Dk Dalaly Kafumu afunika kata ya Mwisi

kupelwa

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
1,087
450
Mgombea Ubunge jimbo la Igunga mkoani Tabora kwa tiketi ya CCM, Dk Dalaly Kafumu akihutubia mkutano wa kampeni jana katika Kata ya Mwisi jimboni Igunga, Uchaguzi wa jimbo hilo unafuatia kujiuzuru kwa mbunge wa zamani wa jimbo hilo Bw. Rostam Aziz. (Picha na Bashir Nkoromo)

attachment.php
 

Attachments

  • 3.jpg
    3.jpg
    70.7 KB · Views: 551
Mwanaume mzima wamemvalisha kanga kama mwali, kweli jamani kura hazina adabu.

Mjomba, sometimes inakuwa ngumu kujua kama kweli ccm inafunika au vipi kwa sababu ya tabia yao ya kubeba makundi ya watu kutoka sehemu moja mpaka nyingine kwahiyo unaweza kukuta nusu ya hao unawaona siyo wakazi wa eneo hilo na halafu wengine wanaweza kuwa wanafuata ubwabwa kofia na mashati ya CCM.

Kuhamisha watu kunaweza kuwafanya CCM wenyewe washindwe kufanya tathmini kamilii ya kukubalika kwao kwa sababu ya kuamisha misha watu. Wangejaribu kutoa matangazo tu ya mkutano kama CHADEMA halafu bila kuamisha watu halafu waone watu wangapi watatokea ili wapate picha kamili ya kukubalika kwao.
 
Kwa mtizamo wangu naona CCM kwa sasa imekuwa kama kumbikumbi mnzee anayetaka kufa kwani huota mabawa ili aruke angani akaliwe na ndege waliopo angani!!! Yani kweli wanaacha kuwasisitiza watoto waende shule wanawapeleka kwenye kampeni kwa mgombea wao aliyevaa kanga??? Lakini labda n dio kasi mpya, ari mpya na kile kingine!
 
Hii picha ni ya siku tatu zilizopita, na wala si ya jana. Jaribu kupata habari live na kufuatilia kinachotokea hapa Jamii Forums vinginevyo unaleta habari na picha ambavyo vilishachuja hapa. Thanks again.
 
Kwa mtizamo wangu naona CCM kwa sasa imekuwa kama kumbikumbi mnzee anayetaka kufa kwani huota mabawa ili aruke angani akaliwe na ndege waliopo angani!!! Yani kweli wanaacha kuwasisitiza watoto waende shule wanawapeleka kwenye kampeni kwa mgombea wao aliyevaa kanga??? Lakini labda n dio kasi mpya, ari mpya na kile kingine!


hivyo vitoto ni vile standard Seven leaver havina kazi ya kufanya sasa hivi...
 
kampeni nyiingi za ccm igunga watoto wanakuwa wengi kwa sababu kuna show nyingi ila wapiga kura ni wachache mno hasa wale wenye nguo za kijani, alafu mzee mzima kavalishwa kanga jamani siasa uchwara zina taabuu! sijui anatoa mtazamo gani kwa wanaume wa igunga mmmh hapana huyu nae atakuwa wale wale!
 
Magamba kazi mnayo waaacheni watoto waende shule wakija kujitambua hao mtapata shida mana watajua shida zao zme7bishwa na nyie Magamba
 
Muonekano wa hadhara anayoihutubia inasema yote. Kwanza wengi ni watoto na pili hadhara yote haioneshi furaha. Ni kama imepigwa butwaa! Maelezo yaweza kuwa mengi. Huenda wanamshangaa mwanamume kujiremba kangha mwli mzima kama demu, au wanashangaa upupu unaotoka mdomoni hauoani na hali halisi ya maisha yao, au wanatafakari jinsi wanawake wanavyodhalilishwa na dume huyu alijivalisha mavazi yao, au wanajiuliza kama huyu Kamafumu ni tofauti na chama chake kilichokosa mvuto machoni pa Watanzania wengi hata kuwekwa mizani sawa na ufisadi, au ..........., au ............... nk., nk. Kilicho dhahiri katika picha hiyo ni kuwa Kamafumu anawahutubia watoto ambao si wapiga kura wake. Atashindaje chaguzi hii !?!
 
Mkuu ingalitosha wewe kusema bila ushahidi huu wa picha maana hawa watoto ni wengi mno .Je nao ni wapiga kura ?
 
Watoto waachwe wasome jamani, mbona mnawashawishi kujiunga na kampeni uchwara kwa zawadi za pipi na ubwabwa?
 
Back
Top Bottom