Dk. Hellen Kijo-Bisimba: Awarushia dogo zito Makinda, Ndugai na Wenyeviti wa bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Hellen Kijo-Bisimba: Awarushia dogo zito Makinda, Ndugai na Wenyeviti wa bunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngandema Bwila, Jul 6, 2012.

 1. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2012
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)kimesema Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepoteza mwelekeo na sasalinaonekana kama kituko kutokana na viongozi wake "kuwabeba" wabungewa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwabana wapinzani katika mijadala mbalimbalibungeni.

  Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC,Dk. Hellen Kijo-Bisimba, katika tamko lililosomwa kwa niaba yake na WakiliImelda Urio kutoka kituo hicho.

  Dk. Bisimba alisema kwa sasa hakuna uwiano katika mijadala ya bajetiinayoendelea ndani ya Bunge mjini Dodoma kwa kuwa viongozi wanaowaogoza wabungewameonekana wazi kufanya upendeleo kwa wabunge wa CCM.

  Aliwataja viongozi hao kuwa Spika wa Bunge na Naibu wake pamoja na wenyevitiambao wamepewa dhamana ya kuongoza vikao.

  Aliwataka viongozi hao kubadili mitizamo yao ili kutoa fursa kwa wabungekujadali kwa uwazi hoja kwa faida ya wananchi badala ya maslahi ya vyama vyao.

  “Tunawataka wabunge watekeleze majukumu yao ipasavyo na kulirudishia heshimaBunge la 10 kama lilivyokuwa Bunge la Tisa, Bunge la sasa limepoteza mwelekeona kuonekana kama kituko mbele ya jamii inayowaangalia,” alisema katika tamkohilo.

  Aidha, LHRC kimewataka wabunge kuachana na utaratibu wa kutumia muda mwingikutoa salaam pamoja na pole kwa kuwa jambo hilo ni kinyume cha kanuni namba151(1)-(4).

  Dk. Bisimba alisema kama kuna jambo la kutakiwa kutoa pole ama pongezi, Spikaanaweza kufanya hivyo kwa niaba ya wabunge badala ya mbunge mmoja mmoja kufanyahivyo kiasi cha kutumia muda mwingi ambao angeutumia kutoa mchango wake katikamijadala.

  Kasoro zingine zilizoainishwa katika tamko hilo la LHRC ni pamoja na wabungekuendelea kutumia lugha za kuudhi, kuzomeana na kutaka miongozo bila sababu zamsingi kinyume cha kanuni namba 64 (1) (g).

  “Bado tunaona lugha za matusi na za kuudhi zikiendelea kutolewa na wabungekatika vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini Dodoma na hili jambo linatakiwakukomeshwa,” alisema.

  Aidha, Dk. Bisimba alisema mahudhurio ya wabunge katika vikao vinavyoendeleabungeni ni hafifu na kwamba jambo hilo ni kinyume cha kanuni namba 143(1), nakwamba mara nyingi viti vimeonekana kuwa vitupu bila watu.

  Jumatatu na Jumanne wiki hii hali ya hewa bungeni ilichafuka baada yaMwenyekiti Sylvester Mabumba, kuonekana dhahiri akiyumba kwenye kiti wakati wakikao cha Jumatatu jioni hali iliyozua msuguano mkali na baadhi ya wabunge.

  Hali kama hiyo nusura itokee tena Jumanne katika kipindi cha baada ya maswalihadi mchana wakati wa mjadala wa makadirio ya Ofisi ya Makamu wa Rais.


  May take: Mama Makinda ni zaidi ya Kichuguu dhidi ya Kilimanjaro katika kuongoza Bunge. CCM ijifunze kuwapa nafasi watu wenye UWEZO badala ya vilaza wenye mtizamo wa kichama dhidi ya maslahi mapana ya Taifa.
   
 2. a

  afwe JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Hakuna alichoongopa. Ni ukweli mtupu
   
 3. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Hawachelewi kumwita msaliti,... magamba wengi wanafikiri kwa kutumia kile kiungo
   
 4. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Hii ripoti ndo ilikuja baada ya wanaharakati kufuta maandamano? Mama Bisimba naye ni msanii. Kauli nyingi ila hatua hamna

  Its time hawa activits waende next step forward ya ku take actions ili na sisi tujifunze kwao. Ila kutoa matamko wanatujazia server zetu bure
   
 5. p

  popobawa2012 Senior Member

  #5
  Jul 6, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kwa kweli
   
 6. K

  Kiboko Yenu JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 312
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  huyu mama huwa anajiona ana impact kwenye jamii ya wtz kumbe hakuna lolote
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Watanzania tukubali kwa miaka 5 (2010-2015) hatuna bunge ila tuna mikutano ya wana-CCM na serikali ya CCM. Nirejee kilio changu cha siku zote kwamba Spika Anne Makinda ameguza bunge kuwa idara ya serikali na ndio maana nasema wananchi hawana tena uwakilishi na kwa hakika serikali haina msimamizi kwa maana ya bunge.

  Nilijaribu kufuatilia wakati wa majumuisho ya hotuba ya Waziri wa fedha Dr Mgimwa na Naibu wake. Naibu Waziri alikuwa mtu wa kwanza kuongea na alitumia takriban dakika 7 kama si zaidi kushukuru/utangulizi kabla ya kujibu hoja za wabunge. Funga kazi alikuwa Dr Mgimwa ambaye alitumi si chini ya dakika 29 (29 minutes!) kushukuru na kusoma majina- moja baada ya jingine- la wabunge waliochangia. Alisoma majina zaidi ya 100! huku wabunge wakipiga meza kila anaposoma jina la mbunge! Huu ni ujuha lakini tunaambiwa ni bunge!

  Mtindo huu wa kushukuru wake, waume, watoto, wapiga kura, Spika/naibu spika etc kwangu mimi ni DHULMA kwa wapiga kura. Na hili liko kwa wabunge wa pande zote. Ukipitia Speech zao utaona family issues. Nimejaribu kuangalia speeches za wabunge wa nchi nyinge na sikuona huu ushenzi wa kushukuru. Kwa mkulima anayetaka mbolea, au mgonjwa aneyehangaika kupata matibabu shukurani kwa spika zinamsaidia nini? Na inakuwaje mbunge anashukuru wapiga kura wake miaka 2 baada ya uchaguzi? Waliwatuma bungeni kushukuru?

  Hata hivyo nawalaumu wabunge wa CCM walioona kuwa mtu anayefaa kuongoza chombo hiki cha juu kabisa na chenye mamlaka ya kuismamia serikali ni Anne Makinda na Naibu wake Job Ndugai wakisaidiwa na wenyeviti style ya Mabumba. Hawa ndio viongozi wanaotegemewa kuongoza wawakilishi wa wananchi ili Tanzania iweze kushindana na nchi zingine ndani na nje ya Afrika Mashariki! Hawa ndio viongozi wanatakiwa kuongoza mijadala itakayoleta mageuzi kwenye utendaji kazi wa serikali na idara zake. Hawa ndio viongozi wanatakiwa kuongoza usimamizi wa serikali ili malengo ya mpango wa maendeleo ya miaka 5 (2011-16), MKUKUTA na Vision 2025 yafikiwe!

  Mpaka sasa hivi najiuliza, wabunge wa CCM wameridhika na uendeshaji wa vikao vya bunge? Nasema wabunge wa CCM maana wako wengi na ndio wenye nguvu kubadilisha chochote ndani ya bunge.

  Mwisho,Ningetaka kujua nani Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii inayohusika na sekta ya afya? Na ningetaka kujua mamlaka ya wenyeviti wa bunge. Nini maoni yake kuhusu upatikanaji wa huduma za afya nchini? Najaribu kurejerea kanuni za mabunge yanayofuata mfumo ya Westiminster Tanzania ikiwepo. Na kwa hali ilivyo sasa wabunge wameridhika kabisa kuwa wanawakilisha wananchi kwenye huu mgogoro ndani ya sekta ya afya? Narudia, wabunge na hasa wale wa CCM wanaridhika na role/untendaji wao kwenye huu mgogoro ndani ya sekta ya afya?

  Kwa maneno mengine, wabune wanasimama upande upi, wa wananchi au wa watuhumia -serikali? Na watanzania tuendelee kuamini kuwa tuna wawakilishi wanaotupigania? Niko MOI
   
 8. sifongo

  sifongo JF-Expert Member

  #8
  Jul 6, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 4,597
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  Ameongea ukweli, Mheshimiwa Makinda bunge limemshinda kabisa, sio yeye wala wasaidizi wake kila anayetizama bunge anajua kabisa wabunge wa upinzani wanakandamizwa, lakni asidhani kwamba hivyo ndivyo anavyosidia chama chake la hasha! ukweli ni kwamba anazidi kukidumaza sababu kinashindwa kukabiliana na changamoto zinazoletwa na upinzani, serikali inabweteka sababu inajua Makinda atatumia kiti kuwakalisha wapinzani wanapoleta hoja za moto.
   
 9. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #9
  Jul 6, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,198
  Likes Received: 10,540
  Trophy Points: 280
  Kijo Bisimba huyu mama ni jembe sana.
   
 10. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #10
  Jul 6, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kwa mtu makini na mwenye uchungu na nchi hii, huwezi kufuatilia mijadala ya bunge linaloendele hivi sasa kwa dakika 10 bila kupata hasira. Wabunge wa upinzani wananyanyaswa sana pamoja na mawazo mazuri wanayoyatoa.
   
 11. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #11
  Jul 6, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  spika anajifunza sheria za bunge, wabunge wa ccm wanajifunza kupitisha hoja na kuziunga mkono zaidi ya waliozileta.
  Wabunge wa upinzani wanajaribu kutetea walalahoi.
   
 12. B

  Bob G JF Bronze Member

  #12
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Watanzania wanayaona hayo ya ccm kutumia uwingi wake kukandamiza Upinzani hasa CDM, Na taarabu zao adhabu ni 2015 mwiho wa ccm
   
 13. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #13
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Wanaharakati siku zote sio wazalendo, ili kutimiza malengo ya wafadhili wapo tayari kuuza utaifa wao. Tuwaogope kama ukoma.
   
 14. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #14
  Jul 6, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Pamoja na mambo mengine, ukweli una baki kuwa mama makinda bunge limemshinda.
   
 15. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #15
  Jul 6, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  huyu helen uzee unamhangaisha tu..
  Hana chochote
  tuna matatizo makubwa zaidi kuliko kujionesha kupata umaarufu na kutaka vijisenti vya wazungu..kusaidia ulaji wa ngos zao
  kuna daktari aliuliwa mbeya 2011 hatukumsikia huyu...na aliuliwa na wafanyakazi wenzake inasemekana
  kuna kesi za walio fukiwa kwenye migodi hawa walikua kama wametiwa maji ya baridi
  hapa tatizo kubwa lipo kwenye madini lakini hawa hata siku moja huwasikii kulaaumu haya kwani hawo wazungu ndio wanawapa mgao na ngo yao
  asitubabaishe
   
 16. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #16
  Jul 6, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  kweli kabisa hana mvuto na hakuna anaemjali...akalee wajukuu
   
 17. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #17
  Jul 6, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  huwa sioni tofauti ya hii mihimili mitatu. Naona serikali ni remote, bunge ni kama screen na mahakama ni kama dvd player. Huyu remote anafanya analotaka kwa screen na dvd player
   
 18. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #18
  Jul 6, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,957
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  hongera mama, ningefurahi iwapo ungesema kuwa huyu makinda na ndugai ni wapu*uzi na wa*pumbav
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Jul 6, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,773
  Likes Received: 83,114
  Trophy Points: 280
  Mkuu FJM labda ungeongeza kuanzia 2000 mpaka 2015. Nakubaliana nawe kabisa kwamba hatuna Bunge maana kuangalia/kusikiliza yanayojiri ndani ya Bunge hili uchwara unaweza kusikia kichefuchefu cha hali ya juu kwa yale yanayofanywa na Wabunge wa magamba.
   
 20. M

  Mbuyi Member

  #20
  Jul 6, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 13
  Issue hapa sio kumjadili Bisimba,issue ni uendeshaji wa Bunge! Je, hivi ndvyo ulivyotegemea bunge kuwa? Mimi naunga mkono muono wake wa Bisimba,tena hapo awali wakati walivyomteua mama kuwa spika nilikuwa nasema, kama issue ni 'awamu ya mwanamke'(kama kweli)! basi bora angekuwa Jennister,lkn sasa naghairi na kufuta kabisa kauri yangu kwa kuwa,ktk true colour yake, namuona ni bomu kuliko wote waliopo! na ukimuangalia anavyoongoza, usoni anaonyesha hata nafsi yake inamsuta! Ama kweli Tz kwa bunge hili la mipasho na kuminyiana kwa maslahi ya chama badala ya wananchi, bado tuna kazi ya kufanya kufika pale tulipochelewa kuwa.Mungu ibariki Tz,Amina.
   
Loading...