Dk Chegeni alisakama Mwananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Chegeni alisakama Mwananchi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mlachake, Sep 22, 2010.

 1. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,923
  Likes Received: 631
  Trophy Points: 280
  MJUMBE wa Kamati ya Kuratibu Kampeni za Urais za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Raphael Chegeni amelisakama gazeti hili akidai lina agenda ya siri ya kukihujumu chama hicho na kuipendelea Chadema.

  Dk Chegeni alitoa malalamiko hayo jana kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya chama hicho,yaliopo Lumumba jijini Dar es Salaam.

  Mjumbe huyo, alitoa lawama hizo baada ya gazeti hili toleo la Jumatatu wiki hii kumnukuu Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe kwamba Kampuni Binafsi ya Synovate imeficha taarifa ya utafiti inayoonyesha mgombea urais wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa anaongoza kwa kura za maoni.

  "Sisi (CCM) tunasikitika sana kwa gazeti la Mwananchi kuandika habari hiyo tena ukurasa wa mbele na kupotosha Watanzania. Tunaamini Mwananchi wanalo lao jambo. Limeonyesha dalili za wazi za kupinga CCM na kuunga mkono chama cha Chadema," alisema.

  Alipoulizwa iweje kulishutumu gazeti la Mwananchi wakati lilizingatia kanuni za uandishi wa habari wakati wa kuandika habari hiyo, kwa kutoa fursa kwa pande zote kutoa maelezo, ikiwemo Synovate, Dk Chegeni alizidi kusisitiza kwamba CCM haikutendewa haki kwenye taarifa hiyo.

  Alisema kwamba pamoja na gazeti hilo, kuzingatia kanuni za uandishi wa habari, jinsi habari hiyo ilivyotoka ilionyesha kuikandamiza CCM na kuifagilia Chadema.

  Dk Chegeni ambaye alikuwa mbunge wa Busega, lakini alishindwa kwenye kura za maoni na Dk Titus Kamani, alidai kwamba Synovate imeliamuru Mwananchi kukanusha na kuomba radhi kwenye ukurasa wa mbele na kwamba wao wanasisitiza hilo kama sehemu ya kuisafisha CCM mbele ya wananchi.

  Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd (MCL), Theophil Makunga alisema hajapokea barua yoyote kutoka Synovate kutaka taarifa iliyoandikwa na Mwananchi ikanushwe na kuomba radhi.

  Kuhusu habari inayolalamikiwa na CCM, Makunga alisema gazeti la Mwananchi lilitimiza wajibu wa kuuhabarisha umma.

  Alifafanua kwamba mwandishi wa mwananchi akaripoti taarifa hizo zilizotolewa na Mbowe kwenye kampeni kama ilivyo kwa vyama vingine ambavyo vinatoa taarifa zao kwenye kampeni.

  Makunga alisema habari hiyo iliandikwa kwa kuzingatia kanuni za uandishi wa habari ikiwa ni pamoja na Synovate kupewa fursa ya kujibu shutuma walizoelekezewa.

  Kuhusu tuhuma kwamba Mwananchi limekuwa liiandika vibaya CCM na kuipendelea Chadema, Makunga alisema hiyo siyo kweli kwa sababu ripoti ya Synovate inaonyesha ni gazeti hili linaandika bila upendeleo kwa asilimia 97.

  "Yeye (Dk Chegeni) anatoa mawazo yake kama mkereketwa wa CCM, lakini ukweli ni kwamba utafiti wa kisayansi uliotolewa na Synovate unaonyesha sisi tuko neutral (bila upendeleo) kwa asilimia 97," alisema Makunga.

  Kwenye mkutano na waandishi wa habari jana, CCM ilionyesha kukerwa na taarifa hiyo ya Mbowe na kuingilia kati kauli hiyo licha ya kwamba Synovate walikanusha na vyombo vya habari vikaiandika kwa kina jana.

  "Tunamtaka Mbowe aache kuwapotosha watanzania," alisema DK Chegeni ambaye baada ya kushindwa katika kura za maoni za kuwania kuwa mgombea wa CCM, Busega, aliripotiwa kutishia kuhamia Chadema kwa kile kilichoelezwa kutokubaliana na matokeo hayo.

  Alipouilizwa kama haoni kitendo cha kuendelea kuvitaka vyombo vya habari vikanushe taarifa hiyo ya Mbowe kwa mara nyingine ni kuonyesha mchecheto wa upinzani wanaoupata kutoka Chadema, Dk Chegeni alisema taarifa hiyo, iliandaliwa kwa makusudi ili kushawishi wananchi kwamba Dk Slaa anaongoza wakati si kweli.

  Alisema kinachowauma zaidi ni kwamba Mbowe alitumia taasisi inayoheshimika nchini ya Synovate, kumuibulia umaarufu Dk Slaa jambo ambalo ni si kweli.

  Maelezo hayo ya Dk Chegeni yamekuja siku moja baada ya Meneja wa Synovate (T), Aggrey Oriwo kukanusha kauli iliyotolewa Jumapili na Mbowe katika mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi mkuu kwamba Synovate imeogopa kutangaza matokeo kuhusu umaarufu wa wagombea yaliyoonyesha Dk Slaa anaongoza.

  "Taarifa hizo ambazo pia zimeripotiwa katika baadhi ya magazeti si za kweli. Mimi kama msimamizi mkuu wa Synovate Tanzania nimekerwa sana na nimeandika malalamiko yangu kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT), kulalamikia vyombo vilivyoripoti," alisema Oriwo.

  Alisema Synovate ni kampuni huru inayofanya kazi zake kwa ukweli na uwazi bila ya kushawishiwa au kulazimishwa na mtu au taasisi yoyote ya kisiasa.

  "Kauli ya Mbowe imetukera sana na …tunamtaka kama ana uhakika na ushahidi wa aliyosema, autoe hadharani kama sisi tulivyotoa matokeo hadharani," alisema Oriwo.

  Alisema hawana cha kuficha na kwamba hawajatishwa wala kulazimishwa na chama au taasisi yoyote kuzuia matokeo ya utafiti.

  "Ubora wa kazi zetu unakubalika kitaifa na kimataifa kwa sababu hatushabikii chama chochote cha siasa na ndio maana mwaka jana tulifukuzwa Zanzibar kwa madai kuwa tulitoa matokeo ya uongo," alisema Oriwo.

  Kuhusu tafiti za kisiasa, Oriwo alisema ni kawaida kwa kampuni yake kukusanya maoni kuhusu hali ya nchi kisiasa kila baada ya miezi mitatu na kwamba tafiti zote za kujua hali ya kisiasa nchini hazitokani na wateja wao bali wanajidhamini wenyewe, hivyo hazina aina yoyote ya upendeleo.

  "Tunakusudia kufanya utafiti mwingine wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu hali ya siasa nchini kabla ya uchaguzi mkuu na matokeo yatatoka kabla uchaguzi huo wa Oktoba mwaka huu.


  "Tukimaliza kazi ya kukusanya maoni hayo, tutatoa matokeo kwa wananchi bila ya kubania hata kama yataonyesha kuwa umaarufu mgombea wa CCM umeanguka kwa sababu hatushabikii siasa," alisema Oriwo.

  SOURCE MWANANCHI:
   
 2. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nilijua ccm wasingeweza kuvumilia kuonekana umaarufu wao unashuka. Kama taarifa hiyo ingekuwa inaeleza vinginevyo, kwamba ccm haishikiki, basi ccm wangechekelea hata kama wangedanganywa. Nawashauri ccm wasubiri kura za maruhani tu na za wizi siku ya siku, ukweli ndio huo kwamba watanzania wa sasa sio sawa na wale wa 1961. Wasisahau kwamba kila kitu kinayo nafasi ya kupanda na kushuka. \hiyo ni tabia asilia. Musolin na Hitla wako wapi leo? Hata taifa la kirumi na la farao sasa hivi sio neno, Nebukadneza kwani bado ni maarufu leo? Goliath alilazimika kutii amri kwa DAudi ingawa alijifunika sana kujikinga na alikuwa na nguvu nyingi. Upinzani nao unao uwezo wa kufanya vitu vyao, tukubali ukweli maana ccm sio sultani wa Tanzania.
   
 3. MANI

  MANI Platinum Member

  #3
  Sep 22, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,410
  Likes Received: 1,863
  Trophy Points: 280
  Mwaka 2005 Kikwete alielezwa ni chaguo la mungu na magazeti yaliandika hivyo na ripoti za kura za maoni zilikuwa upande wao hawakulalamika wala kudai ni upotoshaji wa wananchi,leo wanaelezwa ukweli wamekuwa wakali na kudai watu wanapotoshwa. Hivi ni mtu gani ambaye atakuwa na imani na serekali iliyomuahidi maisha bora miaka mitano nyuma lakini hali ya maisha ni mbaya karibu mara kumi ya hiyo miaka mitano nyuma na bado watu wakakupenda? Leo miaka takribani 50 ya uhuru watoto wetu wanakaa chini madarasani ambako sehemu nyingine hata sakafu ya simenti hamna,wagonjwa mahospitalini wanakosa vitanda na dawa wakati nchi ina rasilimali nyingi lakini haziwanufaishi wameelezwa kuwa utajiri wa asili wetu unatumiwa vibaya ndio maana watu wamebadilika.Halafu hivi unaposhindana na mwenzio si lazima ukabali kuna kushindwa na kushinda au hilo kwao halipo.

  Hayati Bob Marley aliwahi kunena kwenye moja ya nyimbo zake "You can fool some people some time but not all time" huu ni ujumbe tosha kuwa watu wameamka.
   
 4. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  chegeni najua tu atateuliwa kuwa RC Mkoa mpya wa KATAVI, usibishe hapo analinda kibarua kitarajiwa.
   
 5. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  CCM wekeni poll ya 'nani unamchagua kuwa rais 2010' halafu muone matokeo yatakuwaje? Lakini nyie Synovate si mlisema manafanya opinion poll kila quarter, sasa quarter hii imekuwaje?
   
 6. ALU-MASOLI

  ALU-MASOLI Member

  #6
  Sep 22, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  :yield:

  Sioni ajabu kwani hata siku ya ijumaa katika kipindi cha kipima joto kinachorushwa na kituo cha matangazo cha IPP MEDIA-ITV, mheshimiwa Chegeni alialikwa pamoja na wawakilishi wengine toka vyama vya upinzani kujadili siku ya demokrasia na kutoa maoni yao na mfumo na mwenendo wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu. Lakini cha kushangaza zaidi mheshimiwa alianza kwa kuwatupia lawama wapinzani wake wakuu yaani CHADEMA kwa siasa wanazoendesha akiziita ni za kuwapotosha watanzania badala ya kuenda moja kwa moja kwenye mada na kujadili jinsi kampeni zinavyosadifu demokrasia ya kweli.
  "what governs men is the fear of truth"
   
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ila REDET walipotoa uchunguzi wao kipindi kile walikuwa sahihi.
  Naungana na MAN you can not fool us all the time.
  Saa ya ukombozi wa Mtanzania imefika.
  Alafu huyu Chegeni ivi hawajui the more anavyoifuatilia iyo issue ndo inagain popularity.
  Naona this time wameona Makamba akae pembeni pamoja na kinana ili Dr ndo atoe majibu
   
 8. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  tatizo la tanzania ni kuwa na wasomi kama hawa wasioweza kusimama kwa miguu yao wenyewe, yaani wasomi waganga njaa. Msomi kama huyu hawawezi kujisimamia na kuendeleza maiasha nje ya hisani na ufisadi wa ccm.

  juzi tu baada ya kutoshinda katika kura za maoni za ccm katika jimbo la busega, dr chegeni aliingia msituni kiasi cha mhe jakaya kikwete kumuagiza mkuu wa mkoa, dc, usalama wa taifa wamtafute baada ya dr chegeni kutoonekana katika mapokezi ya kikwete, alipokuwa katika kampeni mkoani mwanza.

  cha kustaajabisha leo hii dr chegeni anatambulishwa kama mjumbe wa kuratibu kampeni za mgombe urais za chama cha mapinduzi. Hivi kweli mjumbe wa kuratibu kampeni anaweza kutafutwa na usalama wa taifa? Hivi ni kwanini msomi kama huyu anafikia hatua ya kujidhalilisha kiasi hiki?

  kama kweli dr chegeni angekuwa amehitimu kihalali katika fani alizosomea na sio kuchakachua digrii, kazi inayofanywa na dr slaa na chadema ya kudai mgawanyo sawa wa rasli mali za taifa ikiwemo madini n.k ilistahili kuwa imeanzishwa na dr chegeni ndani ya ccm kwa kuwa alikuwa mmoja wa wabunge kutoka kanda ya ziwa inayoongoza kuchangia pato la taifa kupitia kilimo, madini, uvuvi n.k ilihali wakazi wengi wakiongoza kwa umaskini wa kutupa, ujinga na maradhi.

  wasomi kama hawa wanadhalilisha wasomi wenzao hapa nchini.
   
 9. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  hivi huku Dr.Chegeni ana udakitari wa nini vile??? wa binadamu,wanyama au PhD? HUYU jamaa ni kazi bure kabisa ndio maana amepigwa chini kwenye kula za maoni na ndugu na jamaa yake ,nadhani anadegeree zile fake zilizotangazwa na masemakweli,maana kama anaakili za busara huyu bwana ndo anatoka kanda ya ziwa lakini hajal hata rasilimali zinatumikaje kama madini etc... kuwa na watu kama hawa ni hasara sana katika taifa.
   
 10. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  hebu mwenye Dk Chegeni aimwage hapa tuitathimini.
   
 11. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa na udokta wake wa kuchonga hawezi kupata URC; hicho cheo sio size yake pengine kuwa dc huko Nantumbo!!
   
 12. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #12
  Sep 22, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Hawajaiona hii ja JF ambayo Dr anaongoza kwa 74%?
   
 13. M

  Mswahela Member

  #13
  Sep 22, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni daktari wa miti shamba; NJAA INAMSUMBUA
   
 14. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #14
  Sep 22, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,923
  Likes Received: 631
  Trophy Points: 280
  Rotten in the system
   
 15. M

  MHANJO Member

  #15
  Sep 22, 2010
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwanza ametokea wap? au ndo atatetea ukuu wa mkoa nini?
   
 16. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #16
  Sep 22, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mbona hajaishambulia daily news, tbc, mtanzania, jamboleo et all kwa kuipendelea ccm?
   
 17. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #17
  Sep 22, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Tena waweke kwenye website yao http://www.cms.ccmtz.org, Bp zao zishuke na kupanda
   
Loading...