Dk Bilal kushiriki mkesha wa kuiombea Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Bilal kushiriki mkesha wa kuiombea Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ustaadh, Dec 29, 2010.

 1. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2010
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  MAKAMU wa Rais, Mohammed Dk. Gharib Bilal atakuwa miongoni mwa Watanzania watakaoshiriki mkesha wa kitaifa wa kuiombea Tanzania na viongozi wake jijini Dar es Salaam.

  Mkesha huo pamoja na mambo mengine kutaombwa ufahamu wa kiroho utakaowawezesha wananchi kufanya chaguo jema la ama kuwa na Katiba mpya au kufanyiwe marekebisho ya 15.

  Aidha, imeelezwa kuwa mkesha huo wa 14, utakaofanyika kwenye mikoa 19 ya Tanzania Bara na Zanzibar keshokutwa, utajumuisha maombezi ya amani ya nchi, ufumbuzi wa matatizo yanayosababisha umasikini, ufisadi, dhuluma pamoja na matatizo mengine yanayowasumbua Watanzania.

  Akizungumza na wanahabari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkesha huo Kitaifa ujulikanao kama Dua maalumu, Askofu Godfrey Malassy alisema wamekamilisha sehemu kubwa ya maandalizi ikiwamo kupata vibali vinavyoruhusu mkusanyiko huo.

  Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, kwa Dar es Salaam, mkesha huo utafanyika kwenye Uwanja wa Uhuru kuanzia saa 12 jioni, na maombezi maalumu yataanza rasmi saa 3:00 usiku kwa ushirikiano wa viongozi wengine wa dini ya Kikristo wanaojihusisha na masuala ya maombezi, wanaounda kamati hiyo.

  Akifafanua hoja hiyo, Askofu Malassy alisema ni Mungu pekee atakayewafunua Watanzania na viongozi wao kwa kuwapa ufahamu utakaowawezesha kutoa uamuzi sahihi wa ipi inafaa kati ya Katiba mpya au yenye marekebisho, jambo litakalofanya pande zote zenye maoni tofauti kuwa na msimamo mmoja wenye faida na wenye kujali maslahi ya taifa.

  Alisema suala la Katiba lisipochukuliwa kwa busara na hekima ya Mungu, linaweza kuleta machafuko yasiyotegemewa kwa hiyo Watanzania wanapaswa kutumia siku hiyo kuiombea nchi, viongozi na wao wenyewe.

  “Tumefuata taratibu zote na kupewa vibali vinavyostahili ili kuendesha mkesha huo katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Mwanza, Dodoma, Arusha, Mbeya, Mtwara, Tabora, Kilimanjaro, Kagera, Iringa, Ruvuma na Zanzibar… hata waumini wa dini nyingine wanakaribishwa kwa kuwa maombezi haya hayachagui dini wala dhehebu,” alisema Askofu Malassy.
   
Loading...