DJ FETTY: Somo Kwa Wasanii Wa ANTI~VIRUS

YEYE

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
437
72
Kama msanii unafanya kazi nzuri,basi itapendwa na itanunuliwa...hata kama clouds wasipoicheza nyimbo yako kama ni nzuri si itachezwa
tu kwingine?! Kama msanii ni
mahiri,mweledi wa taaluma/sanaa yake basi atajua jinsi ya kumanage sanaa yake kibiashara
bila kusumbuliwa au kukwazwa na
mtu au kitu chochote iwe clouds
n.k. Naangalia wasanii wote
waliounda kundi zima la Anti- virus...nikitathmini undani
kupanda na kushuka (rise & fall)
kwao kitaaluma/sanaa sio kwamba
wa Clouds iliwapokonya kipaji/
weledi wao au iliwanyang'anya
mafao yao ila ni wao wenyewe walichezea kima chao cha mwanzo
na kushindwa kuendelea pia wengi
walipoteza dira ya sanaa bora na
management ya sanaa hiyo
kibiashara. Ieleweke Clouds ni
radio ya biashara ila kwa mapenzi ya wamiliki wake katika
sanaa na burudani, ndio media ya
kwanza kuwapa platform wasanii
wengi nchini na bado inaendelea
kufanya hivyo, ila haitakubali
kubeba wasanii ambao hawako sokoni tena- kwa maana ya
'fallen heroes' kutokana na
kupumzika sanaa, kubadili
taaluma, kushindwa kuendeleza
kipaji/weledi wao katika sanaa
zao n.k. Ukweli wanaujua, ila wanaamua kupumbaza jamii kwa
kupandikiza chuki dhidi ya
chombo kimoja- chuki ambazo ni
binafsi zaidi kuliko kiweledi.
Ila huwa tunajua muda(time) ni
tiba ya kila gonjwa... hili pia litatibika na tutajua chanzo cha
ugonjwa ni nini. Kwa sababu
mwisho wa siku swala ni
biashara, iwe kwa msanii,
promoter, manager au chombo cha
habari...
Source: DJ Fetty blog

MY TAKE:~
DHUMUNI la ANTIVIRUS sio kutaka kutafuta PROMO/AIRTIME kwenye RADIO na TV, ila ni kutetea HAKI za WASANII wanaonyonywa na kukosa SAUTI ya KUSEMEA labda kwa UOGA au sababu wanazozijua wao..
 
ameamua 'u****ya wake wa uganda kuuhamishia Tanzania. Walikuwa wengi hapoalipo naye bila shaka akipata akili atajua, utot bado unamsumbua huyo demu!
 
MY TAKE:~
DHUMUNI la ANTIVIRUS sio kutaka kutafuta PROMO/AIRTIME kwenye RADIO na TV, ila ni kutetea HAKI za WASANII wanaonyonywa na kukosa SAUTI ya KUSEMEA labda kwa UOGA au sababu wanazozijua wao..

Umemaliza! Huo utetezi wao hatutaki, wakafie mbele!
 
hatupiganii kupewa airtime clouds hapana. Tunachotaka ni mafao. wasanii walipwe kutokana na kazi walio fanya sio mtu unamzungusha tanzania nzima halafu anaambulia nguo za show na nyimbo zako kupigwa kwenye radio zao halafu wanaanza kusema fulani kafulia. Jenga picha. cd ya kibongo inauzwa 3000-5000 lakini msanii anaambulia tsh 200(mia mbili) kwa kila cd. Hela ilobaki anakula Rughe eti ni promota, mala sijui yupo kwenye lebo fulani. watu wanakosa hela ya kuingilia studio sio kwamba wanakaa kimya. Mia
 
Mapenzi ya wamiliki wake katika sanaa? Huyu dada naye vipi au naye ndo vile na wamiliki? Sio mapenzi ya wamiliki kwa muziki bali ni biashara tupu na kunyonya madogo wasiojua kitu. Kuna mrejesho wa haraka wa faida katika mapenzi hayo kwa mziki na ndo maana wananyonya watu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom