Dk. Getrude Mongella ahofia kasi ya awamu ya tano, adai huenda ikawaacha wanawake nyuma

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
20,415
2,000
Rais Mstaafu wa Bunge la Afrika, Dk Getrude Mongella, amesema kuwa kasi ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli, inamnyima usingizi kwa sababu huenda ikawaacha wanawake nyuma na kukosa haki yao

Ameyasema hayo wakati akiwasilisha mada ya nafasi ya mwanamke katika Tanzania ya viwanda kwenye kongamano lililowakutanisha zaidi ya wanawake mia moja kutoka sehemu mbalimbali nchini lililopewa jina la Women Roundtable forum

"Magufuli ana kasi ambayo msiokuwa na mbio mtapiga pua chini, akina mama mnalitazama hilo, mimi hili linaninyima usingizi, tukiachwa na mapinduzi haya tutakuwa wageni wa nani, nawaonea huruma wanawake wenzangu na ujuzi wenu "alisema Mongella

Hata hivyo, Mongella ameitaka Serikali kuwaandaa wanawake kitaaluma ili kuweza kushiriki kikamilifu katika uchumi wa viwanda bila kuwafanya wanawake wababaike na kupiga magoti ili wapate haki zao.

Source : Dar24
 
N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
5,065
2,000
Haki sawa 50kwa50 kwa hiyo wapambane twende sawasawa maana tuna haki sawa 50%kwa50% zama za kuletewa mkate mezani zilishajiendeaga
 
Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,229
2,000
Kasi hiyo ipo wapi? Mbona mimi sioni kasi yeyote naona matamko, sifa na kukurupuka.
 
Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
5,815
2,000
Mongela anapaswa kusema ukweli na aache kuzunguka mbuyu kuwa mkuu ni mbaguzi na mnyanyasaji!

Aidha anapaswa kumwambia mkuu kuwa yeye ni mkuu wa wote na siyo watu wake na wapambe wake tu!
 
ibesa mau

JF-Expert Member
Sep 17, 2015
2,113
2,000
Wasiposema ukweli ndio wanaachwa hivyo . Kikwete alijitahidi sana kuhakikisha wanawake anawavuta na alifanikiwa kwa kiasi kikubwa, fuatilia teuzi mbalimbali alizozifanya JK utaona kila teuzi wanawake walikuwepo . Lakini hivi sasa utawala huu hakuna kitu kama hicho, mkuu anaturudisha nyuma hatua nyingi tena kwa kasi ya ajabu. Wanawake wasomi wanaona haya kulisema hili kazi kwao. wanataka sisi wanaume ndio tuwasemee , asiye na mjomba hujijombeza mwenyewe , kazi kwenu
 
kulwa MG

JF-Expert Member
Aug 29, 2016
1,290
2,000
huwa nawashangaa sana vimada wanaposema wanataka haki sawa!!..haki watazikuta mbinguni,duniani hakuna haki..
 
nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,374
2,000
Nilifanya kazi mahala flani na top bosses walikuwa ni wanawake,ilikuwa shida tupu,..walikuwa hawapendani,mashindano hayaishi hadi yalikuwa yanaathiri kazi..na pale nikaconclude kwamba mwanamke mwenye busara ni mama yangu na mama yako wewe na mama yake yule tu!!
 
hapakazit

JF-Expert Member
Dec 8, 2015
718
500
Wasiposema ukweli ndio wanaachwa hivyo . Kikwete alijitahidi sana kuhakikisha wanawake anawavuta na alifanikiwa kwa kiasi kikubwa, fuatilia teuzi mbalimbali alizozifanya JK utaona kila teuzi wanawake walikuwepo . Lakini hivi sasa utawala huu hakuna kitu kama hicho, mkuu anaturudisha nyuma hatua nyingi tena kwa kasi ya ajabu. Wanawake wasomi wanaona haya kulisema hili kazi kwao. wanataka sisi wanaume ndio tuwasemee , asiye na mjomba hujijombeza mwenyewe , kazi kwenu
Kumbe samia tulia na jenister nao ni male
 
Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
4,894
2,000
Rais Mstaafu wa Bunge la Afrika, Dk Getrude Mongella, amesema kuwa kasi ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli, inamnyima usingizi kwa sababu huenda ikawaacha wanawake nyuma na kukosa haki yao

Ameyasema hayo wakati akiwasilisha mada ya nafasi ya mwanamke katika Tanzania ya viwanda kwenye kongamano lililowakutanisha zaidi ya wanawake mia moja kutoka sehemu mbalimbali nchini lililopewa jina la Women Roundtable forum

"Magufuli ana kasi ambayo msiokuwa na mbio mtapiga pua chini, akina mama mnalitazama hilo, mimi hili linaninyima usingizi, tukiachwa na mapinduzi haya tutakuwa wageni wa nani, nawaonea huruma wanawake wenzangu na ujuzi wenu "alisema Mongella

Hata hivyo, Mongella ameitaka Serikali kuwaandaa wanawake kitaaluma ili kuweza kushiriki kikamilifu katika uchumi wa viwanda bila kuwafanya wanawake wababaike na kupiga magoti ili wapate haki zao.

Source : Dar24
Mtu kama huyu sina hata sababu ya kumsikiliza. Alifanya nini yeye wakati ni mbunge na wakati yuko PAP. Hatuwezi kuendelea kwa kupendeleana hata mambo ambayo hayahitaji gender. Awamu iliyopita iliwajaza watu walioishia kufanya mambo ya fashion, hao ndo wawakilishi tunaowataka?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom