Dk. Bilal: Waislamu msikubali kupotoshwa Sensa; Asisitiza Sensa si ya dini bali maendeleo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Bilal: Waislamu msikubali kupotoshwa Sensa; Asisitiza Sensa si ya dini bali maendeleo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 20, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]JUMATATU, AGOSTI 20, 2012 07:45 NA BAKARI KIMWANGA, DAR ES SALAAM

  *Awataka wapuuze ghiliba hizo
  *Asisitiza Sensa si ya dini bali maendeleo

  MAKAMU wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, amewataka Waislamu nchini, kupinga upotoshwaji unaofanywa na kikundi cha watu kuwataka wasishiriki katika Sensa.

  Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana, katika ibada ya swala ya Eid El –Fitri, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi mmoja.

  Alisema kufikia maendeleo nchini, Serikali imeandaa Sensa kama dira ya kuweza kufikia mipango hiyo, hivyo ni lazima kila Mtanzania ajiandae kuhesabiwa.

  “Ninapenda kutoa salamu zangu za Eid, lakini kubwa ninawaomba Waislamu wote nchini, kuwapuuza wale wanaowataka Waislamu wasihesabiwe.

  “Ili kuweza kufikia mipango ya maendeleo, ni lazima tufanye hivyo na kila Mtanzania ni lazima ahesabiwe na wanaofanya upotoshaji huo, tuwapinge kwa kuwa hilo si lengo la Serikali kwa watu wake.

  “Sensa si dini ni hatua muhimu ambayo itatupa picha halisi ya utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa miaka mitano, MKUKUTA kwa upande wa Bara na MKUZA kwa Zanzibar, hivyo hatuna budi kila mmoja wetu, kuweza kushiriki hatua hii muhimu ifikapo Agosti 26, mwaka huu,” alisema Dk. Bilal.

  Siku chache zilizopita, wakati akizindua rasmi mchakato wa sensa, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alikionya kikundi cha watu kinachowarubuni Waislamu kutoshiriki sensa ya mwaka huu.

  Kikundi hicho kinachoongozwa na Sheikh Ponda Issa Ponda, kinataka kipengele cha dini kiingizwe katika dodoso la sensa.

  Hata hivyo, Serikali imekuwa ikisisitiza kwamba, kipengele hicho si cha muhimu kwa sababu hakisaidii katika kupatikana takwimu muhimu zinazohitajika kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

  Lakini, juzi Ponda alikaririwa akisisitiza azma yake ya kuwashawishi Waislamu kutoshiriki katika sensa, hadi kipengele hicho kiongezwe katika dodoso za sensa.

  Awali, akimkaribisha Makamu wa Rais, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, alisema ni muhimu kwa kila Muislamu kuwa na upendo kwa wenzake kama inavyotaka dini.

  “Katika kipindi cha siku 29 tulikuwa katika semina ya hekima na unyenyekevu mbele ya Mungu na hakika kuisha kwa mwezi huu ni daraja tosha la kutuvusha na kuyaenzi kila yaliyo mema katika maisha yetu ya kila siku.

  “Pamoja na hayo, lakini bado Waislamu tuna jukumu ya kushiriki Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka huu, kwa kuwa kufanya hivyo ni kuunga mkono juhudi za Serikali yetu.

  “Kila mtu na kila Muislamu lazima ahesabiwe, sambamba na kuitumia siku ya Eid kuwatembelea yatima, wagonjwa na wasiojiweza,” alisema Sheikh Alhad.

   
 2. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hawachelewi kusema kuwa msukumo wa kugomea sensa unatoka kwa wapinzani. Maana serikali yetu ya sasa kila unapojitokeza udhaifu kwenye majukumu yake, huwa tunapewa majibu marahisi yasiyo na vielelezo. Sijui kwanini huwa wanapenda kutuambia WAPINZANI ndiyo wanaleta kila tatizo, inamaana hawakubali kukosolewa wala hawapo tayari kujirekebisha.

  Mfano kauli ya karibuni ya Mh. Rais kusema wanaotaka vita na Malawi kuhusiana na mgogoro wa mpaka katika ziwa Nyasa ni wapinzani. Sasa tumeshindwa kuelewa hao wapinzani ni waupande gani?? Maana waliotamka mambo ya Vita Mh. Lowasa, Mh. Membe na Mh. Sitta. Kama ni hivyo, inawezekana hawa wapinzani wanaozungumziwa wapo ndani ya Serikali/CCM. Kama wananchi tuifanyie nini serikali yetu ili iweze kutusimamia kama kimamlaka ya KIKATIBA???
   
 3. Iselamagazi

  Iselamagazi JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 2,221
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Nasubiri jinsi hii Bongo Movie itakavyomalizika! Sielewi movie nyingine itakayofuata itatoka ki-vipi! Lets wait and see.
   
 4. SIM

  SIM JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 792
  Trophy Points: 280
  Hapo wanaposema nikikundi cha watu wachache ndipo wanapoharibu
   
 5. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Na imekuwa safi imesemwa na mtu kama Bilal ambaye dini yake inajulikana na asli yake Zanzibar kunajulikana.
   
 6. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kikundi tena???????????? hii nchi jamani!
   
 7. t

  thatha JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mimi nadhani Bilali hawafanyii haki waislam. wenzetu wakiristo wakiingia Ikulu huenda Kuchukua mabilion ya fedha (MOU) lkn Bakwata wao tunaona wanaalikwa kula ftari na DAKU huku wenzao maaskofu wakifunga Mikataba na serekali wao wanatolewa nje wasione kitu.
   
Loading...