Diwani wa Kata ya Kimandolu, Arusha ni mzigo

calculator

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
279
137
Wana wa Kimandolu na JF kwa ujumla, Salaam.

Ama baada ya salaam naomba nijikite moja kwa moja kwa hoja yangu.

Diwani wa Kata ya Kimandolu (CHADEMA) Bw. Ngowi amekuwa kero na hakika tunajutia maamuzi yetu kumchagua mwaka juzi. Ana mihemko na anadaiwa madeni kila kona ya Kata. Amefikia mahali anamkashifu hadharani Mwenyekiti wetu wa chama wa Kata.

Amejijengea maadui wengi na wananchi wanamuona kama ni mjasiriamali wa siasa aliyekuja kwa siasa kwa maslahi yake binafsi.

Sisi wana wa Kimandolu tunakupa ujumbe huu kuwa safari yako ya kisiasa inaishia October hii. Rudi tu ukachunge kondoo wa bwana pale mlimani kwako.

Nawasilisha
 
Wanachadema wazuri wako wengune washaurin wachukue fomu na mpitishen moja kwa taratibu za kawaida za chama!
 
Tutasikia mengi sana wakati huu wa uchaguzi! Hata hivyo sikubaliani na wewe hasa kwakuwa ulekuja na personal attack! Kama unataka kugombea ungeplay smatter than this!
 
calculator

Wewe ni kada wa CCM, kwa kazi nzuri iliyotukuka ya Mch. Ngowi lazima ujutie kwanini upo CCM, heri ungekuwa CHADEMA ili usiumie maini...... Tuliwapiga kwenye uchaguzi mpaka Mwigulu akakosa njia, mara ya mwisho kabla matokeo hayajatangazwa tukasikia Mwigulu ameonekana KIA. Kata ya Kimandolu hata kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa hakuna hata mtaa moja ulioenda CCM, Mitaa yote CHADEMA walichukua, kazi nzuri ya Mch. Ngowi.

Post zinazodhihirisha wewe ni gamba hizi hapa na umemfuatilia Mch. Ngowi tokea 2013 kabla ya uchaguzi wa kata nne:

Habari zilizothibitishwa na wafuatiliaji wa duru za siasa jijini Arusha zimebaini kuwa Ndg. Rayson E. Ngowi ambaye ni mgombea udiwan kata ya kimandolu, Arusha, kwa tiketi ya CHADEMA hayupo kwai daftar la wapiga kura kwa kata hyo. Ngowi mwenye kitambulisho namba 13214796 alijiandikisha mnamo tar 10 machi 2005, wilayani Rombo, mkoan Kilimanjaro.
Amepigiwa simu mara kadhaa kuthibitisha madai hayo ila hakutoa ushirikiano na amekuwa akitoa jibu moja tu "haikuhusu". Kazi kwenu wakazi wa kimandolu
Mgombea udiwan wa CHADEMA kata ya Kimandolu

Hii hapa ya 2012:
Chadema wameshaanza kuona dalili za kupoteza kiti cha ubunge hapa Arusha. Vilevile viti sita vya udiwani vilivyopo wazi vyote vinarudi CCM na hivi ninavyowaletea huu uzi, viongozi wao wanasigana tu wasijue wanajipangaje. Kwisha kazi yenu.
CHADEMA Arusha wameanza kutoa mapovu

Post hizo hapo juu ni dhahiri upo Lumumba, na kwamba huna la kujutia kwakuwa kura yako hukumpigia Ngowi. Kengenyau wewe!
 
Last edited by a moderator:
Tutasikia mengi sana wakati huu wa uchaguzi! Hata hivyo sikubaliani na wewe hasa kwakuwa ulekuja na personal attack! Kama unataka kugombea ungeplay smatter than this!

Mkuu hilo ni gamba mpumbavu
 
Mungi na DALLAI LAMA...
Naheshimu mawazo yenu. Mim sio mtia nia na wala sio gamba pia. ni mkazi wa kata hii na namjua vzr huyu diwani. msijitoe ufahamu.. tembeeni kuanzia kijenge chini mpk juu.. ulizeni wapiga kura khs huyu mtu.. ni aibu. anawashambulia watia nia wenzake kama vile yeye ana hati miliki ya udiwani. Hatoshi.. hatutampa kura.. tumeazimia.. tutawapima kwa vigezo mujarabu.
 
Last edited by a moderator:
so kweli hata kidogo,ni moja ya madiwani wazuri katika jiji la Arusha.Wewe umemshambulia kwa maslahi yako tu na atashinda kwa kishindo.Pia kama una ugomvi nae si bora umtafute mkaongee ila sio vyema kumwanika hadharani,jifikirie ni wewe umewekwa hapa utajisikiaje?
 
mie ni mtumishi wa Halmashauri ya jiji namfahamu sana ngowi hivyo ni mtu mwema na hili ni kwa sababu ya uchungaji wake.utake usitake ngowi ni mambo yote.
 
Huyu Ngowi ametuletea Barabara ya moramu kwa Mara ya kwanza;tulizuoea kuona Hedi akitujazia udongo wa mfinyanzi na kushindilia ila mvua ikinyesha barabara inakuwa utelezi. Ngowi kwa muda mfupi tumeona juhudi zake. Mtoa mada unaumwa gonjwa baya sisi bado
tunampa nafasi nyingine na kama vipi hama kata.
 
Mungi na DALLAI LAMA...
Naheshimu mawazo yenu. Mim sio mtia nia na wala sio gamba pia. ni mkazi wa kata hii na namjua vzr huyu diwani. msijitoe ufahamu.. tembeeni kuanzia kijenge chini mpk juu.. ulizeni wapiga kura khs huyu mtu.. ni aibu. anawashambulia watia nia wenzake kama vile yeye ana hati miliki ya udiwani. Hatoshi.. hatutampa kura.. tumeazimia.. tutawapima kwa vigezo mujarabu.

Taja majina ya watu angalau 3 wanaomdai Ngowi.Je huyu na Hedi yupi bora?
 
Last edited by a moderator:
Wewe ni kada wa CCM, kwa kazi nzuri iliyotukuka ya Mch. Ngowi lazima ujutie kwanini upo CCM, heri ungekuwa CHADEMA ili usiumie maini...... Tuliwapiga kwenye uchaguzi mpaka Mwigulu akakosa njia, mara ya mwisho kabla matokeo hayajatangazwa tukasikia Mwigulu ameonekana KIA. Kata ya Kimandolu hata kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa hakuna hata mtaa moja ulioenda CCM, Mitaa yote CHADEMA walichukua, kazi nzuri ya Mch. Ngowi.

Post zinazodhihirisha wewe ni gamba hizi hapa na umemfuatilia Mch. Ngowi tokea 2013 kabla ya uchaguzi wa kata nne:

Mgombea udiwan wa CHADEMA kata ya Kimandolu

Hii hapa ya 2012:

CHADEMA Arusha wameanza kutoa mapovu

Post hizo hapo juu ni dhahiri upo Lumumba, na kwamba huna la kujutia kwakuwa kura yako hukumpigia Ngowi. Kengenyau wewe!

You nail at the nail head Kamanda! sina la kuongeza!!!
 
Mkuu Mungi umemfuma huyu gamba namfaham vizuri ni mkazi wa kijenge juu na anabifu na CHADEMA muda mrefu sana lkn wamekuwa wakishindwa
 
Inawezekana mkuu. Mimi ni mkazi wa kata ya Kimandolu.. mpk leo nimeskia kuna watia nia wanne ambao ni Ngowi, Jose Shio, Amani Ritoine na Erick Kitunga. Wafanye siasa safi wasichafuane tafadhali

So wewe unamkampenia nani hapo?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom