Dk Bilali: Sijaficha mabilioni Uswisi

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
227784_m.jpg


Posted Novemba17 2012 saa 9:12 AMKwa ufupi
MAKAMU wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilali, amesema yeye siyo miongoni mwa vigogo wa Serikali wanaodaiwa kuficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi katika sakata lililoibuliwa hivi karibuni na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.



MAKAMU wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilali, amesema yeye siyo miongoni mwa vigogo wa Serikali wanaodaiwa kuficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi katika sakata lililoibuliwa hivi karibuni na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

Dk Bilali alitoa kauli hiyo jana kwenye mhadhara wa 13 wa kumbukumbu ya kumuenzi aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, akijibu swali la mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Jonson Robert.

Katika swali lake hilo, Robert alitaka kujua hatua zinazochukuliwa na Serikali kushughulikia tuhuma za mabilioni ya fedha yaliyofichwa nchini Uswisi, kama ilivyowasiliswa bungeni na Zitto katika hoja yake binafsi.

Robert alisema ukimya wa Serikali katika suala hilo na kutochukua hatua za haraka kunawafanya waamini kwamba huenda hata viongozi wa juu wanahusika na ufichaji wa fedha hizo.

“Mheshimiwa Makamu wa Rais, tumesikia kuhusu umuhimu wa Sokoine katika kulinda rasilimali za taifa na kupambana na wahujumu uchumi, sasa je Serikali imechukua hatua gani dhidi ya watu wanaodaiwa kuficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi?,” alihoji mwanafunzi huyo katika sehemu ya swali lake.

Akijibu swali hilo, Dk Bilali mbali na kueleza hatua ambazo Serikali imezichukua alisema kuwa yeye si miongoni mwa watu wanaotuhumiwa kuficha fedha hizo nchini Uswisi.

Dk Bilali alisema suala hilo limeshafikishwa serikalini na tayari hatua kadhaa za kisheria zimeanza kuchukuliwa na kama endapo kuna watu watabainika kuhusika na ufisadi huo, sheria itachukua mkondo wake.

"Serikali ya Mheshimiwa, Dk Jakaya Mrisho Kikwete iko tayari kulishughulikia suala hilo kama watu hao wapo, tusaidieni kuwapata watu hao," alisema Dk Bilali.

Awali tuhuma za kuwapo kwa vigogo waliochota mabilioni na kwenda kuyaficha katika benki mbalimbali, zilitolewa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama hoja binafsi na mbunge huyo, kisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuahidi Bunge hilo kuwa Serikali italifanyia kazi suala hilo kwa kushirikiana na mbunge huyo.

Chimbuko la hoja
Mapema mwaka huu, baadhi ya vyombo vya habari likiwamo gazeti hili, vilifichua kuwapo kwa fedha zilizofichwa nchini Uswisi na baadaye ilibainika kwamba fedha hizo ni mali ya Watanzania 27 wakiwamo wanasiasa na wafanyabiashara.

Gazeti hili pia lilibaini kwamba mmoja wa walioficha fedha hizo anamiliki Dola za Marekani milioni 56 (sawa na Sh89.6 bilioni).

Katika uchunguzi wake, Mwananchi limebaini pia kwamba kiasi cha fedha kilichothibitishwa kumilikiwa na Watanzania hao ni jumla ya Dola za Marekani 186 milioni (takriban Sh300 bilioni) kwa viwango vya sasa vya kubadilishia fedha ambavyo ni Sh1600 kwa Dola ya Marekani.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa mbali na kigogo anayemiliki Sh90 bilioni, wapo wengine wanne, ambapo anayefuatia anamiliki Dola 30 milioni (Sh48 bilioni), mwingine Dola 20 milioni (Sh32 bilioni) na wengine wawili kila mmoja anamiliki Dola 10 milioni (Sh16 bilioni).

Kuhusu Sokoine
Akizumzungumzia Hayati Sokoine, Dk Bilali alisema atakumbukwa kwa mengi kubwa zaidi ni kuhusu maono yake katika kujenga Tanzania yenye neema kwa kuwa alitumia muda, nafasi yake na vipaji vyake vyote kuhakikisha wananchi wanapata haki na kupunguziwa ukali wa maisha.

Alisema Hayati Sokoine anabakia kuwa tunu kubwa katika historia ya uongozi wa Tanzania akiwamo Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Kambarage Nyerere na Hayati Abed Aman Karume.


Makamu huyo wa Rais alisema, katika kuhakikisha utofauti ulioongezeka kati ya maskini na matajiri ni kinyume na sera za uchumi za wakati ule, ambapo hayati Sokoine alitangaza vita dhidi ya wahujumu uchumi, mapambano aliyosimamia kwa dhati ya moyo wake hadi umauti ulipomkuta.

Alisema, kiongoni huyo kidogo kilichopatikana kitumike kwa manufaa ya wote ndiyo maana alikerwa waziwazi na tabia ya baadhi ya matajiri na wafanyabiashara kuficha bidhaa muhimu wakati huo kwa lengo la kuwalangua maskini.

Kuhusu elimu, Dk Bilali alisema kuwa Serikali imeweka mkazo katika elimu kwa kuhakikisha kuwa Watanzania wengi wanapata elimu, hatua ambayo alisema inalenga kuondoa matabaka miongoni mwa walionacho na wasionacho.

Alisema kwamba utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya elimu ikiwamo Mipango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na ule wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) ni sehemu ya mikakati hiyo.

Alisema kutokana na mikakati hiyo, idadi ya wanafunzi wanaojiunga na shule za msingi na sekondari imeongezeka, hivyo kuongeza idadi ya wasomi katika vyuo vikuu.

"Hizi shule za kata ambazo baadhi ya watu wanaziita 'yeboyebo', zimesaidia vijana wengi kuweza kuendelea na masomo mpaka ngazi ya chuo kikuu. Kama shule hizi zisingekuwapo unafikiri vijana wangapi wangekuwa mtaani?" alihoji Dk Bilali.

Awali Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo ya SUA, Dk Caroline Nombo alisema, chuo hicho kilipewa jina la Sokoine kwa lengo la kuweka kumbukumbu za mambo aliyoyafanya, pia kutekeleza dira na maono ya kiongozi huyo.

Kaulimbiu ya mhadhara huo wa 13 ilikuwa ni ‘Mageuzi ya kisiasa na demokrasia huria Tanzania, urithi aliotuachia hayati Sokoine’.

 
hawa dawa yao ni kuwapiga chini tu naona wanafurahia ujinga wetu watz ...hata boss wake hawajuhi?
 
Hivi hamna namna ya kuwashugulikia haw? Kesi ya ngedere unampelekea nyani!!! Hapa hamna kitu kitakachofanyika,
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom