Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
Dk. Banna aliwashauri kuwafanyia tathimini mkakataa. Haya sasa Lowassa kaondoka na wengine watafuatia. It's the matter of time.View attachment 882409
Wachambuzi wa masuala ya siasa nchini kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pamoja na RUCU, wamevitaka Vyama vya Upinzani nchini kujifanyia tathimini kufuatia hamahama ya Makada wao wa udiwani zaidi ya 100, pamoja na wa ubunge wapatao sita.
Dk. Benson Bana (UDSM) alisema huenda kuna tatizo linaloendelea ndani ya Upinzani na linatakiwa kutafutiwa ufumbuzi haraka. "CHADEMA iache kukimbia tatizo wanapaswa kujiuliza kwa nini yanatokea wakati huu?"
Dk. Bana alieleza kuwa, "Wajifungie wafanye tathimini, kama hawawezi kujifanyia wawatafute hata watu wa nje .... binafsi nipo tayari kufanya hivyo tena bure kabisa."
Naye Dk. Richard Mbunda (UDSM) alieleza kuwa, hakuna sababu ya Wapinzani kuendelea kulalamika bila kurudisha imani yake kwa wananchi. "Kuendelea kulalamika siyo suluhu, wanatakiwa kupambana, siasa ni mapambano."
Prof. Gaudence Mpangala (RUCU), alivishauri Vyama vya Upinzani kujiunga na kupambana na hali inayoendelea. "Hata CHADEMA wakija na Sera mpya hawatafanikiwa katika mazingira haya. Lazima watatue kiini cha tatizo."
Profesa Mpangala aliongezea kuwa, "Ni lazima watambue kuwa, mkakati uliopo ni kuua Upinzani nchini, Sasa wakitambua hilo ninaamini watachukua hatua stahiki."
‘Upinzani wajitathmini hamahama ya wabunge’