Dk. Kafumu atelekeza wanavikundi Igunga; Asema "Siwezi tena kutoa Mikopo Mimi Si Mbunge wa Igunga"

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2][/h]JUMAPILI, SEPTEMBA 02, 2012 07:44 NA ABDALLAH AMIRI, IGUNGA


SIKU chache baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Tabora kutengua ubunge wa Mbunge wa Igunga, Dk Dalaly Kafumu, baadhi ya wananchi wamekumbwa na taharuki kutokana na ahadi kwa wakazi hao.

Wakizungumza na MTANZANIA, baadhi ya wananchi jimboni humo wamesema kabla ya kutenguliwa ubunge, Dk. Kafumu alikuwa amewaambia wananchi kuunda vikundi aweze kuwapatia mikopo kwa ajili ya biashara zao.

Wanasema waliitikia wito huo na walifungua akaunti zao katika tawi la NMB Igunga, lakini cha kushangaza baada ya hatuam hiyo, kesi ya kupinga ubunge ikiendelea, Dk. Kafumu aliwaomba wasubiri mikopo hiyo baada ya kesi hiyo.

Hata hivyo, baada ya kutenguliwa ubunge, Dk. Kafumu hakuweza kuonana na kikundi chochote, jambo ambalo wamesema wanahisi wametelekezwa.

Wanavikundi wamedai kitendo alichofanya Dk. Kafumu kimewavunja moyo kwa vile fedha walizofungulia akaunti walikuwa wamezikopa kwa imani ya kupewa mikopo ambayo ingewainua uchumi.

Naye Dk. Kafumu alikiri kuahidi mikopo kwa vikundi hivyo lakini akasema hawezi kuitoa kwa kuwa yeye si mbunge tena wa Igunga.

“Siwezi tena kutoa mikopo kwa vikundi hivyo kwa sababu mimi si mbunge tena wa Igunga. Hata hivyo kuna baadhi ya vitu nilivyokuwa nimetoa katika jimbo hili vinatosha, siwezi kuongeza tena kitu chochote,” alisema Dk Kafumu.

Mwezi uliopita, mahakama Kuu kanda ya Tabora ilimvua Ubunge Dk Kafumu kutokana ukiukwaji wa taratibu na sheria za uchaguzi zilizofanywa na baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM na serikali

 

Lakini, aliwahamasisha hao Wananchi kuunda hivyo VIKUNDI... Kweli hawezi kwenda kwenye chama chake CCM kilivyo na PESA za

kufanya Party DC na kupeleka DIAMOND hela za hivyo VIKUNDI? Sababu iwe isiwe CCM itashiriki CHAGUZI zijazo hata kama Dr.

Kafumu atakata kona hakuwa Mwanasiasa; ilikuwa Njama ya kumuondoa kwenye CHEO CHAKE PALE WIZARANI; ni kumpa

UBUNGE...
 
hasira hasara dalali kafumu. yaaaani unamuharibia mgombea ubunge ajaye wa magamba akose kura eeeh! wape pesa yao hao wanavikundi ulowahaidi ndio siasa hiyo usizile.
 
Hao wananchi wajifunze! Ahadi za mbunge ziwe za taasisi ya ubunge na sio mtu binafsi. Mfano, kupewa mikopo kutoka kwenye mfuko wa jimbo. Upuuzi wa kumtegemea mtu ndio unawagharimu.
 
Sasa ndiyo wataijua vizuri serikali yetu ya CCM. Siku nyingine wasifanye makosa ya kusikiliza ahadi hewa.
 
Teh....teh....kuachwa kubaya....pumbavu kabisa siwalikua wanamwaga mikwara na ahadi feki
 
Liwalo na liwe..........na mkome kabisa Wana igunga mliponzwa na mahindi ya msaada tena yaliyo oza Tehe Tehe Tehe safi dalaly!
 
Kulikuwa na tetesi kuwa kafumu hataki kukata rufaa na alikuwa na safari ya nje ya nchi kwa ajili ya kuchukua vifaa vya kuanzisha mgodi mdogo na kuachana na siasa,kwa wenye updates je ameshakata rufaa?
 
Hao wananchi wajifunze! Ahadi za mbunge ziwe za taasisi ya ubunge na sio mtu binafsi. Mfano, kupewa mikopo kutoka kwenye mfuko wa jimbo. Upuuzi wa kumtegemea mtu ndio unawagharimu.

nakubaliana nawe. Si kwa ubunge tu hata urais na tuingize kwenye katiba na huu ndio muda muafaka jamani
 
Mwacheni kafumu anamadeni mengi sana mahakamani kulipia gharama za kesi
 
“Siwezi tena kutoa mikopo kwa vikundi hivyo kwa sababu mimi si mbunge tena wa Igunga. Hata hivyo kuna baadhi ya vitu nilivyokuwa nimetoa katika jimbo hili vinatosha, siwezi kuongeza tena kitu chochote,” alisema Dk Kafumu.

Kwani kilichomsukuma kutoa hiyo mikopo ni ubunge au mapenzi aliyonayo kwa wananchi wenziwe? Wababaishaji utawajua tu!
 
hajui siasa huyu! alitaka kuchumia tumbonitu. wengine wanatoa hatakama sio wabunge, but wanaangalia mbele. hata kama sio kesho, kesho kutwa unaweza kugombea tena ubunge
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom