Dk. Bilal: Wenye vijisenti¡ ng'ambo watashughulikiwa bila kujali vyeo vyao.

Brightman Jr

JF-Expert Member
Mar 22, 2009
1,225
232
Na Ashton Balaigwa
17th November 2012
bilali...ipp.jpg

Makamu wa Rais Dk. Mohamed Bilal
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Bilal, amesema watuhumiwa walioficha fedha nje kinyume cha sheria watachukuliwa hatua bila kujali nafasi wala nyadhifa zao na kwamba suala hilo litawekwa wazi.
Kadhalika amejitetea kuwa yeye si mmoja wa viongozi walioficha fedha ng¡¯ambo.
Dk. Bilal alilazimika kusema hayo, kufuatia swali lililoulizwana mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), katika Mhadhara wa 13 wa Kumbukumbu ya Waziri Mkuu wa zamani, hayati Edward Moringe Sokoine uliofanyika katika kampasi ya Solomoni Mahlangu mjini hapa.
Katika swali lake mwanachuo John Robart alitaka kujua ni hatua gani serikali imewachukulia viongozi waliotajwa kuficha fedha nje ikiwa ni sehemu ya kumuenzi hayati Sokoine.
Alisema Sokoine alikuwa mwadilifu na aliyekemea rushwa katika ngazi zote ili kuleta usawa baina ya maskinina matajiri.
Akijibu swali hilo, Dk. Bilal alisema pamoja na kwamba yeye si miongoni mwa walioficha fedha nje, lakini kama wapo Watanzania na wakithibitika kuwa wameficha fedha kwenye benki za ng¡¯ambo sheria na taratibu zitaongoza jinsi ya kuwashughulikia.
Alisema iwapo taarifa sahihi za watu hao walioficha fedha nje zitapatikana ,serikali itawachukulia hatua bila kujalinafasi zao na kwamba suala hilo litawekwa wazi bila kificho.
Watanzania zaidi ya 300 wanadaiwa kuficha mabilioni ya Dola za Marekani katika benki za kigeni ikiwemo Benki ya Uswisi ambapo hivi karibuni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) Zitto Kabwe, aliwasilisha hoja binafsi bungeni kutaka uchunguzi wa kina ufanyike na wahusika washughulikiwe kisheria.
Taarifa hizo alizozitoa zilihusisha madai kuwa baadhiya Watanzania wameficha Dolamilioni 300 kwenye benki za Uswisi ikiwa ni rushwa walizopewa kwenye miradi ya utafiti wa gesi na mafuta inayofanywa na makampuni yakigeni.
CHANZO: NIPASHE
 
Aanother political rhetorics from CCM leader! Action/deeds speaks louder than words.

We need action not any empty words! Huyo kijana ange rephrase swali lake kuonesha kwamba kweli ni mwanafunzi wa chuo kikuu kuliko kuuliza direct question kama hilo. " Je hadi sasa serikali imechukua hatua gani kwa viongozi walioficha pesa Uswiss?

But KUDOS to VP at least he can sustain the heat for taking questions from the audience. Especially audience ya wasomi kama wa SUA.

Piga ua garagaza JK hawezi kuthubutu Jambo hilo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom