Dk. Bilal ana ajenda gani?

Keil

JF-Expert Member
Jul 2, 2007
2,214
801
Dk. Bilal ana ajenda gani?

Omar Maftah, Mkunazini, Zanzibar

Tanzania ni nchi yenye bahati nzuri ambayo inawapa wananchi wake fursa kubwa ya kuzungumza na kujadili mambo yanayowahusu wao au jamii katika vyombo vya habari na hata hadharani. Hivi karibuni tumekuwa tukishuhudia baadhi ya watu, wakiwamo wanasiasa, wanavyuo, wanaharakati, wanahabari na kadhalika wakizungumzia tuhuma za ufisadi dhidi ya viongozi fulani.

Hilo jambo si baya ila ieleweke kuwa mazungumzo kama hayo lazima yawe na muelekeo fulani, ama kurekebisha au kuzuia uhalifu. Si vyema hata kidogo kuyageuza mazungumzo haya au mada hii kuwa ni baraza la kujinadi kisiasa.


Inavyoonekana hivi sasa ni kwamba baadhi ya wachangiaji wa mada hiyo wamepoteza muelekeo na wamo katika kujitafutia umaarufu wa kisiasa.Kwa bahati mbaya, kiongozi mmoja ambaye aliwahi kuwa na cheo kikubwa katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amejiingiza katika sakata hilo. Huyo si mwingine ila ni Waziri Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Mohammed Gharib Bilal. Ni haki yake ya kidemokrasia, Dk. Bilal, kuzungumzia jambo liliopo midomoni mwa watu lakini azingatie ukweli wakati anapotoa maelezo yake. Inaonekana katika mazungumzo na mwandishi wa habari, Dk. Bilal alikuwa na dhamira hasa ya kutafuta baraza la kuzungumzia.


Kutokana na mazungumzo yaliyochapishwa katika gazeti moja la kila siku la Dar es Salaam, Dk. Bilal amechukua fursa ya mazungumzo ya muda ya tuhuma za kile kinachodaiwa, bila ushahidi, kuwa kuna ufisadi miongoni mwa viongozi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kugeuza kuwa baraza la kusengenya uongozi wa siasa Zanzibar. Kwa mujibu wa madai yake “CCM Zanzibar imedorora”na kwamba hivi sasa “hakuna mwamko.” Dk. Bilal alitoa madai kama haya katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.


Inafaa ifahamike kuwa Chama cha Mapinduzi kiko hai, imara na chenye kukubalika kwa wananchi walio wengi, kimeweza kushinda kwa kishindo kikubwa katika chaguzi zote kuu pamoja na ule uliofanyika baada ya madai yasiyo na msingi ya Dk. Bilal, wa mwaka 2005.

Mfano mzuri umeonekana katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huo ambao ulishuhudiwa na Waangalizi mbali mbali wa Uchaguzi wa Kimataifa. Waangalizi hao walikubali na kuridhika na mwenendo wa uchaguzi huo ambao uliendeshwa kwa amani, utulivu na ulikuwa huru na haki. Mafanikio hayo kwa upande wa CCM Zanzibar, yalitokana na uongozi mzuri wa chama uliopo wenye kusimamia Sera na Ilani ya CCM kwa umahiri mkubwa. Iweje leo kiongozi wa CCM, mjumbe wa Kamati Kuu, akurupuke na kutamka kwamba chama kimedorora? Ni vyema akaeleza wazi kama ana ajenda ya siri.


Ieleweke kuwa Chama cha Mapinduzi katika kuimarisha umadhubuti wake kimeteua viongozi wakuu kadhaa kuwa ni walezi wa Chama katika mikoa. Miongoni mwa walezi hao ni yeye Dk. Bilal ambaye aliteuliwa kuwa Mlezi wa Chama wa Mkoa wa Mjini Magharibi na pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama. Jukumu la viongozi hawa ni kushughulika na kushirikiana na wenzao kuhakikisha uimara wa chama wakati wote. Katika mfumo wa demokrasia, chama hakiongozwi na mtu mmoja bali huwa na uongozi wa pamoja (collective responsibilities).


Pia, sehemu moja ya chama haiwezi kujiendesha kama ndio chama peke yake. Sisi wana CCM Zanzibar, tumeshuhudia ushirikiano na ushiriki wa uongozi wa juu wa Chama Zanzibar, chini ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Mheshimiwa Amani Abeid Karume, ukishiriki katika shughuli zote za chama katika ngazi mbalimbali.


Kwa mujibu wa madai hayo ya Dk. Bilal inaonekana yeye hakuwa mshiriki katika shughuli hizo za chama au hakuwa akitekeleza dhamana zake za uongozi alizokabidhiwa, kwani ingekuwa rahisi kwake kubaini uhai na uimara wa CCM kama angekuwa mtekelezaji mzuri wa majukumu yake ya Mlezi wa CCM katika Mkoa wa Mjini Magharibi. Hiyo ni hasara kubwa kwa mtu kama yeye.


Uimara na uhai wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar unakwenda sambamba na uendeshaji imara wa Serikali ya Mapinduzi. Serikali hiyo katika kipindi hiki tokea mwaka 2000 imekuwa na mafanikio yanayoonekana na yanayotolewa sifa na nchi za nje pamoja na mashirika ya kimataifa. Hawezi mtu ye yote, seuze kiongozi wa CCM, kudai kuwa chama ambacho kinaendesha serikali hii, kimedorora ila mtu huyo anaishi nje ya mazingira ya Zanzibar na hataki kukubali ukweli uliopo.


Tumeshuhudia na kusikia mara kadhaa viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakitangaza ukweli kwamba nchi yetu imo katika mapambano dhidi ya umasikini. Wakati huo huo, sisi sote ni mashahidi wa jitihada na hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi, katika kutatua matatizo yaliyopo na kuhakikisha kuna maendeleo ya jamii na uchumi yanayowanufaisha watu. Maendeleo yaliyofikiwa katika elimu kwa kufikia malengo ya Milenia kabla ya 2015, afya na miundombinu zikiwamo umeme vijijini na barabara ni ushahidi wa kutosha wa kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Mapinduzi inayoongozwa na CCM.


Aidha, mipango kama ya Mpango Mkuu wa Maji Zanzibar Mjini ni mojawapo tu ya mipango mingi iliyo katika utekelezaji. Sisi wananchi tunaamini kuwa kufikia mwaka 2010 mafanikio makubwa zaidi yatakuwa yamepatikana.


Kama raia mwema, ningelipenda kumshauri Dk. Bilal awe kiongozi anayeshirikiana na wenzake na pia awe mkweli katika kutetea uhai na uimara wa chama chake ambao upo dhahiri kwa watu wote. Katika kuendesha kampeni, ni vyema atumie sifa bora zilizomo ndani ya Chama badala ya kujaribu kuchafua uongozi imara uliopo ambao yeye ni miongoni mwake akiwa mlezi wa chama, au ameshindwa katika jukumu hilo? Pia, Dk. Bilal ameonekana kupitiwa kutolitumia gazeti la “Uhuru” la chama ambalo yeye ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya gazeti hilo badala ya kutumia vyombo vingine.


Kuhusu sakata la tuhuma za ufisadi, Dk. Bilal bila ya shaka anaelewa msimamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa Serikali inachunguza yote yaliyosemwa na kwamba sheria ichukue mkondo wake baada ya uchunguzi kukamilika na iwapo makosa yatabainika. Si vyema kwa watu kujifanya wachunguzi, askari, waendeshaji mashitaka na mahakimu.


Kama kada wa chama, Dk. Bilal awe wa mwanzo kutii maagizo ya Mwenyekiti wa chama chake.


Source: HabariLeo
 
Kwa nini huyo Omar anamchagulia Balali kisemeo? Kwani kwenye katiba ya CCM lazima ukasemee kwenye gazeti la Uhuru?

Na jingine, bado tupo kwenye enzi za 'zidumu fikra sahihi za mwenyekiti'? I mean ina maana wanachama waheshimu kila wanachosema wenyeviti wao hata kama hawaoni mantiki katika hayo?

Nadhani Balali analindwa na uhuru wa msingi wa katiba unaompa haki ya kutoa mawazo yake (section 18)

Kwangu mimi hii ni counter attack to hakuna zaidi
 
Dk. Bilal ana ajenda gani?

Omar Maftah, Mkunazini, Zanzibar

1. Inavyoonekana hivi sasa ni kwamba baadhi ya wachangiaji wa mada hiyo wamepoteza muelekeo na wamo katika kujitafutia umaarufu wa kisiasa.


2. Kwa bahati mbaya, kiongozi mmoja ambaye aliwahi kuwa na cheo kikubwa katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amejiingiza katika sakata hilo. Huyo si mwingine ila ni Waziri Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Mohammed Gharib Bilal.3. Ni haki yake ya kidemokrasia, Dk. Bilal, kuzungumzia jambo liliopo midomoni mwa watu

FULL STOP AND STOP IT ANYTHING MORE OR LESS IT IS A SPINNING, AND I HATE IT
 
Dk. Bilal ana ajenda gani?

Omar Maftah, Mkunazini, Zanzibar

Tanzania ni nchi yenye bahati nzuri ambayo inawapa wananchi wake fursa kubwa ya kuzungumza na kujadili mambo yanayowahusu wao au jamii katika vyombo vya habari na hata hadharani.

Kwa bahati mbaya, kiongozi mmoja ambaye aliwahi kuwa na cheo kikubwa katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amejiingiza katika sakata hilo. Huyo si mwingine ila ni Waziri Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Mohammed Gharib Bilal. Ni haki yake ya kidemokrasia,

Source: HabariLeo
Bahati mbaya??? Umeanza vizuri kujenga hoja. Ghafla, umegeuka. Unasema Bilali kutumia demokrasia kutoa maoni yake ni bahati mbaya!!! Then, unaendelea....Ni haki yake ya kidemokrasia!!!

Dk. Bilal ana ajenda gani?

Omar Maftah, Mkunazini, Zanzibar

Kutokana na mazungumzo yaliyochapishwa katika gazeti moja la kila siku la Dar es Salaam, Dk. Bilal amechukua fursa ya mazungumzo ya muda ya tuhuma za kile kinachodaiwa, bila ushahidi, kuwa kuna ufisadi miongoni mwa viongozi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano
Source: HabariLeo

Omar Maftah, umejaribu kumuhoji Dr.Bilali kwa nini amejiingiza kwenye hilo sakata??? Una uhakika kuwa Dr.Bilali hana ushahidi kama ulivyodai hapo juu??? Nenda kamshitaki mahakamani basi. Sheria ichukue mkondo wake.

Dk. Bilal ana ajenda gani?

Omar Maftah, Mkunazini, Zanzibar

Inafaa ifahamike kuwa Chama cha Mapinduzi kiko hai, imara na chenye kukubalika kwa wananchi walio wengi, kimeweza kushinda kwa kishindo kikubwa katika chaguzi zote kuu pamoja na ule uliofanyika baada ya madai yasiyo na msingi ya Dk. Bilal, wa mwaka 2005.
Source: HabariLeo

Chukueni challenges zinazotolewa na wapinzani kama compliments. Ni kweli CCM iko hai lakini inanuka kila harufu ya uchafu. Kuwa hai tu pekee haitoshi. Jisafisheni.

Dk. Bilal ana ajenda gani?

Omar Maftah, Mkunazini, Zanzibar

Iweje leo kiongozi wa CCM, mjumbe wa Kamati Kuu, akurupuke na kutamka kwamba chama kimedorora? Ni vyema akaeleza wazi kama ana ajenda ya siri.

Source: HabariLeo

Ndiyo dhana halisi ya demokrasia hiyo. sio kukurupuka.

Dk. Bilal ana ajenda gani?

Kama raia mwema, ningelipenda kumshauri Dk. Bilal awe kiongozi anayeshirikiana na wenzake na pia awe mkweli katika kutetea uhai na uimara wa chama chake ambao upo dhahiri kwa watu wote.

Source: HabariLeo

Bilali anachofanya hapa ni kutetea uhai wa chama. Unatumia vigezo vipi ku-judge ukweli wa hoja zinazotolewa na Bilali???

Dk. Bilal ana ajenda gani?

Kama kada wa chama, Dk. Bilal awe wa mwanzo kutii maagizo ya Mwenyekiti wa chama chake.

Source: HabariLeo

Wewe unataka kumchafua bilali bila kuwa na sababu za msingi hapa. Njoo na hoja zingine. Your hoja are baseless and futile.
 
Inafaa ifahamike kuwa Chama cha Mapinduzi kiko hai, imara na chenye kukubalika kwa wananchi walio wengi, kimeweza kushinda kwa kishindo kikubwa katika chaguzi zote kuu pamoja na ule uliofanyika baada ya madai yasiyo na msingi ya Dk. Bilal, wa mwaka 2005.

Na ni kwa nini Dk Bila alilazimishwa kuondoa jina lake katika kinyang'anyiro kama sisiemu kuna demokrasia ya kutosha? Kwa nini asingeachwa?
 
I am still curious on what really took place in Chimwaga 2005! if anyone will bring forth what happened to Mzee Malecela, Salim, Mwandosya and Bilal nitashukuru sana!

I guess Bilal anajiunga na Butiku!
 
Bilali ni Mtanzania mwenye haki kama wengine wote tulivyo na haki a kusema siasa, ndio maana sasa wanamkingia Mkapa, na maneno ya kuwa akiwa rais hawezi kushitakiwa,


Sasa hapa wanajaribu kusema kwama Bilali, haruhusiwi kusema maana alikuwa waziri kiongozi, mbona hawajatoa hizi spinning against Butiku, au Mwinyi na JM, maana wanajua kuwa hao ngoma ni nzito, wakimgusa Butiku, atawamaliza, sasa wameamua kuonea dagaa Bilali,

Hiyo article ni spinning ya wanaoguswa na tuhuma za ufisadi, huyo mwandishi ametumiwa tu au na yeye anahusika!

Bravo Bilali!
 
hayo mapambano ya kinyang'anyiro cha urais wa zanzibar, inaonekana makundi yanaanza kujipanga.

kazi ipo, tutaona mengi ikiwemo siasa chafu
 
Mzee ES leo unasema wanakwepa tuhuma za Ufisadi wana cook stories? Kumbe umafia wa CCM sasa unawatafuna wenyewe ? Je unaukubali Ufisadi uliosema na Slaa ama bado unazidi kusema Serikali ichukue hatua ili Slaa na wenzake waende jela as you suggested ?

Kwa heshima na taadhima mkuu nisaidie kujibu haya .
 
Mzee ES,Lunyungu, DAR-SI-LAMU,Rev.Kishoka,Mtupori,

Dr.Bilal naye ni fisadi tu. Udini,Uzanzibari,Rushwa, aliopandikiza akiwa PS wa Higher Education ulikuwa Ufisadi.

Siamini kama huyu bwana anafaa kuwa Raisi wa Zanzibar. Ni kweli ana elimu nzuri lakini kijamii ni mtu hatari.
 
joka kuu hebu tunsheleze kuhusu huyu dr, maana mie mmekusudia kura yangu kumpa yeye, kama kuna info nzito nitumie kwenye pm.

na unaona nani kule anatufaa? shamhuna?
 
Mzee ES,Lunyungu, DAR-SI-LAMU,Rev.Kishoka,Mtupori,

Dr.Bilal naye ni fisadi tu. Udini,Uzanzibari,Rushwa, aliopandikiza akiwa PS wa Higher Education ulikuwa Ufisadi.

Siamini kama huyu bwana anafaa kuwa Raisi wa Zanzibar. Ni kweli ana elimu nzuri lakini kijamii ni mtu hatari.

Watu wengi waliokuwa wanasoma Urusi miaka ya tisini wakati yuko Sayansi na Elimu ya juu walikuwa wanamlalamikia sana.
 
jokaKuu

JF Senior Expert Member
-----------------------------------------------------------------

Mzee ES,Lunyungu, DAR-SI-LAMU,Rev.Kishoka,Mtupori,

Dr.Bilal naye ni fisadi tu. Udini,Uzanzibari,Rushwa, aliopandikiza akiwa PS wa Higher Education ulikuwa Ufisadi.

Siamini kama huyu bwana anafaa kuwa Raisi wa Zanzibar. Ni kweli ana elimu nzuri lakini kijamii ni mtu hatari.


Mkuu jokaKuu,

Mkuu heshima mbele, una-raise a very good point, huyu wengi hatumfahamu kwa undani, lakini nimeshawahi kusikia kuwa ana
some uchafu huyu,

na the fact kwamba Mkapa, alipotoka huko kuingia Ikulu, aliwarusha vyeo wale wote aliokuwa "akila" nao yaani huyu, na Mahalu, kwa kweli ni vyema kama ungetuwekea dataz zaidi kama unazo maana hatumjui vizuri huyu, ila for some reasons I do not know, huwa tunaambiwa sana kuwa ndiye anayekubalika hata na CUF, je ni kweli?
 
Kwa kweli ni vyema kama ungetuwekea dataz zaidi kama unazo maana hatumjui vizuri huyu, ila for some reasons I do not know, huwa tunaambiwa sana kuwa ndiye anayekubalika hata na CUF, je ni kweli?

Mkuu FMES,

Kwanini anakubalika kwa CUF? Si CUF hawa hawa ambao walikuwa na ugomvi mkubwa sana na Komandoo? Komandoo inajulikana wazi kwamba ni best wa Dr. Bilal, leo hii inakuwaje akubalike kwa CUF? Ama ndo kampeni za 2010??????????
 
hapo ndio pa kujiuliza sana, kuna msemo unasema adui yako akionesha kukupenda ujue sio bure. sasa sijui kwa nn cuf wanonesha kumpenda? jee wanahisi ni rahisi kwao kumuangusha au ni mtu mwenye kupenda umoja kwa hiyo akipita yeye na wao hatawasahau na hawatoteseka?
 
Mtu-wa-Pwani,

Dr.Bilali anaweza kuwafaa wazanzibari lakini kwetu wabara sidhani kama atatufaa kitu.

Wakati Mkapa,Bilal,na Mahalu, wapo wizara ya elimu ya juu, kulikuwa na mambo mabaya sana yaliyokuwa yanaendelea.

Rushwa, Udini, Ubara, Uzanzibari, vilikuwa vikionekana waziwazi. Ni sababu hiyo ndiyo inayonifanya niwatilie shaka wazee wetu hawa.
 
Kwanini anakubalika kwa CUF? Si CUF hawa hawa ambao walikuwa na ugomvi mkubwa sana na Komandoo? Komandoo inajulikana wazi kwamba ni best wa Dr. Bilal, leo hii inakuwaje akubalike kwa CUF? Ama ndo kampeni za 2010??????????

Mkuu Keil,

Heshima mbele, mkuu hizi siasa za visiwani sizielewi kabisa, Komandoo alikuwa adui wa CUF, Bilali ni mtu wa komandoo, alkini anayekubalika na CUF, kama ninavyosikia huko visiwani,

Sasa na mimi mkuuu I am lost?
 
Mkuu Keil,

Heshima mbele, mkuu hizi siasa za visiwani sizielewi kabisa, Komandoo alikuwa adui wa CUF, Bilali ni mtu wa komandoo, alkini anayekubalika na CUF, kama ninavyosikia huko visiwani,

Sasa na mimi mkuuu I am lost?

Kabisa, inafaa tuelimishwe kuhusu siasa za Zenji.
Pia inawezekana Bilal akawa alibana maslahi ya wakubwa siku za nyuma ndio maana anabaniwa leo, tutasikia mengi sana kumhusu.
Hamjasikia jamaa aliyeachishwa kazi kwa majungu pale wizara ya Elimu?
 
DR BILAL hana ajenda yoyote
ila kasema
si unajua aliye sema kasha sema.
kinachobaki ni maumivu au starehe.
tena wana ccm wazuri ni wale wanaosema kuliko kuongelea vijiweni au chumbani.
kumbuka katiba ina linda wanao ongea ilimradi hawavunji sheria za nchi.
asante
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom