Dk. Hassan Kitine dhidi ya Upson Mwang'onda kuelekea 2015

Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,067
2,196
Wakuu katika hali ambayo si ya kushangaza sana, wiki hii tumeona two heavyweights waliokuwa wakuu wa TISS wanatia uzito wao kwenye uchaguzi 2015.

Inaanza kuonekana wazi kuwa kwa sasa ni kama ndoto ya Urais ya Kitine imeyeyuka kabisa, baada ya kufanyiwa zengwe huko nyuma. Kwa hiyo ni kama sasa anataka kuweka uzito wake, na kusema ni nani anafaa kuwa Rais wa Tanzania, na nani hafai. Alieleza mambo kama sita au saba hivi ambayo ukiyatafisri unaoweza kuona yanamlenga kabisa mtu fualni, na unaweza kuhisi kuwa he is a bitter opponent of EL's bid (this is my personal view, he did not say that). Been asking whether he is doing this just to pave a way for a candidate who he knows will help him deal with waliomfitini, or it is for the good of Tanzania.

On the other hand, it is becoming increasingly obvious that Mzee Mwang'onda has thrown all his weight on EL's bid for reasons that not many know. Sidhani kama inaweza kuwa ni uchungu wa mwanaye kuzuia na baadhi ya watu uliofanya kushindwa kupanda rank ndani ya CCM, au kuna picha kubwa anayofikiria ambayo anadhani inaweza kutekelezakea EL akiingia madarakani.

Lakini hii kidogo inanifanya nijiulize kama kweli TISS hawana moja wanachojua kuwa wanataka rais wa namna fulani. Yaani hawajui as institution, which candidate will enable them to be a 21st Intel agency, that can match or surpass regional intel agencies, au watakuwa happy kuwa na kiongozi ambaye ataifanya idorore na kuwa last before Somalia.
 
mtifuano CCM unaendelea kama kawa kabla ya kuanzishwa New episode.
 
Usalama wa taifa nao wanangojea upepo uvume. Tatizo la nchi hii kwa sasa kila mtu amekuwa ni mbinafsi kiasi kwamba hatufikirii tena jinsi ya kusukuma gurudumu la maendeleo lisonge mbele. Usalama wa taifa una mafaili ya viongozi wote na kama ni nani msafi wa chama chochote wanamjua na hao ndio wanantakiwa wajulikane wapigiwa kura za maoni tupate wagombea safi.
 
Kuna wanaopiga mayowe na kuna wanaofanya kazi usiku na mchana ili mambo yaende. Naamini kuwa TISS wanafanya kazi zao kwa mujibu wa majukumu na taaluma zao. Hao wastaafu aendelee na mipango yao ila mwisho wa siku Watanzania ndo wanajua nani wa kumchagua
 
Usalama wa taifa nao wanangojea upepo uvume. Tatizo la nchi hii kwa sasa kila mtu amekuwa ni mbinafsi kiasi kwamba hatufikirii tena jinsi ya kusukuma gurudumu la maendeleo lisonge mbele. Usalama wa taifa una mafaili ya viongozi wote na kama ni nani msafi wa chama chochote wanamjua na hao ndio wanantakiwa wajulikane wapigiwa kura za maoni tupate wagombea safi.

Mkuu kuna kitu huwa tunasahau sana tunapojadili mambo ya nchi yetu. Hawa jamaa wa usalama wa taifa tunatakiwa tuwasaidie kwa kupitisha sheria zinazofaa na kuwa-equip kisawasawa ili waweze kuilinda nchi hii vizuri zaidi na waingie kwenye field ya uchumi walau na sisi tuwe formidable force. Inabidi rais ajaye awe na plan nzuri kwa TISS na hata TISS establishment iwe na clear picture ya nani wanamtaka. Hii ya maboss waliopita kuwa na maoni tofauti kidogo inasumbua.
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Tatizo ni kutoaminiana tu ....... kama idara lazima wanajua ukweli halisi na weakness ya kiutawala na mtu wa aina gani anafaa .......lakini hata hao wakuu sidhani kama wanaweza kuamini taarifa kutoka huko ili wasimamie taarifa hizo zenye takwimu za kiweledi ....... hawa walipaswa kuitwa kupewa facts za hapa tulipo kama taifa ili nao watoe mchango wao then wakae kimya ........... misimamo yao mwisho wake ni kugawa taifa tu ........
 
Mkuu, kwa mtazamo wako unataka Usalama wa Taifa wadisclose taarifa za wanasiasa wote nchini? Hao watakuwa usalama wa taifa au maadui wa taifa? Kama wakifunua kila kitu, unafikiri nini kitatokea?
 
Mkuu, umeeleza mambo ya msingi sana. Nakuunga mkono
 
Mkuu, kwa mtazamo wako unataka Usalama wa Taifa wadisclose taarifa za wanasiasa wote nchini? Hao watakuwa usalama wa taifa au maadui wa taifa? Kama wakifunua kila kitu, unafikiri nini kitatokea?

Tumia akili hii mada sio bavicha vs uvccm!!!!
Wanasiasa wakiwekwa wazi "usalama wa taifa" unatingishikaje kwa mfano???!!
Hizi siri ndio zinaleta makundi sasa sababu kila mwenye madudu anataka awe na wa kumfichia huu ndio mtikisiko wa "usalama" sasa!!!

Wanatakiwa wawe wazi ndio "uadilifu" kupitia "tume" utafanikiwa
 
Tatizo idara ya Usalama wa Taifa imegeuzwa na CCM kama moja wapo ya vitengo vyake vya Propaganda,sitaki kuamini hawa wastaafu wameanza kupiga hizi propaganda baada ya kustaafu,no,they were doing it before kwa kujificha ficha wakiogopa kuzodolewa maana ni kinyume kabisa na taratibu za TISS
 
Mkuu, mbona mnavyoelezwa madudu ya Apson na Lowasa mnakuja juu?
 
Mkuu kuna kitu huwa tunasahau sana tunapojadili mambo ya nchi yetu. Hawa jamaa wa usalama wa taifa tunatakiwa tuwasaidie kwa kupitisha sheria zinazofaa na kuwa-equip kisawasawa ili waweze kuilinda nchi hii vizuri zaidi na waingie kwenye field ya uchumi walau na sisi tuwe formidable force. Inabidi rais ajaye awe na plan nzuri kwa TISS na hata TISS establishment iwe na clear picture ya nani wanamtaka. Hii ya maboss waliopita kuwa na maoni tofauti kidogo inasumbua.

Katiba , katiba, katiba!!!!!
 
Tumia akili hii mada sio bavicha vs uvccm!!!!
Wanasiasa wakiwekwa wazi "usalama wa taifa" unatingishikaje kwa mfano???!!
Hizi siri ndio zinaleta makundi sasa sababu kila mwenye madudu anataka awe na wa kumfichia huu ndio mtikisiko wa "usalama" sasa!!!

Wanatakiwa wawe wazi ndio "uadilifu" kupitia "tume" utafanikiwa
Mkuu, kwanza nikuhakikishie kuwa akili nilizotumia zinazidi uwezo wako kufikiri. Wewe unalishwa tu maneno ndo maana haupo consistance kwenye kuandika. Umetaja maneno tume na uadilifu bila ya kujua maana yake. Pole sana ndugu. Kajipange upya
 
Inawezekana unatumia akili lakini kwa lengo gani????!!!!
Ndio maana nikasema hii ni politics from intelligents for intelligents!!!!
Hii sio "majitaka"!!!!!!

Yaani huwezi ona string between tume na uadilifu kwa muktadha huu???!!!
 
Tatizo idara ya Usalama wa Taifa imegeuzwa na CCM kama moja wapo ya vitengo vyake vya Propaganda,sitaki kuamini hawa wastaafu wameanza kupiga hizi propaganda baada ya kustaafu,no,they were doing it before kwa kujificha ficha wakiogopa kuzodolewa maana ni kinyume kabisa na taratibu za TISS
Mkuu, binafsi naamini kuwa TISS kama taasisi inaundwa na watu ambao wanakuwa na utashi wao kisiasa. Ni sawa na TFF. Wote wanaochaguliwa kuongoza TFF wanaweza kuwa na mapenzi na ama na Simba au Yanga. Ila miiko ya kazi inawwfanya waweke pembeni mapenzi yao. Vivyo hivyo kwa TISS. Naamini kuwa wapo wenye mapenzi na CCM na wengine Upinzani. Ila inavyokuja kwenye suala la kazi, naamini kuwa mapenzi ya vyama yanakaa pembeni. Kumbuka kuwa watumishi wa TISS hawajaletwa toka mbinguni. Wamezaliwa Tanzania kwenye jamii ya kitanzania na wanaishi na watanzania kwa vile wao ni watanzania na siasa za Tanzania zinawasthiri
 
Hivi sheria ya TISS inasemaje kuhusu wastahafu kujiingiza kwenye siasa moja kwa moja?
 
Hakuna usalama wa taifa bongo hii pale kumejaa wachuuzi tu wa kawaida,kila mtu ni msaka tonge sasa kwa mazingira hayo hata usalama wenyewe upo wapi hapo?
 
Hii quote yangu??!!

Must be a misdestination
Wewe kaka una hasira sana. Kwani haiwezekani ukajibu quotation ya mtu mwingine? Na je ni vipi mjadala utaendelea kama unataka kila hoja ijibiwe na aliyeulizwa. Hoja za humu nyingi ni za general. Kila mtu anaweza kujibu. Kama Lizaboni angeulizwa specific issue kama ana umri gani, hapo nisingeingia
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom