Dk. Hamis Kigwangalla: Kima cha chini cha madaktari kiwe TZS 3.5 milion | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Hamis Kigwangalla: Kima cha chini cha madaktari kiwe TZS 3.5 milion

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mhondo, Jan 21, 2012.

 1. m

  mhondo JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Dk. Kıgwangalah ana/amependekeza kıma cha chını cha mshahara wa madaktarı kıwe tsh. 3.5 mılıonı na walıpwe posho ya shılıngı lakı 2. Akaendelea kusema kwa kuwa udaktarı nı kazı ya wıto. Je nı sahıhı kudaı kıası hıcho cha mshahara na posho na wakatı huo huo kusema udaktarı nı kazı ya wıto?.
  Source : www.vıewtz.com habarı ınasema matıbabu yasımama hospıtalını.
   
 2. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ni sahihi kabisa

  Kuhusu wito waulize "Manabii/Mitume" unaowajua....
   
 3. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  3.5mil/month i think is stll a chicken feed.
  Nchi haitaweza kuzuia madokta kukimbia kwenda botswana, namibia, swaziland hata kama hali ndo hiyo
   
 4. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kwanza wewe unaonaje mkuu?
  Mimi nionanyo hii kazi ni wito hapa kwetu, lakini nchi nyingine hii ni profesion inayohitajika?
  Lakini pia ni vema tukajiuliza ikiwa mwenye wito hali, hahitaji kuishi katika, hahitaji kuheshimiwa au yeye haathiriki na ugumu wa maisha na mfumuko wa bei?

  Vitu vingine sio lazima kuingia kwenye ligi, ni swala la kutumia akili tu. Mimi ningeulizwa kazi ya wito, ningesema urais, ubunge na uongozi ktk maswala ya kidini.
   
 5. m

  mhondo JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Ukısema nı wıto nafıkırı ıtabıdı urıdhıke na unachopata au ulıchopangıwa.
   
 6. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #6
  Jan 21, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kwa tafsiri hii boss, nahisi kabisa kujisaidia haja ndogo.
  Kwa hiyo boss ni haki ya watumishi hawa tu kuridhika na wanachopata au wanachopangiwa. So, TRA, TANAPA, JWTZ, Usalama wa Taifa nk. wao wanaruhusiwa kutoridhika na wanachopata au wanachopangiwa. Kwa maneno mengine wao hawatakiwi kufanya kazi kwa wito, sio?
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Jan 21, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ni haki na ni sahihi kudai maslahi mazuri kutokana na kazi yako hasa taaluma kama hizi.lakini nina wasiwasi na uwezo wa kufikiri wa mh.Kigwangala.namheshimu lakini namshangaa kidogo kwa hoja zake tata za mara kwa mara.sijui anaishi katika ulimwengu wa kufikirika?

  Anapopendekeza kima cha chini 3.5M wakati 315,000 imeshindikana anakuwa anaota au anavuta bangi za kujificha.
   
 8. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #8
  Jan 21, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu umenifurahisha kidogo usiku wa leo.
   
 9. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #9
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,127
  Likes Received: 3,315
  Trophy Points: 280
  Huyo kweli kigwalagwalagwala.
   
 10. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #10
  Jan 21, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  nampenda kigwangalla kwa misimamo yake thabiti juu ya madaktari
   
 11. b

  balzac Member

  #11
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 85
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  mbona unamkosoa mwenzio nawewe unaonesha kiwango kidogo cha uelewa? HK amezungumzia kiwango cha chini wanachotakiwa kulipwa ma-daktari,kwa scale yao si kima cha chini cha mshahara (kcc) unachozungumzia wewe cha 315,000 abacho wanalipwa wale wasio na skills kama wafagiaji
   
 12. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  wito ni pale we unaponieleza matatizo yako na mke wako aafu mi nikaweka siri. Aafu kitendo cha kukutana na watu wenye different difficulties na kuwasikiliza kila matatizo yao ni wito. Sio kuniambia mi nitembelee TZ 11 miaka yote ndo wito! Hata kwenye kiapo kuna mstari unasema NIISHI KWA AMANI NA FURAHA.
   
 13. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #13
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  wanajiangalia wao tu hizo fedha zitapatikana wapi kuwalipa wkt kuna huduma zingine pia hakuna fedha?
  na mahakimu nao walipwe ngapi? je wakuu wa mikoa,wachumi,nk?
  mshahara unaendana na cost of living,je walimu nao walipwe sh ngapi?
  Tanzania bado hatujafika huko uwezo bado mdogo,angesema walau 1.5m kwa wanaoanza ningemuelewa.
   
 14. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #14
  Jan 22, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  kama vipi madaktari walipwe kwa kila kichwa wanachokiona(every single patient wanaomuattend)
  hii itaongeza tija na ufanisi wa kazi.mfano kila mgonjwa unayemuhuduma unalipwa sh 5000.
   
 15. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #15
  Jan 22, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,141
  Trophy Points: 280
  Na kima cha chini kwa mfanya kazi wa kawaida kiwe kwa uchache Million 1.
   
 16. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #16
  Jan 22, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,141
  Trophy Points: 280
  Jamani Million 3.5 kwa madaktari ni ndogo sana tena sana. Mimi ningeonelea kwa uchache wangeanzia mshahara wa Million tano kwa waliomaliza "intern" na million 7.5 kwa waliomaliza miaka 3 ya ajira. Na wauguzi wangeanzia Million 1.

  Hapo hata wakifanya uzembe wanajuwa nikiwachiswa hapa nimekosa mengi. Na ujuvi wa wauguzi utakwisha.
   
 17. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #17
  Jan 22, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Tatizo letu Tanzania ni kwanza ubinfasi na kingine ni SIASA ndio ajira inayolipa zaidi kuliko utendaji.......

  kiwango Anachopendekeza Dr kingwala kinaweza kuwa kidogo sana au kikubw lakini Ninaona amesema hivyo kwa ubinafsi zaidi yeye kama Dokta mwenzao. Let say kuanzia mwezi ujao madkari wanalipwa 3.5 anazopendekeza Kingwala.. Wakaanza ugoma walimu waliomaliza Vyuo Vikuuu. kingwala atasema walipwe shiligi ngapi? Baadae wakigoma Wahandisi na wanasheria waliomaliza Chuo Kikuu Dr kingwala atapendekeza walipwe shilingi ngapi?
  Hapo hapo anasema Udaktari ni wito so kama ni wito nadhani basi hizo 3.5 ni kadirio la chini
  Je
  • madakatari wote wanatambua kuwa hiyo taaluma yao ni wito.(Sidhani) nadhani wengi wanaona udaktaari kama uhandisi
  • Je madkari wanapgoma wanajua wanamkomoa nani au nani anaumia zaidi ?
  • Je daktari wameshindwa mbinu za kuibana serikali juu ya madi yao bila kugoma na kuumiza wagonjwa?

  Na huyu Dr Kingwala turned to politician kwa nini hajawai kuhoji au haoni tatizo bungen SIASA iwe ni ajira na kazi ya umma inayplipa zaidi kuliko utendaji.

  Mimi napenda kumuuliza kingwala. Ni ni haki jimboni kwake wilayani kwakee au mkoani kwake yeye kama mbunge(Mwanasiasa ) kupokea mshaharana stahiki kubwa kuliko
  • Mganga Mkuu wa Mkoa au Wilaya
  • Afisa Elimu Wa Mkoa
  • Afisa Kilimo wa Mkoa
  • Mhandisi wa Mkoa
  • Afisa Mifugo au maji
  • Afisa nyuki
  • RPC
  • etc
  Kama kingwala haoni tatizo na hajawai kuhoji kwa ninii watendaji hao amabao ndio wanatakiwa kuelta mabadiliko kwenye jamii mafao yako chini kuliko wanasiasa ambo wanataiwa kuwa waangalizi then Kingwala ni sehemu ya tatizo na sio suluisho.

  Kam kingwala hajui ukubwa na umuhimu ya mjukumu ya hivyo vyeo na watu hapo juu kuwa ni zaidi ya yale ya wanasiasa kama mbunge basi aache kucheza na kili za watu.
  Kama Kingwala na wabunge wengine wakiwemo na wa Upinzani wajua umuhimu n ukubwa wa kazi ya mganga mkuu na kazi nyinginezo ni zaidi mbunge basi tunatakiwa kuwasikia bungeni wakihoji kwa nini wao mafao yao yanazidi watendaji wanaotakiwa kuleta mabadiliko kwenye jamii
   
 18. D

  DOMA JF-Expert Member

  #18
  Jan 22, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Kweli hilo ni gamba
   
 19. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #19
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kwa mishahara hii dadangu nafikiri nidhamu mahospitalini ingekuwepo na bughudha za manesi tunazozipata zingepungua sana kama siyo kwisha kabisa.
   
 20. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #20
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  sisi si watoto, wala mataahira.
  Huwa tunadai mahala ambapo tunajua kuna uwezekano wa kupata, kama nchi haina hela, mishahara duni ingekuwa kwa kada zote.
  Nafasi za kisiasa zinalipiwa mishahara mikubwa wakati zile za uweledi hakuna kitu. Wasipodai utakuwa ni ujuha!
  Kuhusu Kigwa, anachosema ni sahihi, ingawa pia kuna mgongano wa kimaslahi. Kwanini asiwasemee walimu? Simply kwa kuwa na yeye ni dakitari.
   
Loading...