eliesikia
JF-Expert Member
- Oct 29, 2010
- 787
- 755
Dk. Bana mkuu wa kitivo cha siasa na bosi wa REDET leo asubuhi akiwa na David Kafulila alitoa kauli zenye busara ya utata...
Kwa nini nasema BUSARA YA UTATA???
Yeye kwa minajili ya kujiweka sawa na kusema kuwa kitendo cha CHADEMA kimehatarisha utamaduni kwa kuwa vijana huiga wanachokiona.. Akaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa ipo siku kiongozi wa upinzani anaongea bungeni na CCM wakatoka nje..
Baadae kidogo akaongezea kwamba CHADEMA wapeleke hoja binafsi ya tume huru na katiba..( huku akijua fika kuwa katiba mpya ilizua mijadala toka bunge la 7 lililokuwa na vyama vingi)..
Akashauri CHADEMA wakishindwa basi waende kuwaeleza wananchi kama walivyozoea... Hayo mengine acha kabisa hili la mwisho ndio alinishtua kwa kuwa linapingana na marejeo yake hapo juu..
TAFAKURI:
Je Dk. Bana anajua tafsiri ya kwenda kwa wananchi na kusema tume haikuwa huru na Raisi alichaguliwa kwa kuchakachua???
Mimi nahisi ulimi wake uliteleza lakini si kweli kwa kuwa pia hata kwenye gazeti la Mwananchi nimemnukkuu akisema hayo ya kwenda kwa wananchi...
Huku akinajisibu kuwa kutoka Bungeni kunahatarisha amani na usalama wa taifa... Alishawahi kuwaza kilichotokea Kenya ilikuwaje au 2001 kule Zanzibar???
Mimi napingana sana na huyu kibaraka wa CCM ambaye anajaribu kujenga busara tata kwenye mambo mazito.. Yeye kama kada wa CCM anadhani kuwa anaweza kushawishi jamii kuwa kitendo cha CHADEMA ni maadili kushuka na utomvu wa nidhamu... Sasa anajaribu kutaka kupoteza taifa kabisa...
Hivi anajua watu wangapi wanaunga mkono CHADEMA achana na hao waliosusa kupiga kura wakiwana uhakika kuwa kura zao zitaibiwa...
.Huyu mzee ashauriwe aishie hapohapo na huo ushauri wake kwa CHADEMA waitishe mihadhala kama njia sahihi kwa kuwa hajui kitakachotokea hapo na hiyo chuki dhidi ya Raisi itakapofikia.. Ni hatari saana...
Maoni aliyotoa kwenye Mwananchi Newspaper na StarTV yanafanana sana lakini namshauri aachane na hicho anachowaza kwa kuwa CHADEMA ni chama kikubwa tofauti na anavyodhani wana-uwezo wa kuleta chuki ya hatari sana hapa nchini dhidi ya CCM lakini tunaepukana na haya kuepusha shari..
USHAURI: CHADEMA waendelee kutomtambua raisi mpaka pale atakapowaita na kuwaambia waongee ili waweze kumtambua kwa yeye kukubali katiba mpya na tume huru...
Naomba kutoa Hoja
Eliesikia