Diwani wa kinyerezi afisadi eneo la shule kwa ujenzi wa night club | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diwani wa kinyerezi afisadi eneo la shule kwa ujenzi wa night club

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mak89, Sep 28, 2012.

 1. mak89

  mak89 JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2012
  Joined: Sep 21, 2012
  Messages: 974
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 80
  Hapa kinyerezi kuna night club inajengwa, kujengwa kwake siyo tatizo ila eneo linapo jengwa ndiyo tatizo. Kwasababu gani nasema linapo jengwa ndo tatizo? Hili eneo ni mali ya shule ya msingi na pia hii night club ipo karibu na shule na ndipo ilipo njia inayo tumiwa na wanafunzi wengi wanao kaa mitaa ya zimbili. Na inasemekana wamiliki ni ridhiwani kikwete na rafiki yake anaitwa Ben. Diwani wa kata ya kinyerezi alifuatilia ila ghafla akaachana nalo kuulizia nikaambia diwani pamoja wajumbe wa kamati ya shule akiwemo mwalimu mkuu (anaitwa Omari) walipewa rushwa kwa wajumbe wengine sijui ila diwani alipewa milioni 7 akaenda kutengenezea madawati 100 tu, mwalimu mkuu akavuta Noah.

  Kamati ya shule ilishiriki katika kuuza eneo la shule ambamo kuna nyumba ya mwalimu anaishi humo (mwalimu mrema) na kiwanja cha michezo wakaenda kujenga nyumba nyingine upande wa pili wa shule. Je kisheria na maadili night club inaruhusiwa kujengwa karibu na shule na tena ndo njia inayotumiwa na wanafunzi kupita kwenda shule?

  Source: mmoja wa wajumbe aliyejiondoa kutokana na mambo yanayo fanywa na kamati ya shule kushirikiana na mwalimu mkuu.
   
 2. by default

  by default JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2012
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu haya mambo kwa jimbo la segeraa yameshamiri mimwenyew jirani na ninapoish open space nying zimeuzwa au kubadiliswa milk ya ccm .
   
 3. mak89

  mak89 JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2012
  Joined: Sep 21, 2012
  Messages: 974
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 80
  Hapo sijagusa kwenye open space huko ndo mbaya zaidi, yule diwani aliyetangulia aliuza mpaka eneo la makaburi, bila kilele za watu wachache eneo la shule ya sekondari ya kinyerezi lilikuwa limeisha uzwa
   
Loading...