Dj Majizo, Muasisi wa muziki wa Mchiriku, Mnanda, Singeli redioni!

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,840
43,292
uploadfromtaptalk1464938050421.png
uploadfromtaptalk1464938059098.png
uploadfromtaptalk1464938067764.png



Wasalaam wana jamvi!

Ni ukweli usio pingika kuna muziki fulani uliokuwa umezoeleka ndio unatakiwa kupigwa radioni na hii ilikuwa ni uniform za Radio zote kana kwamba ilikuwa ni sheria ambayo imewekwa!

ilikuwa ni vigumu na hakuna uthubutu wa miziki ya mnanda ,visingeli na mchiriku kusikia ukipigwa radioni na sio kwamba hauna mashabiki bali una mashabiki wengi sana sema radio muda mwingine hulazimisha walaji kula hata wasicho kitaka!

Dj Majizzo baada ya kuanzisha kutuo cha E-FM imekuwa kama mkombozi wa miziki yetu ya asili na wamekuwa wakiupa muda wa kutosha kuupromote kiasi kwamba hata walio kuwa hawajui uzuri wake sasa wanaelewa!

Mimi sikuwa mshabiki wa miziki wa namna hii lakini sasa nimekuwa kama teja maana kwakweli nyimbo hizi kuna zenye jumbe nzuri sana kiasi kwamba ukisikiliza una hamasika hakika!

Kupitia DJ majizzo (E-FM) leo hii sasa nyimbo za mnanda,mchiriku na singeli zimeanza kusikika kwenye radio nyingine na wasanii hao wanapata showa kitu ambacho hakikutegemewa!

Leo hii ukisikiliza East africa radio utasikia wakipiga nyimbo hizi na hata Clouds na kwenye matamasha tunaona wasanii wa minanda,mchiriku na visingeli wanapewa show tofauti za zamani wale wa bongo fleva ndio walikuwa wanakula hela peke yao!

Ni wazi kabisa Wasanii wa minanda ,mchiriku na visingeli wanapaswa kumshukuru Majizzo kwani amechangia sana kwenye mafanikio yao na mapinduzi yao!

Mimi nimshukuru tuu Majizzo kwa kuwasaidia vijana hawa na kuupa thamani mziki wao!

Karibuni Wana jamvi!
 
Kwa wapenzi wa lugha ya Kiswahili, kama nilivyo mimi wenu mtiifu, hizo aina za muziki ni njia nzuri sana za kujifunzia hii lugha yetu.

Ndiyo maana mimi, tena kwa fahari kubwa sana, huwa najivunia upenzi wangu wa aina hiyo ya muziki zikiwemo Taarab asilia, Taarab ya kileo, pamoja na chakacha.

Nimejifunza mengi mno yahusuyo lugha ya Kiswahili na lahaja zake kupitia hizo aina za muziki.
 
hiyo miziki ya mnanda,singeli ndio ya aina gani?
mwenye video ebu atupie sisi watu wa mkoani tujue........
 
"Nasikia hainaga ushemeji tunakulaaa,nasikia hainaga ushemeji tunakulaga
Majita zamu ya nani leo,zamu ya Man Fongo
Zamu yako itakuja kesho,usijali baharia wangu"
Mwisho wa kunukuu...
Huyu man Fongo ni njaa nyingine baada ya Msaga sumu.
YNWA
 
Kwa wapenzi wa lugha ya Kiswahili, kama nilivyo mimi wenu mtiifu, hizo aina za muziki ni njia nzuri sana za kujifunzia hii lugha yetu.

Ndiyo maana mimi, tena kwa fahari kubwa sana, huwa najivunia upenzi wangu wa aina hiyo ya muziki zikiwemo Taarab asilia, Taarab ya kileo, pamoja na chakacha.

Nimejifunza mengi mno yahusuyo lugha ya Kiswahili na lahaja zake kupitia hizo aina za muziki.
Mimi tatizo huwa sijui majina ya nyimbo lakini nimekuwa mshabiki mkubwa sana na huu ndio mziki wa kitanzania halisi!
 
Clouds fm nao nawaona wanapiga kwa kudeep siku moja moja! Mwenye collection ya nyimbo za mdananda aziweke hapa
Naona wana wapa hadi show wakina Man fongo,Msaga sumu..
 
nakukubali sana kaka majizzo kwa ubunifu wako na uchakarikaji...kw amuda mchache niliobahatika kufahamiana na wewe umeniinspire sana tatizo lako ni moja tu ukishapata unachokitaka unampotezea kama humfahamu vile!!!
 
Mashabiki wengi wa singeli ni wahuni wa mtaani wavuta bangi na wabwia unga.
Majizzo naona kaamua kuwapa shavu "wateja wake" as per mange's dot dot.....
 
Back
Top Bottom