Diwani wa kata ya Usa-River akacha msibani Magadirisho! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diwani wa kata ya Usa-River akacha msibani Magadirisho!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Emashilla, Sep 26, 2012.

 1. Emashilla

  Emashilla Senior Member

  #1
  Sep 26, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Poleni wafiwa wote, watu wa Majengo, Mbuguni, Magadirisho, na maeneo yote kwa vifo vya jamaa zetu katika ajali

  Siku ya Jumamosi, 22 Septemba 2012 kulitokea ajali mbaya katika barabara ya Magadirisho eneo la Ayonite Safari Lodge & Pub, majira ya saa moja jioni. Ajali ilihusisha gari dogo na pikipiki au boda boda. Dereva wa bodaboda alifariki papo hapo na abiria wake maarufu kwa jina la Mama Mzungu alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali. Dereva wa gari hakupata madhara yoyote pamoja na wenzake aliokuwa nao ingawa gari lilipinduka na kuharibika. Chanzo cha ajali imeelezwa ni mwendo kasi na ulevi wa Derava Shukurani, mkazi wa Magadirisho na jirani wa marehemu Mama Mzungu.
  Jana, Jumatatu 24 Septemba kulifanyika maziko ya Mama Mzungu nyumbani kwake karibu na msikiti wa Masjid Zahru Magadirisho. Watu walikuwa wengi sana na wimgu la huzuni lilitanda msibani. Lakini katika hali ya kushangaza Mwenyeikti wa Kitongoji cha Magadirisho (CCM) alikaribishwa kutoa salamu za rambirambi za serikali ya kitongoji cha Magadirisho; alipomaliza, alimakribisha diwani kwa maneno ya kumpamba,
  akisema; "Hapa katika msiba huu mkubwa tuna mheshimiwa diwani Bwana Zuberi wa kata ya Usa-River, naye ni mkuu wangu ni vizuri nimpatie heshima kama kiongozi wa wananchi aweze kutoa salamu za kata yetu"
  Diwani hakujitokeza ingawa mwenyekiti alisisitiza kwamba alikuwa naye na yupo hapa anampisha ili asalimie waombolezaji. Wananchi walimtafuta huku na huku kwa macho lakini hapakuwepo dalili za Diwani kujitokeza. Juhudi za mwenyekiti ziliishia hewani kwani diwani aliyeyuka. Ndipo Mwenyekiti, akasema; "Sijui imekuaje maana tulikuwa naye sasa hivi, basi!"


   
 2. Thegreatcardina

  Thegreatcardina JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2012
  Joined: Mar 29, 2009
  Messages: 396
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Duh hii nayo kali.
   
Loading...