Dkt. Abbas: Ndege tunanunua na huduma za kijamii tunawekeza fedha za kutosha, wanunaji waendelee kununa

Msemaji wa serikali amesha tolea majibu kuwa, mwezi huu wa march mtalipwa malimbikizo yenu ya mshahara, na pia kafafanua vizuri tu kuwa kwa mujibu wa miongozo hatakiwi kabisa taasisi ya serikali au wizara kutengeneza au kulimbikiza madeni ya watumishi wake. Nakusihi kuwa na amani malipo yenu ya malimbikizo yanalipwa mwezi huu.
Hizi ngonjera Zina muda mrefu Sana lakini huo muda wa malipo haijawahi fika zaidi mnaongeza madeni.
 
Hivyo wale wanaonuna wakiona madaraja na mabwawa ya kufua umeme yanaendelea kujengwa basi wajiandae " kununa" zaidi kwani mengi mazuri yanakuja, amesema.
Yaani sijawahi kuona watu ambao hawana Busara kama hii Awamu. Hivi anadhani hapo kazi yake ni mipasho ?, Hao anaongea nao ni walipa kodi kwahio hata kama hawafurahii matumizi ya Kodi zao, ni vema wakaeleweshwa / wakabembelezwa na sio Kubezwa.

After all Kodi zao bado zinatumika (uongozi ni kuunganisha watu na sio kuwatenganisha) hivyo hawana budi kufanya juu chini ambao hawakubaliani na wao wakubaliane nao, na sio kuonyesha mashindano ya Sisi na Wao.
 
Yaani sijawahi kuona watu ambao hawana Busara kama hii Awamu.Hivi anadhani hapo kazi yake ni mipasho? Hao anaongea nao ni walipa kodi kwahio hata kama hawafurahii matumizi ya Kodi zao, ni vema wakaeleshwa / wakabembelezwa na sio Kubezwa.
Wanaongea hivyo kwa sababu cha kuwafanya hakuna, sisi ni kama vijidudu flani tu mbele yao wanaweza kutufanya chochote kile popote pale.

Tutalia lia hapa mwisho wa siku imeisha hio.
 
Msemaji mkuu wa serikali yuko mubashara TBC akielezea mafanikio ya awamu ya 5.
Mkuu mimi ni kada, ninyi mnanitia wasiwasi.

Morani ukiua simba kuendelea kumpiga virungu ilhali amekufa inatia mashaka juu ya umorani wako.

Chadema tumesha msuuza uchaguzi mwaka jana sasa ni vipi tena mwajipa kiki kupitia wao.

Hiyo ni dalili ya kutojiamini ushindi wako.
 
Hahaahaaa!

Hukukosea yule msanii aliyeimba:

"Huo ni ushamba!"

Au nasema uongo ndugu zangu?
Lakini leo ni siku ya wanawake duniani. So serikali imeamua kuwaunga mkono kwakuitisha press na kusuta wananchi wake
 
Hakuna kitu kibaya duniani kama kuwa na dharau. Maana mtu mwenye dharau anaweza akasema bora binadamu wale nyasi ili ndege zinunuliwe.

Hivi kwa akili ya kawaida, jinsi huduma za jamii zilivyo duni msemaji wa serikali anaweza kujinasibu kuwa serikali imefanya vizuri? Kwamba inatumia tril mbili kwenye elimu hiyo kununua midege 8 cash ni sawa.

Hivi huyu Dk Abbas anaishi maisha halisi ya Watanzania?

Kwamba anafahamu migambo na watendaji wanavyosumbua watu kuchangisha michango ya ujenzi wa madarasa? Kwamba wanafunzi hawana madarasa ya kutosha?

Kama mnawekeza vya kutosha kwenye elimu, michango ya nini?

Hizo ndege ambazo mnajisifia kuzinunua zinamsaidia mwananchi wa kawaida?

Ndege mlizonunua zinaleta faida kiuchumi? ATCL inabeba abilia mil 60 kati ya watu mil 60 hii ni faida?

Je, msingenunua ndege mbili na bil 500 zikatumika kwenye elimu na maji leo hii mgesaidia wananchi wangapi wa kawaida?
 
Msemaji wa serikali amesha tolea majibu kuwa, mwezi huu wa march mtalipwa malimbikizo yenu ya mshahara, na pia kafafanua vizuri tu kuwa kwa mujibu wa miongozo haitakiwi kabisa taasisi yoyote ya serikali au wizara kutengeneza au kulimbikiza madeni ya watumishi wake, kwa maana hakuna lolote litakalo fanyika bila fedha kutengwa.
.nakusihi kuwa na amani malipo yenu ya malimbikizo yanalipwa mwezi huu.

Hamna uwezo huo.
 
Kuna aliyoyasahau kwenye taarifa yake. Angeyamalizia tu. Nakazia kwa kumwekea hapa kama itampendeza:

".... chanjo za Corona nazo japo zipo na zinapatikana bure wala hatuzihitaji. Sisi K kizezeta zezeta, tumeamua kuwa wa kufa na wajifie kibudu tu. Wa kuishi nao hali kadhalika..."

IMG_20210218_173848_589.jpg


Au nasema uongo ndugu zangu.
 
Back
Top Bottom