Dk Bashiru: Msiihusishe Serikali na matukio ya watu kutekwa

Dk Bashiru: Msiihusishe Serikali na matukio ya watu kutekwa,

By Joseph Lyimo, Mwananchi jlyimo@mwananchi.co.tz

Simanjiro. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Dk Bashiru Ally amesema si sahihi kuihusisha Serikali ya Tanzania na matukio ya utekaji wa watu.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Julai 11, 2019 katika kata ya Naisinyai wilayani Simanjiro katika siku yake ya kwanza ya ziara yake mkoani Manyara.

Amebainisha kuwa baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanatoa taarifa potofu kuhusu watu wanaotekwa na kupotea na kuhusisha matukio hayo na Serikali.

"Ulinzi na usalama ni wajibu wa Serikali, baadhi ya watu kuihusisha (Serikali) na watu wasiojulikana wanaoteka watu hapo watakuwa wanaoichonganisha na watu wake," amesema Bashiru huku akibainisha kuwa mwenye jukumu la kutoa taarifa katika Mkoa ni Mkuu wa Mkoa na kamanda wa polisi wa Mkoa.

“Hao wawili ndio wanapaswa kutoa taarifa ya hali ya ulinzi na usalama ya Mkoa na si viongozi wengine wanaochafua hali ya hewa kwenye mitandao ya kijamii," amesema Bashiru.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Mkoa huo amesema Serikali imepiga hatua kwenye miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu, afya, miundombinu ya barabara, umeme na maji.
Bashiru naye yuko mexani, hauhusiwi kusema. Tukiwa tunakula hatusemi! naye ameshakengeuka! Ya Mtue Mohamed SAW ameshayaweka kando
 
Kuitetea CCM inabidi uweuke haswaa ujitoe ufahamu yhn uwe mwehu kwelikweli.
Uko sahihi kwa 100% mkuu.
tapatalk_1558852188968.jpeg
 
Hawa wana ccm nasubiri tu ujio wa Yesu nione nyuso zao na mioyo yao itakavyoteseka. Haki ya Mungu nitawasogezea magogo makubwa ya kuwachoma moto
 
Huwaga nina hamu ya kumjua mchawi ndani ya ccm, maana ukiingia tu kule, lazima zikutoke.
 
Usalama kuwa wajibu wa serikali hakuifanyi serikali isiweze kukiuka wajibu wake.

Zzaidi, usalama ni wajibu wa kila Mtanzania, kwa hiyo, wananchi tunapoona serikali inakiuka usalama au kuzembea kuhakikisha usalama, tutasema hilo.

Hizi habari za "Ulinzi na usalama ni wajibu wa Serikali, baadhi ya watu kuihusisha (Serikali) na watu wasiojulikana wanaoteka watu hapo watakuwa wanaoichonganisha na watu wake," ni logical non sequitur.

Alichosema Bashiru ni kama vile ukiwa na wajibu wa kulinda hela benki huwezi kuiba hela, kwa sababu tu una wajibu wa kulinda hela.

That is some ridiculous malarkey.
 
Maprofesa majalala wanazidi kuongezeka mambo ni mengi mnoo muda mchache , nlichogundua hawa watu si kwamba hawana akili ila wanajitahidi kucopy na baba yao ndio maana wanajichetua, ila ni aibu sana zaidi ya aibu sijui wake zao hawawaambiaga wakiwa vitandani kama mume wangu unajiaibisha sijui wakoje hawa binadamu, yaani ukienda Ccm kichwa inakuwa kopo kabisaaa
 
Wanafunzi wake aliowafundisha UDSM wanamshangaa sana mpuuzi huyu. Wanasema yule aliyewafundisha chuoni na huyu mpuuzi wa ccm wakikutana watauana maana ni watu wawili tofauti kabisa.
😂😂😂😂
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Dk Bashiru Ally amesema si sahihi kuihusisha Serikali ya Tanzania na matukio ya utekaji wa watu.

"Ulinzi na usalama ni wajibu wa Serikali, baadhi ya watu kuihusisha (Serikali) na watu wasiojulikana wanaoteka watu hapo watakuwa wanaoichonganisha na watu wake," alisema Dr. Bushiru
Kwa kweli ujumbe aliouwakilisha kwa wananchi ni kwamba ulinzi na usalama si jukumu la serikali na hivyo serikali isilaumiwe matukio ya utekaji wa watu yanapotokea, kweli? Kwa maneno mengine ni kwamba watu wanaodai ulinzi na usalama ni wajibu wa serikali wanafanya hivyo wakitaka tu kuichonganisha serikali na watu wake. Hakika huu ni ushahidi wa umbumbumbu usio kifani na huweza kutolewa tu na wenye phD feki na kwa Tanzania watu kama hawa hii ni awamu yao wanaimiliki.
 
Dk Bashiru: Msiihusishe Serikali na matukio ya watu kutekwa,

By Joseph Lyimo, Mwananchi jlyimo@mwananchi.co.tz

Simanjiro. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Dk Bashiru Ally amesema si sahihi kuihusisha Serikali ya Tanzania na matukio ya utekaji wa watu.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Julai 11, 2019 katika kata ya Naisinyai wilayani Simanjiro katika siku yake ya kwanza ya ziara yake mkoani Manyara.

Amebainisha kuwa baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanatoa taarifa potofu kuhusu watu wanaotekwa na kupotea na kuhusisha matukio hayo na Serikali.

"Ulinzi na usalama ni wajibu wa Serikali, baadhi ya watu kuihusisha (Serikali) na watu wasiojulikana wanaoteka watu hapo watakuwa wanaoichonganisha na watu wake," amesema Bashiru huku akibainisha kuwa mwenye jukumu la kutoa taarifa katika Mkoa ni Mkuu wa Mkoa na kamanda wa polisi wa Mkoa.

“Hao wawili ndio wanapaswa kutoa taarifa ya hali ya ulinzi na usalama ya Mkoa na si viongozi wengine wanaochafua hali ya hewa kwenye mitandao ya kijamii," amesema Bashiru.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Mkoa huo amesema Serikali imepiga hatua kwenye miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu, afya, miundombinu ya barabara, umeme na maji.
Bado inakuuma mtu kuwa na PhD. Una wivu wa kike, tafuta yako ili roho itulie
 
Back
Top Bottom