Dk Batilda Burian kuwalipia vijana wote Arusha kodi ya nyumba wakimchagua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Batilda Burian kuwalipia vijana wote Arusha kodi ya nyumba wakimchagua

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Gerad2008, Oct 27, 2010.

 1. Gerad2008

  Gerad2008 JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni(farao)
  siku za mwisho wa kampeni zinavyozidi kwisha ndivyo na wagombea ubunge wasiokubalika kama Dk. Batilda Buriani wanavyozidi kuchanganyikiwa na kujikuta wakitoa ahadi ambazo za kuwatia hasira wapiga kura.

  Jana pale Moshoni stendi Batilda aliwaahidi wapiga kura vijana kwamba wakimchagua atawalipia wote kodi za pango na wataishi nyumba za kupanga bure bwerere!!!!.

  Jamani jamani huyu mama atatoa wapi hizo hela za kuwalipia vijana zaidi ya laki 5 kama siyo kutaka kutuambia yeye ni fisadi na anataka kutakatisha hela chafu.

  Kwa kweli wananchi walilalamika sana kwani hakuna aliyetarajia kama huyu DK siku za mwisho atapoteza hata zile kura chache alizotegemea kupata.

  Wazee, vijana na akina mama wameshtuka na WAMEAPA ATAWATAMBUA SIKU YA TAREHE 31/10/2010 kama wao ni Mazezeta au watu na akili zao

   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  pIGA RUNGU KWA KUTUMIA KURA YAKO!
   
 3. Gerad2008

  Gerad2008 JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Mwache atape tape hajui majumbani tulishamaliza kupiga kura tunasubiri tu hayo masanduku yao tutie karatasi zetu
   
 4. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kaishiwa sera huyo. Kwanza hana mvuto na ni bora kiongozi.
   
 5. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Halafu atakuwa analala nao au atawalipia tu, basi?
   
 6. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Inafurahisha....Are you serious? Atajuaje sasa kijana yupi alimpigia kura?
  Hilo tamko latosha kujua kuwa anakwenda bungeni kufanya biashara...No free lunch :nono:
   
 7. awesome

  awesome Member

  #7
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu mama anatufanya sie wajinga kabisaaaaaaaaaaaaa........... Cha msingi kilichobaki ni kutompa kura hata moja ili akawalipie wazenji kodi ya nyumba asituzingue.
   
 8. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2010
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hii kali...
   
 9. M

  MathewMssw Member

  #9
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kadiri siku za zinavyozidi kukaribia na ndipo utamu wa unazidi!
   
 10. K

  KIURE Member

  #10
  Oct 27, 2010
  Joined: May 8, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu mama si ndio alikuwa Chief Whip pale bungeni siku wanamfungia Zitto au mmesahau? Huyu alisema Zitto anasea uongo akaungwa mkono na machizi wenzie akiwapo Mudhihir, Malechela, n.k. Anapaswa kulipia dhambi ile sasa, asipewe kura hata mmoja ili arudi akapambane na mke mwenza kule Zenji!
   
 11. L

  Lubaluka JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 496
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Duuuu!!! kazi ipo mwaka huu !!! kama ni kweli alinena hayo na kuhaidi hio ahadi hadharani basi sina neno tena juu yake ... Kwanza hastahili picha yake kuwepo hata kwenye karatasi za kupigia kura, bora pawe kivuli !!!

  My God bless Tanzania.
   
 12. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  kama anazo basi alipe advance kabisa kisha mpigeni na chini tarehe 31/ hawa ndio wanaochapisha fedha bandia atazitoa wapi pesa zote hizo. jamani mwambieni atoe kwanza kisha ataisikilizia kimoyomoyo tarh 31. Msidanganyike watu wanatapatapa sasa milango imefungwa hamna pa kukimbilia. Trh 31 tunagong'oa mafisadi na mizizi yao mmoja baada ya mwingine.
   
 13. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Pale soko kuu alishawahi kupondwa matango hata huko Moshono mlitakiwa mmtimue maana kuna maneo ambayo haya vumiliki eti atawalipia kodi ya vyumba mimi hata sitaki kuamini kama aliwatuka wakazi wa Moshon kiasi hicho
   
 14. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hawezi kutekeleza ahadi hii,hata kama ni fisadi!!
   
 15. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Vijana msije danganyika hata kidogo, kama kweli anazo awape advance ya miaka 5 lakini tarehe 31 mnampiga na chini. Mafisadi wamebanwa kila kona hakuna pa kutokea mwaka huu na msikubali hata kidogo. rambeni chenu mapema kisha terehe 31 yeye ataisoma kimoyomoyo. Tena hakuna muda wa kupoteza alikuwa wapi kulipa siku za nyuma. Kikaango kinachemka mafuta tunasubiri tarehe 31 tu. Angalieni vijana maana wengine wataweza kutoa hata rushwa ya n.......hi. Msikubali :israel:
   
 16. Gerad2008

  Gerad2008 JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Hata ilipotimia tarehe 31/10/2010 saa 10 jioni' JK na wabunge na Madiwani wao wakapaaza sauti kwa uchungu wakasema" WAPIGA KURA WAPIGA KURA JE MMETUAACHA" walipomaliza kusema hivyo wapiga kura wakanyamaza kimya huku wakifuatilia na kuchunga kura zao. Na ilipofika tarehe 1 November 2010, CCM IKASALIMU AMRI HUKU ikikubali matokeo na kusema "TUMEKWISHA!!!!!!!. Na woote waliosikia maneno hayo wakashangilia kwa furaha huku wakiruka ruka na kusema MABADILIKO, MABADILIKO YAMEKUJA NA CCM BYE BYE!!!!!
   
 17. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  hivi huyu mama ni mjinga kiasi hiki?!!!!
   
 18. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #18
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Teh teh Wana JF,

  Kwa akiri ya haraka haraka kabisa ni kuwa huyu Mgombea CCM jimbo la arusha mjini hukufafanua hilo la nyumba bure nacho dhani a ni kuwa mmoja atafanya mbinu zake esp kwenya swala la malipo ya kodi katka halmashauri hiyo kupunguza na watu kulipa kodi kwa bei ya chini sana na pili nilivyo mwelewa either kuna mradi unategemea kuanzisha hapo Mjini Arusha ambao wananchi wengi wa mji huo watafaidika na mradi huo wa majumba mapya na nina wasi wasi sana kama sio mradi wa PPF,NSSF au msaada kutoka Japani au China utatupiwa mkoani hapo sasa mama alisha ichungulia hiyo Deal

  Tatu twasikia ati Manager Campaign wake aliye anza nae Mwalusamba -Mwenyekiti UVCCM - wilaya ya Arusha-Mjini katemwa kuwa manager Campaign na amewekwa mwingine.

   
 19. j

  jack chance Member

  #19
  Oct 27, 2010
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimesikia kuna mkakati kabambe wa kuiba kura hapa arusha, namwomba Ndg G. Lema na kamati nzima ya ushindi CHADEMA iweke mikakati madhubuti kwa siku hizi zilizosalia ili hata kura moja mwaka huu isiibwe au kuongeza kura feki, mwana Arusha mwenye simu ya Leme tupeane ili data tunazopata tuzitawanye kiurahisi.
   
 20. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Sasa mijihela yote hiyo ya kuwalipia kodi anang'ang'ania ka-ubunge ili iweje....iko namna si bure..
   
Loading...