Dk Bashiru: Vyama vya upinzani vitakufa kimoja baada ya kingine

Mnamshangaa Dr wa kuokotwa majalalani? Muuluzeni kwenye uchaguzi CCM wameshinda kwa asilimia ngapi ya waliojiandikisha kupigwa kura?
Nakumbusha kwa kumnukuu CCM hawajawahi pigiwa kura na asilimia 30 ya wanaostahili kupiga kura.
Mambo ya Kanda ya Ziwa
 
Ni ULEVI tu wa MADARAKA! Wanafika wakati wanajitoa UFAHAMU! Wanatuona watanzania kama PUMBA tu! Hatuna akili! Hatuna ufahamu! Hivi mtu mwenye Akili TIMAMU unaweza kumwambia hivyo wakati kila mtu ANAJUA vyama vya upinzani VINAFANYWAJE?
 
Baba anaogopa watoto wake mwenyewe hadi anawaombea kifo.Hii kali.Hawa watu kwenye hicho sijui wananyweshana nini maana wote wakiongea ni ugoro mtupu.
 
"Kwa hisani ya watu wa marekani " inakaribia ukingoni. Siku tukianza kulipia ARVs, dawa za TB na chanjo za watoto,akili itarudi.
 
Dr ameongea maneno ya kiubaguzi
Hazingatii haki ya upinzani
Hawajaweza na hawataweza hata siku 1 kuwashinda wananchi
Wameonyesha ujasiri wa roho mbaya na ulafi wa madaraka
Hakuna mamna njema ya kuongoza isipokua hila
Matamshi yake ni hatari kwa ustawi na usalama wa taifa
Si kazi ya chama tawala kulinda usalama wa taifa isipokua taasisi zinazosimamia usalama wa taifa
Misingi yao mibovu na sera zisizotekelezeka wanageuza upinzani kuupa picha ya ugaidi
Ni aibu mnoo

Ipo siku hao wanyonge watakua mbogo hata ikiwa ni chini ya utawala usiokua na vyama vya upinzani

Utaona kuwa ni viongozi wa majina tu,ila wamekosa maono na usimazi dhabiti


Swala si upinzani uongoze ila ni namna ipi wananchi wanapata mateso katika utawala wao


Dr awaze mara mbili si kutoa kauli za kizembe
 
Shame on him! Too low for a Ph.D. Watu wa ajabu sana hawa! Hii ndiyo siasa wanayotaka vyama shindani vifanye! Kuombea mshindani wao afe badala ya kukijenga kwa wananchi! Hapana ubishi wowote kuwa baada ya uchaguzi wa 2015 kuna wanasiasa wa ccm wame-panick kupita kiasi na kupoteza kabisa ustaarabu, utu na rationality. These people are so desperate wanaweza kutuharibia nchi! Wamewazuia wenzao kufanya siasa! Wamewafunga jela! Wamempa Msajili wa vyama nguvu za kisheria kuua vyama shindani! Wamewazuia kushiriki uchaguzi!
 
Katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema vyama vya upinzani nchini Tanzania vitaendelea kufa kimoja baada ya kingine kwa kuwa vinashindwa kufanya siasa vikubalike kwa wananchi.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Novemba 27, 2019 wakati akizungumza na viongozi wa chama hicho tawala Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Amesema baadhi ya vyama hivyo huibuka wakati wa uchaguzi jambo linalovifanya vishindwe kukubalika.

Amesema kwa msingi huo, CCM kitaendelea kuimarika zaidi, akibainisha kuwa udhaifu wa vyama vingi vya upinzani ni kukosa watu sahihi wa kuviongoza.

“Adui wa vyama vya upinzani yupo ndani mwao wenyewe wasitafute mchawi lazima wakubali kubadilika,” amesema Dk Bashiru.


Source: Mwananchi
Vitauwaw
 
Back
Top Bottom