Dk. Bilal: Viongozi msichanganye dini, siasa

HISIA KALI

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
694
108
na Mwandishi wetu


amka2.gif
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal, amewataka viongozi wa dini nchini kutochanganya dini na siasa.
Dk. Bilal alitoa rai hiyo jana alipozungumza na waumini wa dini ya Kiislamu wakati wa Baraza la Eid lililofanyika kwenye msikiti wa Simbambali, Temeke, Dar es Salaam.
"Ni vema masuala hayo mawili (dini na siasa) tusiyachanganye kama alivyosema Kaimu Mufti, kwani masuala hayo yamewekewa sheria na mamlaka tofauti," alisema Dk. Bilal.
Awali akimkaribisha kuzungumza katika hafla hiyo, Kaimu Mufti wa Tanzania, Sheikh Ismail Habib Makusanya, alitoa wito kwa viongozi wa dini kutochanganya dini na siasa.
Kaimu Mufti huyo mbali ya kuwataka viongozi wa dini kuepuka kuyatumia majukwa ya nyumba ya ibada kuzungumzia masuala ya kisiaisa lakini pia alihimiza na kutilia mkazo umuhimu wa waumini wa dini ya Kiislamu kupendana ili kuimarisha umoja miongoni mwao.
"Tunahitaji kuwa kitu kimoja na hatuwezi kuwa hivyo bila ya kwanza kujenga na kuimarisha upendo miongoni mwetu. Tunapaswa kuacha kuchukiana na kubugudhiana, tunahitaji upendo ili tuweze kuwa wamoja," alieleza.
Akiendelea kuzungumza katika baraza hilo, Makamu wa Rais, alilishauri Baraza la Waislamu Nchini (BAKWATA) kuchukua jukumu la kuratibu safari za mahujaji ili kuzuia kasoro mbalimbali zinazojitokeza kila mwaka.
"Naliomba Baraza lichukue jukumu la kuratibu shughuli za kupeleka mahujaji wa Tanzania huko Mecca ili kuzuia kasoro zinazojitokeza mwaka hadi mwaka katika taasisi mbalimbali na kusababisha waumini wengine kukosa kutimiza nguzo hiyo muhimu wakati wamekamilisha taratibu zote za safari," alisema na kutoa mfano wa mahujaji wapatao 20 walioshindwa kusafiri mwaka huu wakiwa wameshalipia gharama zote za safari hiyo.
Alisema suala hilo halina budi kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu, kwani vitendo vya waumini kukosa kutimiza nguzo hiyo ya ibada wakati wameshalipia gharama zote sio tu vinasababisha migogoro baina ya Waislamu na taasisi hizo bali pia ni aibu kwa BAKWATA.
Katika salamu zake hizo, Makamu wa Rais aliipongeza BAKWATA kwa jitihada zake za kuimarisha elimu, afya, uchumi na mambo mengine ya ustawi wa jamii na kulitaka kuongeza nguvu katika kuimarisha elimu toka ngazi ya chekechea hadi chuo kikuu.
Naliomba Baraza litilie mkazo suala la elimu katika ngazi zote, kuanzia shule za awali hadi elimu ya juu. Dini yetu inaitukuza elimu na tumeamrishwa kuitafuta elimu popote ilipo," alisisitiza. Dk. Bilal alitumia fursa hiyo kuwapongeza Watanzania kwa kufanikisha kwa amani na utulivu uchaguzi mkuu uliofanyika hivi karibuni na kuwanasihi kuwaheshimu viongozi waliowachagua huku akisisitiza kuwa viongozi walichaguliwa ili kutekeleza wajibu wao kwa uadilifu na kuheshimu Katiba na sheria ya nchi ikiwemo ile ya kuheshimu uhuru wa kuabudu wa kila Mtanzania.

Hivi hawa viongozi wa siasa Tanzania wanapokwenda kwenye shughuli za kidini na kuanza kusema watu wasichanganye dini na siasa wana maana gani? Mimi huwa nashindwa kuwaelewa, kwanza wao wameenda na kupewa nafasi ya kuongea kwa sababu ni viongozi wa siasa wala sio wa dini. Kwa maana hiyo basi wao kuwepo kwenye shughuli za dini wakati wao ni viongozi wa siasa ina maana wanachanganya dini na siasa. Hii ina maana ili shughuli ya kidini iwe na uzito unaokubalika kwa jamii kiongozi wa kisiasa lazima awepo. Hii ina maana kuwa siasa na dini vinaenda pamoja. Kwa mawazo yangu mimi huwa nashindwa kuwaelewa kwa nini wanakuwa wanasema usichanganye dini na siasa wakati wao wanafanya hivyo. Basi kama hakuna kuchanganya dini na siasa basi viongozi wa siasa wasiende kwenye shughuli za kidini na wale wa dini wasiende kwenye shughuli za kisiasa.

Lakini hili halitawezekana kwani kwangu mimi dini na siasa havitengani kwa sababu mwananchi ambaye anategemewa kupiga kura kwenye siasa ndiye huyo huyo anayetegemewa na viongozi wa dini kwenda kwenye shughuli za kidini.
 
Kama mwanasiasa aliwezaje kusema mambo ya siasa na dini!! haya mambo wafanye wao halafu waseme wengine!!
 
Hawa wagonjwa wa akili na wao mnawapa kipaumbele!!!!!!!! Ni unafiki mtupu, au hajui muasisi wa SIASA ZA UDINI NI MKUU WAKE WA KAZI????

AANZE KWANZA KWENDA KUONGEA NA MKUU WAKE ALIEASISI ARUDI KWENYE MSTARI NA MBELE YA UMMA AMUOMBE RADHI SALIM AHMED SALIM, SUMAYE, MWANDOSYA & Co., Dr. Slaa na WANANCHI WOTE KWA UJUMLA KWA KUTULETEA SIASA ZA UBAGUZI WA KIDINI, KIKABILA, KIASIA NA KIAFRIKA n.k. BAADA YA HAPO SASA NINAWEZA KUANZA WASILIZA.

OTHERWIZE WATAKUWA WANANFIKI TU NA KUENDELEA KUWATHIBITISHIA WATANZANIA KUWA WAO NI WANAFIKI KWA KUJIDAI KUTAKA KUJENGA WALICHOTUMIA NGUVU NYINGI NA MALI NYINGI KUKIHARIBU
 
Jamani huyu Sioo wa kuamini alipokuwa katibu mkuu Wizara ya Sayansi na Technologia enzi za miaka ya 90 alikuwa anauendeleza udini kwa kuhakikisha waisilamu hasa vijana wa Zanzibar wanapata Scholarship; Sasa amaongelea kuacha udini na Siasa? Alikuwa katibu mkuu...
CCM kweli wanasahau wanapotoka...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom