Diwani wa kata ya Makiba Meru, Emmanuel Pendaeli avuliwa uwanachama wa CHADEMA

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Taarifa rasmi ni kuwa Bwana Emanuel Pendael Mollel Aliyekuwa Diwani wa kata ya Makiba Halmashauri ya Meru Avuliwa uachama rasmi.

Hii ni baada ya Mwendo wake kutiliwa mashaka kwa kukosa uaminifu na kusaliti Maagizo ya chama pamoja na madiwani wenzake alionywa Mara kadhaa na hakuonekana kubadilika baada ya chama kujiridhisha aliambiwa aandike barua ya kukiri makosa yake hata hivyo hakutekeleza maelekezo ya Mdhamini wake Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.

MAAMUZI

Baada ya kukahidi maelekezo aliyopewa ya kuandika barua Juu ya tuhuma zake
*1.Kukiuka makubaliano ya Madiwani wa Chadema kutokupokea posho yeye alisaini posho kwa siri na alipobainika alikataa ndipo Waandishi wa vikao walitoa ushahidi hata hivyo alikataa na aliposikia TAKUKURU Wataingilia swala hilo alikubali kosa*

*2.Tangu achaguliwe kuwa Diwani haonekani kwenye Kata yake wala hana makazi huko hivyo hakuweza kuwajibika kwa wananchi wake kwa mda wake wa Udiwani .Kimsingi makosa yake makuu ni matatu 1.KUKOSA UAMINIFU 2.KUSHINDWA KUWALETEA WANANCHI MAENDELEO KWA MWAKA WA PILI SASA*

*3.Kukataa kufanya kazi na na kumdharau mwenyekiti wa Kijiji cha Patanumbe kitendo kilichosababisha Mwenyekiti kushindwa kuendelea kuhudumia ofisi kwa ufanisi na kumtengenezea Zengwe kuwa hataki kuongoza wananchi hivyo kusababisha Mwenyekiti kukosa sifa ya kuwa mwekiti wa Kijiji na uchaguzi kurudiwa*
Chama kiliazimia kumvua uanachama rasmi tar *24/05/2017*

Taharifa ambazo siyo rasmi zinadai kuwa mkuu wa wilaya ya Arumeru Amemwahidi kumpa kazi ya Afisa mtendaji kata ya Bangata. Hivyo bwana Emanuel Mollel kwa sasa anajiandaa kuwa Afisa mtendaji wa kata ya Bangata Arumeru magharibi
*Kutoka kuwa Mh Diwani mpaka kuwa Katibu wa Diwani (WDC)*
*Kila la kheri katika majukumu yako ukiwa Chini ya bosi wako Mpya Diwani wa kata hyo utakayo pangiwa kazi*
 
Kuna baadhi ya wanachama wa CCm tuliwapokea wakati Mhe. Lowassa alipokuja CHADEMA wakabaki na chembechembe za tabia za kule. Wanatupa shida sana. Ila ni funzo kubwa sana tumepata.
 
Si ameandika barua ya kuomba kujiuzulu? Ki utawala aneshuka lkn ki payroll amepanda. Ametoka kwenye hakuna, sasa ana tgts a hadi tgts h
 
Kumbe kiongozi aliyechaguliwa na wananchi anaweza kuvuliwa madaraka na chama?
 
Hawakosagi sababu hawa jamaa ila walio na akili timam wanawaelewa
 
Mmeanza Kuruka Na Kukanyagana Wenyewe!! Kama Mmeweza Kuwaamini Makapi Ya Ccm Lowassa, Sumaye, Mwiru Et Al, Mnashindwa Nini Kumvumilia Diwani Wenu!
Hujui lolote nyamaza. CDM ukileta ujinga wa dharau unaondoka.
Magu anatekeleza sera za CDM.
Ma CCM hawana tabia hizo wanalindana tuu!!
 
Taarifa rasmi ni kuwa Bwana Emanuel Pendael Mollel Aliyekuwa Diwani wa kata ya Makiba Halmashauri ya Meru Avuliwa uachama rasmi.

Hii ni baada ya Mwendo wake kutiliwa mashaka kwa kukosa uaminifu na kusaliti Maagizo ya chama pamoja na madiwani wenzake alionywa Mara kadhaa na hakuonekana kubadilika baada ya chama kujiridhisha aliambiwa aandike barua ya kukiri makosa yake hata hivyo hakutekeleza maelekezo ya Mdhamini wake Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.

MAAMUZI

Baada ya kukahidi maelekezo aliyopewa ya kuandika barua Juu ya tuhuma zake
*1.Kukiuka makubaliano ya Madiwani wa Chadema kutokupokea posho yeye alisaini posho kwa siri na alipobainika alikataa ndipo Waandishi wa vikao walitoa ushahidi hata hivyo alikataa na aliposikia TAKUKURU Wataingilia swala hilo alikubali kosa*

*2.Tangu achaguliwe kuwa Diwani haonekani kwenye Kata yake wala hana makazi huko hivyo hakuweza kuwajibika kwa wananchi wake kwa mda wake wa Udiwani .Kimsingi makosa yake makuu ni matatu 1.KUKOSA UAMINIFU 2.KUSHINDWA KUWALETEA WANANCHI MAENDELEO KWA MWAKA WA PILI SASA*

*3.Kukataa kufanya kazi na na kumdharau mwenyekiti wa Kijiji cha Patanumbe kitendo kilichosababisha Mwenyekiti kushindwa kuendelea kuhudumia ofisi kwa ufanisi na kumtengenezea Zengwe kuwa hataki kuongoza wananchi hivyo kusababisha Mwenyekiti kukosa sifa ya kuwa mwekiti wa Kijiji na uchaguzi kurudiwa*
Chama kiliazimia kumvua uanachama rasmi tar *24/05/2017*

Taharifa ambazo siyo rasmi zinadai kuwa mkuu wa wilaya ya Arumeru Amemwahidi kumpa kazi ya Afisa mtendaji kata ya Bangata. Hivyo bwana Emanuel Mollel kwa sasa anajiandaa kuwa Afisa mtendaji wa kata ya Bangata Arumeru magharibi
*Kutoka kuwa Mh Diwani mpaka kuwa Katibu wa Diwani (WDC)*
*Kila la kheri katika majukumu yako ukiwa Chini ya bosi wako Mpya Diwani wa kata hyo utakayo pangiwa kazi*

Hii kamati iliyomuondoa ndio ina majungu.

1-Ina maana Chadema bado wanang'ang'ania posho badala ya maendeleo?yaani baada ya mkurugenzi kuwapunguzia posho hadi leo wamesusa???

2-Eti leo hii Chadema ndio inagundua mtu waliyempitisha kugombea udiwani sio mkazi wa eneo husika...shame on you!

3-Mwenye wajibu wa kumsimamia mwenyekiti ni nani kisiasa kama sio diwani.Wananchi wangekubali vipi kumuondoa mwenyekiti kama kweli alifanyiwa majungu?

Swali la kizushi...

Hivi huyo diwani ni kambi ya Nassari au Mwenyekiti wa halmashauri??maana huo mgogoro hautakaa uishe.
 
Kuna baadhi ya wanachama wa CCm tuliwapokea wakati Mhe. Lowassa alipokuja CHADEMA wakabaki na chembechembe za tabia za kule. Wanatupa shida sana. Ila ni funzo kubwa sana tumepata.
Hivi huyu naye ni kati ya wale waliohamia cdm dakika za majeruhi!!? Kwa kweli naipenda chadema ila zoa zoa nayo sio kabisa. Hata ujio wa Lowasa ulinipa wakati mgumu sana kuukubali akilini mwangu. Lakini nilipo kumbuka ule usemi wa Bush baada ya Sept. 11, "yeyote asiye upande wetu basi naye ni adui yetu kama Osama" ndipo nikasema ok, karibu kwa akili yangu. Lakini in future tuwe makini cdm
 
Inamaana mwaka huu ndio Chadema wamegundua kuwa huyo Diwani hana nyumba kwenye kata husika? Sasa walimpitisha vip kuwa mgombea wao?
Safari bado ndefu
 
Wapigania chama mnawafukuza kisa hawana pesa kama Lowassa?

Mbona Tundu Lissu hakai Singida?
 
Hivi huyu naye ni kati ya wale waliohamia cdm dakika za majeruhi!!? Kwa kweli naipenda chadema ila zoa zoa nayo sio kabisa. Hata ujio wa Lowasa ulinipa wakati mgumu sana kuukubali akilini mwangu. Lakini nilipo kumbuka ule usemi wa Bush baada ya Sept. 11, "yeyote asiye upande wetu basi naye ni adui yetu kama Osama" ndipo nikasema ok, karibu kwa akili yangu. Lakini in future tuwe makini cdm
Usiwe na hofu
 
Hujui lolote nyamaza. CDM ukileta ujinga wa dharau unaondoka.
Magu anatekeleza sera za CDM.
Ma CCM hawana tabia hizo wanalindana tuu!!
maendeleo hayana chama, sisi makapuku tunachotaka ni maendeleo tu basi.....mbona kama ni case study CCM ndo inaongoza kwa kupiga chini wanachama wake,,,, rejea Nape, Lowassa, Sumaye, Sofia simba etc.. ila mimi naamini kina Lowassa na sumaye ni mafisadi
 
Back
Top Bottom