Dk. John Pallangyo ameapishwa leo Mei 22, 2019 kuwa mbunge wa Arumeru Mashariki

wakatanta

JF-Expert Member
Feb 5, 2018
2,593
3,148
Dk John Pallangyo ameapishwa leo Jumatano Mei 22, 2019 kuwa mbunge wa Arumeru Mashariki (CCM) kuchukua nafasi ya Joshua Nassari (Chadema) aliyepoteza sifa za kuwa mbunge.

Dk Pallangyo ameapishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai huku wabunge wa CCM wakimsindikiza kwa mbwembwe na kuimba nyimbo za CCM, wakati wakimsindikiza.

Mara baada ya kuapishwa alikwenda kusalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Wenye Ulemavu.

Baadaye alihamia upande wanapokaa wapinzani na kusalimiana na Kaimu Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Joseph Selasini na Mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika ambao kwa pamoja waliteta kidogo kama sekunde kadhaa.

Kisha mtumishi wa Bunge alimpeleka eneo ambalo atakuwa akikaa.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom