Dk Chami: Wafanyabishara ‘feki’ wageni ondokeni nchini

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,574
2,000
Dk Chami: Wafanyabishara ‘feki' wageni ondokeni nchini
Friday, 10 December 2010 20:49

Fidelis Butahe
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk Cyrill Chami jana alitangaza vita dhidi ya wafanyabishara wa kigeni wanaofanya shughuli kinyume na leseni zaao, akiwataka waanze kurejea kwao kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria. Chami ametoa agizo hilo wakati mitaa ya miji kadhaa nchini ikizidi kufurika wageni ambao wamejikita kuanzia kwenye biashara kubwa hadi ndogondogo, idadi kubwa ya wanaofanya kazi hizo ikiwa ni Wachina.

Chami, kama ilivyo kwa mawaziri wengine, ametoa kauli hiyo baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwatahadharisha kuwa hatakuwa na simile na waziri atakayeboronga katika utekelezaji wa majukumu yake. Kikwete, ambaye alikuwa akieleza majukumu ya mawaziri wanaounda baraza lake jipya, pia aliwataka kuwajibika, kufuata kanuni, sheria na pia kupambana na rushwa huku akisisitiza kuwa vita dhidi ya rushwa ni suala la kikatiba na kuwataka kuhakikisha kuwa Mpango wa Pili wa Mkakati wa Kitaifa wa Kupambana na Rushwa (NACSAP-11) unatekelezwa.

Jana, Dk Chami alisema jijini Dar es Salaam kuwa wapo wafanyabiashara wa kigeni nchini wanaofanya shughuli zao kinyume cha sheria na taratibu za leseni na kuwataka wajisalimishe kabla ya kubainika na kuchukuliwa hatua. Bila ya kutaja aina ya wafanyabiashara hao, Dk Chami, ambaye alikuwa akizungumza na wafanyakazi wa ofisi ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), alisema:
"Wapo wanaoingia nchini kwa mgongo wa kufanya kazi katika makampuni, lakini baada ya muda wanajitosa katika baishara mbalimbali katikati ya jiji.

Wapo wanaotoka katika nchi rafiki, lakini hatutasita kuwachukulia hatua kwa kuwa hata huko wanakotoka kuna sheria za kufanya biashara. "Huu ni mchakato ambao umeshaanza kazi; tunawafuatilia; ni vyema kumjulisha mtu kabla hujamchukulia hatua. Kwa hiyo wajue kuwa tunalifuatilia jambo hili na kama wapo wanaojijua, basi wafungashe virago mapema." Alisema kuwa kauli hiyo si ya kisiasa, utani wala kufurahisha wananchi na kusisitiza kuwa yeyote aliyeingia nchini kwa njia za panya, ajiandae kufungasha virago.

Alisema kuwa wingi wa wafanyabisahara hao umekuwa kero ya muda mrefu kwa Watanzania kwa kuwa wanauza bidhaa zao kwa bei ya chini hali inayowafanya wafanyabiashara wazawa kufanya kazi yao katika mazingira magumu. "Unaweza kukuta wanauza bidhaa zao kwa Sh2,000 wakati mfanyabiashara Mtanzania anauza bidhaa kama hiyo kwa Sh5,000. Wizara yangu kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani, Kituo cha Uwekezaji (TIC) tutazitazama leseni za biashara kwa hawa wageni kama kweli biashara walizosajili ndizo hizo wanazozifanya," alisema Dk Chami.

Dk Chami alisema: "Haiwezekani mtu aje kama mfanyabiashara wa madini halafu kesho tumkute Kariakoo akifanya shughuli nyingine kabisa. "Jambo hili tutalitazama pia hata kwa Watanzania wanaofanya biashara kinyume na leseni walizoomba." Alifafanua kuwa operesheni hiyo ya kuwabaini wafanyabiashara hao ni ya muda mfupi na kusisitiza kuwa serikali haitasita kumtimua nchini atayebainika hata kama atakuwa na biashara iliyotoa ajira kwa Watanzania kiwango kikubwa. "Ndio maana tumelizungumza hili jambo mapema ili kuepuka malalamiko, watu wenye hekima zao watajua nini cha kufanya ikiwa ni pamoja na kufanya biashara kulingana na leseni zao zinavyosema," alisema Dk Chami.

Dk Chami hakutaja ni wafanyabiashara wa asili gani, lakini kwenye miji mingi nchini Wachina wamekuwa wakiuza bidhaa kwa bei ya chini na kufanya zile zinazouzwa na wazalendo kukosa soko. Wachina, ambao wanakaribia 10,000 nchini kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2008 za Shirika la Habari la China (Xhinua), pia wamekuwa wakiuza bidhaa ambazo hazidumu kwa muda mrefu, zikiwemo tochi, taa, viatu, mapazia, nguo, samani na vitu vingine.

Dk Chami pia aliipongeza Brela kwa utendaji wake wa kazi pamoja na kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya na kuwataka wananchi kusajili biashara zao ili kuweza kupanua wigo wa biashara na kuvutia uwekezaji. Naye mkurugenzi mtendaji wa Brela, Esteriano Mahingira alisema zoezi la kuhakiki makampuni yanayofanya shughuli zake kinyume na leseni husika bado linaendelea.

"Zoezi hili tuliliweka bayana mwishoni mwa mwaka jana na linaendelea. Yapo makampuni ambayo baada ya kupata taarifa hizi yemejisalimisha," alisema Mahingira.
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,574
2,000
Chami awakunjulia makucha Wamachinga wa kigeni


na Zainab Mlimbila


amka2.gif
WAFANYABIASHARA wa kigeni ambao wanafanya shughuli zao kiholela pasipo kusajili mashirika yao ama wanafanya shughuli zao kinyume na usajili wao unavyotaka wamepewa onyo la kufungasha vilivyo vyao kabla hawajaanza kutimuliwa na kuharibiwa mali zao.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za kampuni ya kusajili Leseni na Makampuni (BRELA) Waziri wa Viwanda na Biashara Cyril Chami alisema kuwa watu ambao waliingia nchini kwa nia ya kufanya kazi kwenye kampuni lakini hawafanyi watafukuzwa hata kama wana mkataba wa kisheria.
"Ili kuwadhibiti watu hao lazima tushirikiane na Idara ya Uhamiaji , Wizara ya Kazi na Ajira na TIC , hii ni kwa wale wasiotimiza masharti," alisema Chami.
Chami alisema kuwa wenye sifa za kuomba kibali cha kuwekeza nchini ni lazima wawe na leseni ya daraja la kwanza katika biashara na pia serikali haiwezi kuzuia mashirika yaliyowekeza kuleta wataalam wao nchini.
Mbali na hilo aliwataka wale walioshindwa kuviendeleza viwanda waviachie ili kuwapa fursa wanaoweza kuviendeleza.
Alisema kuwa wakala wa serikali katika usajili wa leseni na biashara nchini wana kazi kubwa ya kudhibiti watu kama hao, na kwamba kwa kutambua kazi kubwa inayofanywa na Brela, serikali ina mpango wa kukarabati jengo lao mpaka pale jengo la Wizara ya Viwanda na Biashara litakapokamilika na wao kujiunga nao ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Katika hilo pia Brela wanatarajia kuanzisha usajili wa makampuni kwa njia ya mtandao itakayosimamiwa na watoaji huduma hiyo Nchini ICT.
 

Mziba

JF-Expert Member
Feb 7, 2010
245
225
Asante wakubwa kwa kutembeza ndula. Naona kaka anadalili za kuwajibika, mkuu. Biashara zikifanyika kihalali maisha yatabadilika kwani watu wengi watapata kazi na wakina bibi wauza vitumbua watapata mikopo kutoka benki, kwani nazo sitato mikopo kihalali. nadhani. kuna mwenzetu mwana JF aliwahi kudokeza kua, benki huwa hawaangaalii Business plan. Ingekua vizuri banki wakifundisha wafanyakazi kuchuja urongo kwenye business plan. its not a rocket science as long as unajua kusoma na kuandika, bas. na hesabu za kujumlisha na kutoa. Daasa la saba. Kwa maana hiyo, kusitokei bonde la ufa katika Money Velocity and a shift in the market equalibriums. wakiondoka wasije wakaacha vacuum in a supply side. lakini tuheshimu sheria jamani. inchi itasaidia.
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,574
2,000
Asante wakubwa kwa kutembeza ndula. Naona kaka anadalili za kuwajibika, mkuu. Biashara zikifanyika kihalali maisha yatabadilika kwani watu wengi watapata kazi na wakina bibi wauza vitumbua watapata mikopo kutoka benki, kwani nazo sitato mikopo kihalali. nadhani. kuna mwenzetu mwana JF aliwahi kudokeza kua, benki huwa hawaangaalii Business plan. Ingekua vizuri banki wakifundisha wafanyakazi kuchuja urongo kwenye business plan. its not a rocket science as long as unajua kusoma na kuandika, bas. na hesabu za kujumlisha na kutoa. Daasa la saba. Kwa maana hiyo, kusitokei bonde la ufa katika Money Velocity and a shift in the market equalibriums. wakiondoka wasije wakaacha vacuum in a supply side. lakini tuheshimu sheria jamani. inchi itasaidia.

I cincur with this averment....the guy looks very determined......................ila halahala ajihadhari na mafisadi wasije wakamkwaza..........
 

Koba

JF-Expert Member
Jul 3, 2007
6,136
1,500
Huyu naye bure tuu na kutafuta cheap popularity isiyo na mpango,tatizo la kufanya biashara bila kufuata utaratibu sio la wageni peke yao na wacheza foul wengi ni hao hao wazawa,across the board kila mfanyabiashara lazima afuate leseni yake haijalishi wewe ni mgeni au mzawa,to singleout wageni au kundi fulani ni very unfair & unproductive,this careless & irresponsible statement kutoka kwa waziri ni hatari sana na inaweza kufanya watu wakaanza kufikiri wageni wote ni wabaya na hawafuati sheria...enforce the law sio vitisho vya vilabuni.
 

newmzalendo

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
1,377
2,000
Takwimu hana,atawezaje kuwaondoa hizi ni blah blah za kipolitiki.Je imigration inajua wageni wangapi wapo nchini kwa biashara na wangapi wameondoka
waliopo nchini wapo wapi,address yao nchini,adress yao walipotoka,je wanalipa kodi kiasi gani,wametoa ajira kwa watz wangapi na wageni wenzao wangapi
Jana na Leo nimekutana na Mchina amepakia mabox na wachina wenzake ktk pikipiki ya tairi Tatu,kama Guta type ya pikipiki.leo nimemuona mchina huyo huyo amepakia wachina wawili na mmasai mmoja ktk pikipiki hiyo hiyo.
inamaaana anafanya biashara ndogondogo nchini.Je hii inatija gani kwa taifa,sasa hapa elimu ya biashara na utalii inabidi itolewe kuanzia primary ili hata mtaani wanachi waweze kutambua yupi mtalii na yupi kaja kuiba rasilimali zetu bila kulipa kodi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom