Dk John Magufuli kutulisha vibudu xmass si vizuri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk John Magufuli kutulisha vibudu xmass si vizuri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Dec 25, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,136
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  WAKATI NIKIANDIKA HAYA NATUMAINI KABISA NDG MH DK MAGUFULI KIONGOZI ULIEKAMATA MOYO WANGU KWA UWADILIFU LAKINI HILI LA KULISHA VIBUDU SIKUUKUU YATIMA SI VYEMA,,NATUMAINI HATA WEWE UTOWEZA KUKUBALI NDUGUYO AKILA SAMAKI ALIEKAA MWAKA KWENYE BARAFU...NADHANI KUNA UMUHIMU WA KUWAOMBA WAFUNGWA,MAPOLISI,YATIMA MSAMAHA KABLA YA MWAKA MPYA KWA HAYA YALIYOFANYIKA


  Samaki wa Magufuli wageuka kitoweo cha Krismasi Dar[​IMG]Na Festo Polea

  BAADA ya kutokea kwa mapingamizi mbalimbali za kuzuia tani 296.32 za samaki waliokamatwa kutokana na kuvuliwa kwa njia haramu katika fukwe za bahari eneo la Tanzania maarufu kama ‘Samaki wa Magufuli’ leo zimegeuka kuwa kitoweo cha sikukuu ya Christmas baada ya kugaiwa jana kwa baadhi ya taasisi ambazo hata hivyo zilionekana kususua kuchukua samaki hao kutokana na kukosa vifaa vya kubebea.

  Zoezi la ugawaji wa kitoweo hicho lililoanza kwa kusuasua huku walengwa wakionekana kutokujua kilichokuwa kikiendelea eneo la ugawaji kjwani walionekana wakirandaranda huku na huko bila kuwa na magari ya kubebea samaki hao.

  Zoezi hilo lilianza jana mchana katika kiwanda cha kuhifadhia samaki cha Bahari Foods kilichopo Mwenge jijini Dar es salaam ambapo Tani 26 ndizo zilitarajiwa kugaiwa na wawakilishi wa vituo vya kulelea watoto yatima ndiyo walioonekana kuchangamkia kwa haraka haraka kuchukua samaki hao huku wengine wakiwemo jeshi la polisi wakibaki kutafuta magari na vifaa vya kubebea samaki hao.

  Ugawaji wa samaki hao ulipangwa kwa Jeshi la Wananchi Tanzania kupata tani 10, Jeshi la Magereza kupata tani tatu, Tani mbili kwa Jeshi la Polisi na tani moja kwa Chuo cha Uvuvi Mbegani.

  Taasisi nyingine zilizopangwa kupata samaki hao jana ni Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ambayo ilitakiwa kupata tani tatu, Vituo vya kulelea watoto yatima tani sita, Chuo Kikuu cha Dar es salaam tani moja na nusu tani kwa Chuo cha Utalii, ambapo hata hivyo baadhi ya taasisi ziliomba hudhuru ya kutochukua samaki hao jana hadi kesho kwa kuwa hawakuwa na vifaa vya kubebea samaki hao.

  Kabla ya ugawaji huo wa jana taasisi mbalimbali za uma na serikali 115 zilizopita katika mchujo wa kuomba samaki hao baada ya Serikali kuamua kuwagawa bure samaki hao kutokana na agizo la mahakama la Oktoba 5 mwaka huu na la Oktoba 20, iliyoitaka serikali kuwauza samaki hao au kugawa kwa wananchi wake bure kwa zilikwama kutokana na kutokea kwa vipingamizi vingine vilivyozua sababu mbalimbali zikiwemo za kutokuwa na vifaa.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana kabla ya zoezi la ugawaji wa samaki hao kufanyika, Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, John Magufuli alisema samaki hao wapo katika hali nzuri ya kuliwa kama wananchi watazingatia hali ya afya katika kuwabeba kwenda kwenye maeneo yao.

  Magufuli alisema thibitisho la ubora wa samaki hao limetolewa na wataalamu kutoka maabara ya Nyegezi na pia Mkemia Mkuu alishirikishwa katika kuwapima samaki hao naye ametoa taarifa kuwa wanafaa kuliwa kwa afya za wanadamu bila madhara yoyote.

  “Samaki hao tunaoanza kuwagawa leo (jana) wamethibitishwa kuwa na ubora kwa afya za walaji kutoka kwa mkemia mkuu na ripoti kutoka maabara yetu ya Nyegezi, pia wamehifadhiwa kwa ubora wa hali ya juu na kiwango cha kimataifa cha nyuzi joto (-20).

  Katika hatua nyingine Magufuli alisema samaki hao huhifadhi wa samaki hao hadi jana Sh 1.2 bilioni ndizo zimetumika kwa ajili ya uhifadhi wa samaki hao na kufafanua kuwa kwa siku hutumika Sh 3.5milioni, fedha ambazo hata hivyo alisema hazijalipwa zote kwa wamiliki wa kiwanda hicho.

  “Serikali imegharamia kiasi hicho cha fedha hadi sasa na bado fedha hizo hatujalipa zote, zimelipwa nusu na zilizobaki zitalipwa baada ya zoezi la ugawaji wa samaki hao kukamilika,’’ alisema Magufuli huku akidai kutojali muda wa kumaliza zoezi hilo kwa kuwa kinachotakiwa ni kufanikiwa kwa zoezi hilo.

  Akizungumzia wizi uliokuwa ukifanyika katika bahari ya hindi kwa muda wa miaka 48 waziri Magufuli alisema ulitokana na kutokuwa na sheria za kuwabana wavuvi haramu hivyo kwa kupitia sheria mpya ya uvuvi ya namba ya namba 17 ya mwaka 2007 ambayo regulation yake ni ya mwaka 2009 zitasaidia kukomesha kabisa uvuvi haramu na kuifanya nchi kunufaika na eneo lake la bahari.

  “Kwa miaka 48 tumeibiwa samaki wetu na hivi karibuni ndiyo tumeshika maujizi ya samaki wetu, hapo awali kwa miaka hiyo yote tumeibiwa zaidia ya trilioni kadhaa lakini leo tumewashika tumetumia 1.2bilioni za uhifadhi kwetu siyo hasara ni jambo la kujipongeza kwa kuwa tutanufaika nalo baadae,’’ alisema Magufuli kwa msisistizo.

  Hata hivyo Magufuli aliongeza kuwa kitendo cha serikali kuwashikilia samaki hao kimeipa Tanzania heshima mbele ya mataifa mengine makubwa na januari serikali inatarajia kusaini mikataba ya uvuvi salama katika bahari ya hindi eneo la Tanzania ambapo nchi itaanza kunufaika na bahari hiyo.

  Pia Magufuli aliwataka wananchi wote kuwa walinzi kwa wale watakaogeuza samaki hao kuwa biashara kwa kutao taarifa zao ili waweze kushitakiwa mahakamani kwa kukiuka sheria. Wakati taasisi mbalimbali zikinufaika na samaki hao leo katika sherehe ya Christmas raia 37 ambao ni wa mataifa ya China, Vietnam, Indonesia, Filipino na Kenya waliokamatwa wakivua samaki hao kinyume na utaratibu hadi sasa wako rumande wakisubiri hatma ya kesi yao baada ya kunyimwa dhamana.
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,136
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  WAFUNGWA na wanajeshi ni miongoni mwa watu walioanza kunufaika na shehena ya samaki waliokamatwa na serikali kutokana na kuvuliwa kinyume cha sheria.

  Samaki hao aina ya jodari maarufu kama 'Samaki wa Magufuli' jana walianza kugawiwa bure kwa taasisi mbalimbali ikiwamo Idara ya Magereza, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Polisi ikiwa ni siku moja kabla ya sikukuu ya Krismasi.

  Jodari hao tani 296 inadaiwa walivuliwa kinyume cha sheria na raia 37 wa China, Vietnam, Indonesia, Ufilipino na Kenya Machi mwaka huu. Ugawaji wa samaki hao waliokuwa wamehifadhiwa na Kampuni ya Bahari Food Limited, awali ulisitishwa kutokana na wanufaika kukosa vifaa bora vya kuwachukulia lakini pia pingamizi lililokuwa limewekwa mahakamani.

  Uamuzi wa kuwagawa samaki hao ulitangazwa jana Dar es Salaam na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. John Magufuli, wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuongeza kuwa yeyote atakayekamatwa akiuza samaki hao atafikishwa katika vyombo vya sheria.

  Alisema taasisi zilizonufaika na mgawo kwa jana kuwa ni Jeshi la Wananchi wa Tanzania - JWTZ (tani 10), Magereza (tani3), Jeshi la Polisi (tani 2), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM tani moja), vituo vya watoto yatima (tani 6), Hospitali ya Taifa Muhimbili (tani 3), Chuo cha Uvuvi Mbegani (tani moja), Chuo cha Utalii (nusu tani) na Zanzibar (tani 80).

  Dk. Magufuli alisema tani zote 296 zitagawiwa sehemu mbalimbali hadi zitakapokwisha na serikali imetumia Sh bilioni 1.2 kuhifadhi samaki hao tangu walipokamatwa, ambapo gharama za kuhifadhi kwa siku ni Sh milioni 3.5.

  Hata hivyo, alisema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kuliisaidia nchi na nchi nne zimeshasaini mkataba na Tanzania wa kuvua samaki kwa njia halali.

  “Sekta hii ikitumiwa vyema, inaweza kulipatia taifa pato kubwa sana, kwani nchini inachangia asilimia 1.4 tu ya pato la Taifa wakati nchi kama Namibia inachangia kwa asilimia 40”, alisema Dk. Magufuli.

  Aliongeza kuwa jambo la kushangaza ni Ziwa Victoria hupata fedha nyingi kwa ajili ya mazao ya uvuvi kuliko ilivyo kwa bahari kuu, wakati bahari ni kubwa zaidi.

  Kuhusu usalama wa samaki hao, alisema maabara ya Nyegezi iliyoko Mwanza ikishirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ambao hukagua samaki wanaovuliwa kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi ndio waliothibitisha kuwa wanafaa kwa afya na hawawezi kudhuru.

  Mkurugenzi wa Uvuvi, Godfrey Nanyaro, alisema licha ya kwamba samaki hao wapo katika viwango vinavyotakiwa, ila wasipoangaliwa vizuri wanaweza kuharibika na kuwataka wahusika wanapokwenda kuwachukua, kuhakikisha wanakuwa na vifaa vinavyotakiwa kutokana na kwamba serikali haiwezi kugharamia ubebaji tena.
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Dec 25, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Hivi unajua maana ya neno vibudu??????
   
 4. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #4
  Dec 25, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kama ni hivyo basi watu wa dar wanaokula samaki wa maji baridi wanakula vibudu kila siku, maana samaki wanatolewa mwanza wakiwa kwenye baridi wakati mwingine alifiki international standard kama samaki wa magufuri na watu tunanunua na kula, mimi ninavyofahamu ni kuwa samaki wa magufuli wako salama kuliko samaki wengine wote tunaotumia even kuliko hata tunaonunua soko la ferry kwani kuna wakati unakuta wameoza.
   
 5. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #5
  Dec 25, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,437
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Samaki akihifadhiwa vizuri mara tu baada ya kuvuliwa yaani joto la hasi chinu ya 20 degrees centgrade (-20 degrees centgrade) anaweza kuhifadhiwa kwa zaidi ya miaka 2 na bado akawa anafaa kuliwa na binadamu. Hao wako very fit and safe for human consumption!
   
 6. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #6
  Dec 25, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Pdidy, waache wanokulaga vibudu wale, hata hao wafungwa watakaopelekewa hivyo "vibudu" hawatalazimishwa kula.
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  Dec 25, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mtoa mada nafikiri anamawazo ya mwaka 1947. Akitembelea nchi za watu sijui kama ataweza bei ya fresh fish/meat.
   
Loading...