Dk.Jakaya Kikwete afunguka kuhusiana na kinachokwamisha Afrika

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
4bf9dec72f823e10a94b885acaa8b7c0.jpg
Rais Mstaafu wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amesema uchangishaji fedha kwa ajili ya miundombinu na kilimo ni lazima uende kwa pamoja kwa sababu masuala hayo ni masuala mtambuka kwa maendeleo ya taifa lolote duniani.

Dk. Kikwete amesema hayo leo wakati akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa jijini New York, nchini Marekani, baada ya kushiriki kikao cha ngazi ya juu cha Wiki ya Afrika ambapo masuala ya tabianchi, miundombinu, kilimo na vijana yamejadiliwa.

Dk. Kikwete amesema uchangishaji usiotosheleza wa fedha katika sekta ya kilimo unakwamisha wakulima kushiriki kilimo cha kisasa kwa kutumia mbegu zisizo na ubora na kusababisha wakulima kukosa mavuno yenye tija.

"Ukiendeleza kilimo unasaidia watu wengi sana na umasikini wa Afrika una sura ya vijijini kwamba masikini wengi waliopo Afrika wapo vijijini na tatizo kubwa la kilimo ni kwamba tunatumia dhana za zamani jembe la mkono linatumika zaidi kuliko mashine na mitambo, asilimia 4 tu ya kilimo chetu tunatumia umwagiliaji na mvua ya Mwenyezi Mungu, tatu kilimo chetu hatutumii mbegu bora tunatumia mbegu za asili ambazo hazizalishi sana", alisema Dk. Jakaya Kikwete.
 
Yaani angefunguka kinachokwamisha Tanzania ambapo yeye alikuwa Rais ingekuwa poa mno. Kuliko kuangalia zaidi Afrika kwa ujumla wake.
 
4bf9dec72f823e10a94b885acaa8b7c0.jpg
Rais Mstaafu wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amesema uchangishaji fedha kwa ajili ya miundombinu na kilimo ni lazima uende kwa pamoja kwa sababu masuala hayo ni masuala mtambuka kwa maendeleo ya taifa lolote duniani.

Dk. Kikwete amesema hayo leo wakati akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa jijini New York, nchini Marekani, baada ya kushiriki kikao cha ngazi ya juu cha Wiki ya Afrika ambapo masuala ya tabianchi, miundombinu, kilimo na vijana yamejadiliwa.

Dk. Kikwete amesema uchangishaji usiotosheleza wa fedha katika sekta ya kilimo unakwamisha wakulima kushiriki kilimo cha kisasa kwa kutumia mbegu zisizo na ubora na kusababisha wakulima kukosa mavuno yenye tija.

"Ukiendeleza kilimo unasaidia watu wengi sana na umasikini wa Afrika una sura ya vijijini kwamba masikini wengi waliopo Afrika wapo vijijini na tatizo kubwa la kilimo ni kwamba tunatumia dhana za zamani jembe la mkono linatumika zaidi kuliko mashine na mitambo, asilimia 4 tu ya kilimo chetu tunatumia umwagiliaji na mvua ya Mwenyezi Mungu, tatu kilimo chetu hatutumii mbegu bora tunatumia mbegu za asili ambazo hazizalishi sana", alisema Dk. Jakaya Kikwete.
Hongera JK
 
Mazungumzo na kutenda vingekua sawa tungeshaendelea kitambo sana.
Afrika na wanasiasa wake
Kwa viongozi wa Afrika hilo limezidi kuwatafuna. Na sababu kuu ni kuwa Uchu wa Madaraka ni mkubwa zaidi kuliko Uchu wa Maendeleo

Hivyo kupata maendeleo ni jambo mtambuka
 
Nilijiuliza humu katikati,kwa nn kila kiongozi akipita anaonekana bora kuliko aliyepo?

Kwa kikwete machozi yalikuwepo tu,kwa huyu yy hadi machozi ya damu,,,

Lakin nashangaa anaanza kusifiwa,,,zingatia hata Nyerere waliolia kipindi chake hao hao wanamsifia,

Hivi waombolezaji hawa wanakuwa wanaigiza au?

Au viongozi ndo wanaigiza,kisha wakitoka madarakani ndo wanaishi kwa uhalisia sasa?????
 
Watutafutie Masoko, kulima tunalima sana Sema Serikali ina wivu na wakulima kwa kukataa wauze kwenye bei nzuri
 
Hivi hizi akili wakiingia kule mjengoni huwa wanaziacha mlangoni

Nakumbuka Sera ya kilimo kwanza ilinona na mbwebwe za kila aina uwaziri akapewa wasira wizara ya kilimo,kasi mpya nguvu mpya ari mpya

Mnafiki tu huyu mzee

Matrekta yapo sumajkt dar mkulima anaisha namtumbo
 
Back
Top Bottom