe na bunge ili wawajibike kwa bunge. Wateule kama jaji mkuu na wakuu wa majeshi 3. Nafasi za makamu wa rais,manaibu waziri,wakuu wa mikoa na wilaya ni redundant na wasteful of state resources,ivyo zifutwe. 4. Rais aapishwe miezi 3 baada ya matokeo kutangazwa ili kutoa fursa ya kupinga matokeo mahakamani. 5. Tume ya uchaguzi iwe huru na viongozi wake wawajibike kwa bunge,na iwe na wafanyakazi wa kudumu waajiriwa,wakiwamo wasimamizi wa uchaguzi majimboni,na sio wakurugenzi kama ilivyo sasa. 6. Itikadi ya dola iwekwe wazi,aidha ujamaa au ubepari. 7. Rais hasiwe na mamlaka na uamuzi wa mwisho juu ya ardhi na matumizi yake. Hiyo iwe kazi ya bunge kwani ndio sauti ya wananchi. 8.Suala la wabunge kupita bila kupingwa lisitishwe,na pawepo na kura za ndio na hapana inapojitokeza hali ya kuwepo mgombea 1. 9. Nafasi 10 za uteuzi wa rais wa wabunge zifutwe,hazifuati misingi ya demokrasia. 10. Nafasi za makatibu wakuu wa wizara na wakurugenzi wa halmashauri,miji,wilaya na majiji ziwe za kugombaniwa yaani za kuaajiriwa. 11. Mawaziri wateuzi wasiwe wabunge,na uteuzi wao lazima uidhinishwe na bunge. 12. Maamuzi makubwa ya rais,kama ya kuanzisha au kufuta nafasi za madaraka mbalimbali katika utumishi wa umma, lazima yaidhinishwe na bunge. 13. Katika uchaguzi mkuu na mdogo,mshindi wa urais,ubunge udiwani,uenyekiti wa kijiji au mtaa,lazima awe amepata asilimia 50 ya kura kutokana na idadi ya waliopiga kura. 14. Iwepo nafasi ya wagombea huru kushiriki katika chaguzi kuu na ndogondogo,katiba iwekwe wazi. 15. Kuwe na wizara za kudumu ambazo hakuna rais atakaeweza kuzibadili,ziwe za fedha, elimu,ulinzi,afya,kilimona mazingira,maliasili na utalii,nishati,maendeleo ya jinsia na ustawi wa jamii,michezo na utamaduni,mambo ya ndani,mambo ya nje na wizara ya sayansi na teknolojia. Hizi ndo issues zinazonifanya nitake na kudai KATIBA MPYA.
 
Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
9,547
"Many people are claiming and advocating for a new constitution, but most don't give reasons why? Why do you think we need a new constitution? or Major changes in the current constitution? What are the issues people?" Kutoka post yake kwenye facebook.

He was the third in the opinion poll. So he does not have any idea.
 
Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
10,766
23,679
Huyu Kigwangala ni mbunge kweli au kapewa ubunge? Ni Dr kweli au katunukiwa? Nashindwa kuelewa kama kweli Kigwangala mpaka leo hii anahitaji watu waanze kuorodhesha sababu za kuwa na katiba mpya. Kama ni kweli basi kumbe aheri Mzee Hashim Mbita ana upeo mkubwa wa kuelewa kuliko huyo Kigwangala wenu. Katiba hubadilishwa mfumo wa uendeshaji wa nchi unapobadilika. Tulikuwa kwenye ujamaa, sasa haupo tena, na huo mfumo ulikuwa na mambo mengi ndani ya katiba ya kuulinda. Tulikuwa na mfumo wa Chama kimoja ........... Aah! Huyu atatupotezea muda. Mwambieni akasome ripoti ya Jaji Nyalali, Kisanga, n.k. humo kuna mambo lukuki, ataelimika. Baadaye aende kwa Dr Slaa, Mbowe, Dr Mvungi, Prof. Mpangala, n.k. walikwishaeleza mara nyingi, wanaweza kumkaririsha. Akishindwa kuelewa, tuachane naye, ni mbabaishaji.
 
Cynic

JF-Expert Member
Jan 5, 2009
5,146
1,642
Huyu naye ni nani hadi awe gumzo tz? nimejaribu kumgoogle naona giza tu
 
MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
8,115
3,058
The issues: 1. Madaraka ya rais ni makubwa mno hususani katika uteuzi wa viongozi wa nafasi nyeti. 2. Wateule wote wa rais wanapaswa waidhinishwe na bunge ili wawajibike kwa bunge. Wateule kama jaji mkuu na wakuu wa majeshi 3. Nafasi za makamu wa rais,manaibu waziri,wakuu wa mikoa na wilaya ni redundant na wasteful of state resources,ivyo zifutwe. 4. Rais aapishwe miezi 3 baada ya matokeo kutangazwa ili kutoa fursa ya kupinga matokeo mahakamani. 5. Tume ya uchaguzi iwe huru na viongozi wake wawajibike kwa bunge,na iwe na wafanyakazi wa kudumu waajiriwa,wakiwamo wasimamizi wa uchaguzi majimboni,na sio wakurugenzi kama ilivyo sasa. 6. Itikadi ya dola iwekwe wazi,aidha ujamaa au ubepari. 7. Rais hasiwe na mamlaka na uamuzi wa mwisho juu ya ardhi na matumizi yake. Hiyo iwe kazi ya bunge kwani ndio sauti ya wananchi. 8.Suala la wabunge kupita bila kupingwa lisitishwe,na pawepo na kura za ndio na hapana inapojitokeza hali ya kuwepo mgombea 1. 9. Nafasi 10 za uteuzi wa rais wa wabunge zifutwe,hazifuati misingi ya demokrasia. 10. Nafasi za makatibu wakuu wa wizara na wakurugenzi wa halmashauri,miji,wilaya na majiji ziwe za kugombaniwa yaani za kuaajiriwa. 11. Mawaziri wateuzi wasiwe wabunge,na uteuzi wao lazima uidhinishwe na bunge. 12. Maamuzi makubwa ya rais,kama ya kuanzisha au kufuta nafasi za madaraka mbalimbali katika utumishi wa umma, lazima yaidhinishwe na bunge. 13. Katika uchaguzi mkuu na mdogo,mshindi wa urais,ubunge udiwani,uenyekiti wa kijiji au mtaa,lazima awe amepata asilimia 50 ya kura kutokana na idadi ya waliopiga kura. 14. Iwepo nafasi ya wagombea huru kushiriki katika chaguzi kuu na ndogondogo,katiba iwekwe wazi. 15. Kuwe na wizara za kudumu ambazo hakuna rais atakaeweza kuzibadili,ziwe za fedha, elimu,ulinzi,afya,kilimona mazingira,maliasili na utalii,nishati,maendeleo ya jinsia na ustawi wa jamii,michezo na utamaduni,mambo ya ndani,mambo ya nje na wizara ya sayansi na teknolojia. Hizi ndo issues zinazonifanya nitake na kudai KATIBA MPYA.

hizo zote ni sababu moja tu, ambayo inahitaji marekebisho mawili tu ktk katiba iliyopo
 
Buyengwa

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,175
10,366
QUOTE=MkamaP;hizo zote ni sababu moja tu, ambayo inahitaji marekebisho mawili tu ktk katiba iliyopo.

Marekebesho mawili yepi? Pia toa sababu zako nawewe. Don't be a critic with no ANSWERS,unless you are a POLLUTER by making NOISE.
 
MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
8,115
3,058
QUOTE=MkamaP;hizo zote ni sababu moja tu, ambayo inahitaji marekebisho mawili tu ktk katiba iliyopo.

Marekebesho mawili yepi? Pia toa sababu zako nawewe. Don't be a critic with no ANSWERS,unless you are a POLLUTER by making NOISE.
Rekebisho la kwanza
1.Madaraka ya Rais ambalo litaikumbuka pia tume ya uchaguzi. Hii inahitaji katiba mpya??
 
Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,379
10,152
"Many people are claiming and advocating for a new constitution, but most don't give reasons why? Why do you think we need a new constitution? or Major changes in the current constitution? What are the issues people?" Kutoka post yake kwenye facebook.

Tumjibu Kigwangala kwa staha badala ya kumshambulia;inawezekana akawa hajui kwa nini tunataka katiba mpya na wala sio hii iliyopo ifanyiwe amendments zaidi!

Kigwangala;

Mimi naona tunataka katiba mpya maana tukisema tuirekebishe hii iliyopo bado tutatia viraka kila sehemu ya na kuifanya iswe tena na uasilia wake!

Mosi;Madaraka ya Rais wa TZ ni makubwa sana;Rais anapaswa kupunguziwa madaraka yake kwa nusu ya asilimia aliyo nayo.Rais asiwe na nguvu ya kuteua TUME YA UCHAGUZI inayosimamia uchaguzi ambao yeye anashiriki;Watendaji wa Rais kama vile Wakurugenzi wa Wilaya wasiwe ndiyo wasimamizi wa chaguzi mikoani na Wilayani!

Pili;Matokeo yanayotangazwa na Tume yasiyo ndiyo ya mwisho kama mgombea aliona kuna nyufa kadhaa zilizosababisha yeye kushindwa;watu wawe huru kwenda mahakamani kupinga ushindi wowote ule kutoka udiwani hadi RAIS

Tatu;Rais aendelee kuteua watendaji wake lkn Bunge ndiyo liwathibitishe na wakivurunda hata kama Rais bado anawahitaji Bunge liwe na uwezo wa kumwambia Rais kuhusu uzembe wa watendaji wake,asipochukua hatua Bunge liwe na uwezo wa kupiga kura ya kutokuwa na imani na watendaji hao!

Nne;Mhimili wa Serikali yaani Bunge liwe na nguvu yake na Rais asiliingilie;Bunge liwe na uwezo wa kukataa hoja za serikali na nguvu yake iendelezwe hadi kwenye idara nyeti za serikali,ni bunge tu ndilo lipewe uwezo wa kuthibiti mapato ya serikali na HAMNA MATUMIZI yatakayaofanywa na serikali bila kupitishwa na Bunge

Tano;Mhakimu na majaji wateuliwe na Rais lkn wathibitishwe na Bunge na wakisha thibitishwa RAIS asiwe tena na uwezo wa kuwaondoa madarakani lkn wanaweza ondolewa na kura ya kutokuwa na imani ndani ya Bunge

Sita;Katiba itamke wazi idadi ya wizara zinazopaswa kuundwa na anayeshinda nafasi ya RAIS;kama katiba labda itasema Mawaziri wawe 20,Makatibu wakuu 20 na hamna manaibu basi lzm sheria hii itekelezwe kama ilivyo

Saba;Misamaha ya kodi ni suala ambalo linapaswa kuingizwa ndani ya katiba;hapo katiba ioanishe ni misamaha ipi inapaswa kutolewa hasa ya kibinadamu tofauti na sasa ambako Waziri tu anaweza jiamulia asemehe kodi

Nane;Ingawaje Rais ndiye amiri jeshi mkuu lkn katiba yetu haisemi lolote uwezo wa Bunge kumdhibiti Rais kuyatumia majeshi yetu vibaya;katiba mpya iseme kuwa ni Bunge tu ndilo litakalopiga kura kulipeleka Taifa vitani,ni bunge tu ndilo litakalo amua jeshi letu likatoe wapi misaada ya kibinadamu;tofauti na sasa ambapo Rais kwa uwezo wake mwenyewe anaweza lipeleka taifa vitani

Nane;Katiba mpya iseme nafasi ya znz huru ndani ya Tanzania;katiba mpya iongelee coalition governamnt iliyoundwa znz;katiba mpya iweke sheria kuhusu jambo hilo kama litakuja kutokea hata bara;na katiba mpya iseme kuwa na serikali tatu tanzania sio dhambi!

Kumi;ni mengineyo mengi sana ambayo kuyataja yote nitajaza kurasa na kurasa,katiba mpya iongelee hata mali asili,michezo,mila,desturi,Utanzania na kumiliki uchumi wao,iongelee hadi hatima ya vizazi vyetu vijavyo!

Kigwangala;

Kwa sababu hizo na zingine nyingi zilizoachwa bado utazidi kusema hujui kwa nini tuandike katiba mpya ?
 
Mie naona ni madaraka ya rais tu kurekebishwa na kwa sababu hizo sioni umuhimu wa katiba mpya.

NA ukiangalia kwa makini unaona ni wanasia manyang'au tu wanataka katiba irekebishwe ili wapate uhaueni wa kuingia madarakani, angalia sababu zao za katiba ni kwa rais na tume tu? sisi wananchi mbona hiyo katiba haina sababu za misingi za wananchi??
 
Buyengwa

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,175
10,366
QUOTE=MkamaP;Rekebisho la kwanza
1.Madaraka ya Rais ambalo litaikumbuka pia tume ya uchaguzi. Hii inahitaji katiba mpya??

Unaielewa katiba lakini? Madaraka ya rais na tume ya uchaguzi ni tofauti kabisa. Rais anateua mwenyekiti na makamishina wa tume tu. Ivyo unaporekebisha madaraka ya rais,sielewi namna gani utaikumbuka na tume kwa upande wa utendaji wake. Kwaiyo hakuna kitu hapa. Bado hujaniconvince,KATIBA MPYA bado ninaitaka.
 
Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,379
10,152
MkamaP

Yanayopaswa kurekebishwa ni mengi sana;

(I)Check and Balance

A.Madaraka ya Rais

B.Nguvu ya Bunge

C.Uhuru wa mahakama

(II)SYSTEM

A.Nguvu za amiri jeshi mkuu wa majeshi

B.Uteuzi

C.Muundo wa serikali

(III)MENGINEYO

A.Nafasi ya ZNZ na Tanganyika
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom