Dk Bilal azomewa Mbeya; Wananchi wagoma kumsikiliza na kutaka mbunge wao aongee! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Bilal azomewa Mbeya; Wananchi wagoma kumsikiliza na kutaka mbunge wao aongee!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Feb 26, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal,akisalimia wananchi alipowasili kwenye Soko la Tunduma juzi, kwa ajili ya kuzindua soko hilo lililoteketea kwa moto baada ya kukarabatiwa.

  Stephano Simbeye na Godfrey Kahango,

  Tunduma

  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib Bilal jana alianza vibaya ziara yake mkoani Mbeya baada ya kupokelewa kwa zomeazomea za kulaani ufisadi, huku wananchi wakinyoosha vidole viwili juu, kuonyesha alama inayotumiwa na chama kikuu cha upinzani cha Chadema.

  Wananchi hao ambao waliokuwa wazomea walimshangilia kwa nguvu mbunge wa Jimbo la Mbozi Mashariki (Chadema), David Silinde aliposimama kwa kuimba wakismea; "Rais...rais....rais..."

  Hali hiyo ilisababisha zoezi la kutambulisha wageni mbalimbali waliojifika kumpokea Dk Bilal ambaye alifika eneo hilo kufungua soko la Tunduma, kukwama kutokana na wananchi hao kuzidisha kuzomea huku wa kimba; "Fisadi..., fisadi...!"

  Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Gabriel Kimolo alijikuta katika wakati mgumu kutokana na kuzomea huko aliposimama kusoma ratiba ya ugeni huo.

  Naye Mwenyekiti wa Soko la Tunduma alisimama kusoma taarifa ya soko hilo, lakini kelele hizo za wananchi hao ziliwafanya washindwe kusikika vizuri.

  Huku hali ikiwa bado haijatulia, DC Kimolo alilazimika kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro ili amkaribishe Makamu wa Rais, aweze kufungua Soko la Tunduma ambalo liliteketea kwa moto Novemba 28, mwaka jana lakini alipata wakati mgumu kutokana na kelele za wananchi hao.

  Kandoro alijitahidi bila mafanikio kuwatuliza wananchi hao kwa kuwasihi kuacha kuzomea na kupiga kelele.

  Hata hivyo alimkaribisha Dk Bilal azungumze nao, wakati bado kukiwa na hali ya zomeazomea.

  Hali yawa tete zaidi

  Dk Bilal alipopanda jukwaani kuzungumza, wananchi hao ambao wengi walikuwa vijana, waliendelea kupiga kelele huku wakinyosha vidole viwili juu pamoja na vitambaa vyenye rangi za bendera ya Chadema.

  "Nawaomba tusikilizane, nchi yetu imeweka utaratibu wa kusikilizana na kufikia muafaka, pia zipo mamlaka zilizowekwa kwa ajili ya kusimamia masikilizano ili kufikia muafaka wa matatizo yetu kwa mazungumzo," alisema Makamu wa Rais huku akiwa hasikiki vizuri kutokana na kelele kutawala umati huo.

  "Nimekuja kuwapeni pole ya kuunguliwa moto soko lenu na pia kuwapongezeni kwa kutafuta riziki zenu kwa uhalali," alisema Dk Bilal.

  Pamoja na kuzungumza kwa upole na kuwataka wananchi hao kutulia, alipingwa vikali na umati huo huku ukimtaka, ampishe Mbunge Silinde ili azungumze nao, ombi ambalo lilikubaliwa na Dk Bilal.

  Silinde aliwaomba wananchi hao wawe watulivu ili wamsikilize Makamu wa Rais ambaye amefika hapo kama kiongozi wa Serikali na kwamba ni mgeni wa wananchi wote bila kujali chama.

  "Nawaomba mtulie kama nilivyowaomba awali na pia naomba muwaruhusu watani zetu CCM ili nao wasikilize mkutano wa Makamu wa Rais," aliongeza Silinde na kufanikiwa kutuliza umati huo.

  Katika hotuba yake, Silinde alimwambia Dk Bilal kuwa wananchi wa Tunduma wana utaratibu wa kuhoji masuala mbalimbali yanayofanywa na viongozi wa Serikali na sio kwamba wanafanya fujo.

  Alitoa mfano kuwa, hivi karibuni wananchi hao walihoji kitendo cha Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha kuhudhuria Sherehe za Miaka 35 ya CCM mkoani hapa huku akitumia magari ya Serikali.

  Alisema hoja hiyo sio fujo bali ni kutaka kufahamu utaratibu mzima wa matumizi ya magari ya Serikali katika shughuli za kichama.

  Alisema kuwa tukio lililowaudhi wananchi hao hadi kufikia hatua ya kupiga kelele katika ufunguzi wa soko hilo, ni kuondolewa kwa bendera ya Chadema saa chache kabla ya Dk Bila hajafika eneo hilo.

  Mbunge huyo baada ya kumaliza kuzungumza, alimwomba Dk Bilal amruhusu Diwani wa Kata ya Tunduma, Frank Mwakajoka (Chadema) naye awasalimie wananchi, ombi ambalo lilikubaliwa na Dk Bilal.

  Hali yawa shwari

  Baada ya Silinde na Mwakajoka kuzungumza wananchi hao, walionekana kuridhika na kutulia na kumfanya Makamu wa Rais kuendelea na hotuba yake ambapo alianza kwa kuwataka kuheshimu utaifa wao, ikiwa ni pamoja na kumaliza matatizo yao kwa njia ya mazungumzo na si vinginevyo.

  "Tutashirikiana na wote walio tayari kuonyesha ushirikiano na kuheshimiana na tukikuza uhusiano wetu kwa kusikilizana, tutaonyesha Utanzania wetu," Alisema kwa kifupi na kumaliza hotuba yake.

  Kabla ya Dk Bila kuwasili

  Hali ya kuwapo vurugu katika mji huo, ilijionesha tangu asubuhi ambapo ilidaiwa kuwa chanzo chake ni kitendo cha Jeshi la Polisi kushusha bendera za vyama vya siasa katika eneo ambalo lilitarajiwa kufanyika mkutano huo.

  Mmoja wa aliyeonja chungu ya ghasia hizo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Mbozi, Lucy Mfupe ambaye licha ya gari alilokuwa akisafiria aina ya Toyota Prado kupigwa mawe, alivamiwa na vijana waliokuwepo eneo hilo kabla ya kuokolewa na walinzi wa CCM.

  Mwingine ni Mwenyekiti wa CCM Tunduma, Danny Mwashiuya na Katibu wake ambao gari walilokuwa wamepanda, lilipigwa mawe na kuharibiwa vibaya.

  Hilo ni tukio la tatu kwa viongozi wa kitaifa kufanyiwa fujo katika eneo hilo.

  Hali kama hiyo ilishawahi kuwakuta Rais Jakaya Kikwete na mke wake Mama Salma pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani Nahodha.

  Pia mwaka 2009 Mwenge wa Uhuru ulilazimika kubadili njia kutokana na wananchi wa eneo hilo kupanga kupopoa mawe msafara wake.

  [​IMG]
  WAFUASI WA CHADEMA MJINI TUNDUMA MKOANI MBEYA WAKISHANGILIA HOTUBA YA MAKAMU WA RAIS KWA KUONESHA ALAMA YA VIDOLE
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Interesting people now knows weak leaders and they know how to reach to their bogus speeches...

  If U look @ the pic Regional Commissioner is just looking down, he cannot believe his ears what he hear from the people
   
 3. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  CCM: Je mwananchi gani mzalendo anakitaka?
   
 4. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  aibu sana hii,lile lizee hata kuongea haliwezi kila saa kusoma kwenye karatasi eti ana masters'ovyo kabisa
   
 5. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,094
  Likes Received: 10,451
  Trophy Points: 280
  Habari kama hizi huwa zinausuuza moyo wangu kweli khaaa....
   
 6. only83

  only83 JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Mfano wa kuigwa...good job.
   
 7. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  :lol::lol::poa
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hahaha, alipoona idadi kubwa ya mahudhurio alifikiria ni kukubalika kumbe wapo pale kwa mahudhurio ya kuzomea na ni zoezi lililofana.
   
 9. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Uzee (na si kingine chochote) ndio karata iliyompa umakamu wa Rais
   
 10. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kwenye Siasa, hii familia ya Billal wanalaniwa sana kuwa ni Weupe na hakuwafai ila unajua tena njaa.....

  Ila unapowaweka Darasani, tafadhali bana. Huyu jamaa ni mkali sana kwenye field yake ila alichukuliwa enzi ya Kigoma Malima na kuingizwa kwenye siasa kwa wimbo wa "Waislaam sasa zamu yetu."

  Akiwa wizara ya elimu kama katibu Mkuu na Mkapa kama Waziri, alikuwa na dharau kubwa sana kwa boss wake kwa kumruka mara nyingi na kwenda moja kwa moja kwa Homeboy wake Rais Mwinyi, hapo upande wa Pili wa Wizara ya elimu yaani Ikulu.

  Sijui kwa nini yeye na mdogo wake waliacha kazi wanazoziweza zaidi na kujiingiza kwenye Siasa ambazo hawaziwezi?

  Huyu si kuwa ana Masters ila ana PhD ya Nuclear Physics... Waliosoma UDSM Engineering wanamfahamu sana na kumvulia kofia yake kama mtaalam wa hayo mambo. Ila ukweli ni kuwa Physics siyo Siasa.
   
 11. Pendael laizer

  Pendael laizer JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  That's good. let's us do too.
   
 12. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Sijui kama watawala wanajifunza chochote kuhusu huu mwamko mpya wa vijana kuanza kuhoji kwanini ziara za kiserikali zijumuishe kazi za chama!
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Huko itakuwa majority ni tabaka fulani.
   
 14. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #14
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Dr bilal ni phd na aliweza kutuliza umati ule bana uwezo anao na c porojo za urojo zenu CDM
   
 15. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #15
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Iliwahi kumtokea Pinda Musoma
   
 16. mluga

  mluga JF-Expert Member

  #16
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 678
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Director

  Unasema kweli yaani mtaalamu wa aliyebobea wa nyukilia anaongea na wauza karanga lazima asome ki karatasi? ha ha ha
   
 17. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #17
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ni makamu wa rais kutokana na Uzanzibar wake tu na si uwezo.
   
 18. Yombayomba

  Yombayomba JF-Expert Member

  #18
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 23, 2006
  Messages: 818
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Sikonge,

  Huyu jamaa hakuwa COE, huyu alikuwa department ya Physics. Sasa kama ni mkali saana hebu tuambie ame publish paper ngapi? na kukufanya wewe umuone mkali saana, au amefanya nini cha ajabu hapo Physics?
   
 19. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #19
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Mkuu, yule dingi ni 'PhD holder'
   
 20. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #20
  Feb 26, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Ndio maana hata matokeo mnafutiwa, yaani umeshindwa kuelewa wananchi walitulia baada ya kitendo gani?


  Baada ya Silinde na Mwakajoka ....

   
Loading...