Diwani wa Chadema asalimisha AK47 kwa RC Mara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diwani wa Chadema asalimisha AK47 kwa RC Mara

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Pepombili, Apr 16, 2011.

 1. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  DIWANI wa Serengeti, Chacha Samwel Gibewa (Chadema) amesalimisha kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Enos Mfuru bunduki aina ya AK 47 ambayo amekuwa akimiliki kinyume cha Sheria.

  Kiongozi huyo wa wananchi aliwasilisha bunduki hiyo Jumanne jioni baada ya madiwani wenzake kumtuhumu kwa kuchochea ugomvi wa kikabila na kupinga kusajili wa Shule ya Sekondari Machochwe kuwa Shule ya Kidato cha Tano na Sita.

  Kabla kukubali kukabidhi bunduki hiyo wakati wa kikao cha bajeti cha baraza la madiwani, Mkuu wa Mkoa alimuonya kuwa atakabiliwa na hatua kali dhidi yake ambazo hatazisahau maishani. “Kuwa makini.

  Natamani ungefahamu mimi ni mtu wa namna gani. Leo lazima unipe bunduki ama sivyo utakaa jela mpaka utajuta,” Kanali Mfuru alimuonya Gibewa ambaye ni Diwani wa Kata ya Machochwe.

  Diwani huyo alilazimishwa kuomba msamaha kufuatia tuhuma zilizotolewa na wazungumzaji kadhaa waliosimama kuzungumza katika mkutano huo na kumtaka abadilishe tabia yake.

  “Napenda kuomba msamaha na kama kuna dalili za ukabila ndani ya moyo wangu nitaacha na kuhusu bunduki nitaitoa kama ninayo,” alisema Gibewa ambaye alipigiwa makofi na wajumbe wa baraza.

  Mfuru alimshukuru diwani huyo kwa uamuzi wake lakini aliendelea kumshinikiza kutoa bunduki mara moja. Diwani Gibewa alikubaliana na amri hiyo na kukubali kuongozana na Mkuu wa Mkoa bpamoja na Mkuu wa Wilaya Edward Lenga na kwenda kijijini Machachowe ambapo ni kilometa 20 kutoka sehemu ulipokuwa ukifanyika mkutano.

  Gibewa alimpeleka mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya hadi shambani kwake ambapo alitoa bunduki kutoka kwenye shimo na kumkabidhi Kanali Mfuru.

  “Lilikuwa ni shimo refu na alisalimisha na risasi ambazo hazijatumiwa,” alisema Lenga.
  HAPA NAZIDI KUOGOPA MMMM CHADEMA

  source:Habari leo
   
 2. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Anastahili kupongezwa kwa kukubali udhaifu na kuchukua hatua............ndvyo kiongozi anavyopaswa kuwa..

  Pia swala la kuogopa kwa kukutwa na silaha unadhani ni huyo tu wa CDM ndiye anayo? Kama leo ikitokea wote ikawekwa wazi unadhani wa Chama Cha Magamba (CCM) ni wangapi watakuwa nazo kinyume na sheria? Au unadhani hawapo?
   
 3. h

  hoyce JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,119
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kwa mkoa wa mara hata hao wengine ambao hawajasalimisha wanazo bunduki kibao. Sishangai sana
   
 4. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  bunduki hazina chama...nahofia kila anyekamatwa nayo akiulizwa chama chake mbona ile chama nzee itaumbuka
   
 5. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Huyo kajivua gamba la ujambazi kivitendo. Lowasa na genge lake nao wangeiga mfano huo kwa kurudisha zile 152 m walizokuwa wanavuta kilasiku bila kufanya kazi kwa miaka miwili, vile vijisenti walivyojikatia kwenye malipo ya rada, ndege ya Nkapa nk
   
 6. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kuwa CCM,CDM au CUF kuna uhusiano gani na kumiliki silaha kinyume cha sheria? kama ni hivyo basi masheik,maaskofu na wachungaji wote wataiona pepo.
   
 7. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  RC na DC wasiishie kupokea silaha tu. Sheria ichukue mkondo wake ifahamike hiyo silaha alikuwa anaifanyia shughuli gani kama siyo kukodisha kwa majambazi.
   
 8. M

  Makaramu JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 277
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hapa kaka umesema kweli,..,,,,,,.wakisema kila mtu asalimishe ile chama itaumbuka aswaaaaaa,..,,..,,sababu wale jamaa wanamiliki hadi magrunet,...,,,,.wapo baadhi nawajua na wamekuwa wakidhamini majambazi polis ambao ni wafanyakazi wao.
   
 9. z

  zamlock JF-Expert Member

  #9
  Apr 16, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  hilo ni swala lingine jaman kama kweli alikuwa ana miliki silaha pasipo kufuata taratibu basi sheria ichukue mkondo wake tuache ushabiki wa siasa hapa kwenye makosa basi tukubali kuwa tumekosea
   
 10. Ellyson

  Ellyson JF-Expert Member

  #10
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 1,717
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Rostam naye anyang'anywe uraia kwa ufisadi.
   
 11. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #11
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ellyson usitoke nje ya mada, RA ni suala lingine. Hapa tunataka sheria ichukue mkondo wake tujue AK47 ilikuwa kwa kazi gani? Utawala bora unataka uwazi, ingekuwa amri yangu huyo mheshimiwa diwani angekuwa muda huu anahojiwa na RCO na OC CID
   
 12. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #12
  Apr 16, 2011
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Kwani waliorudisha pesa za EPA walichukuliwa hatua gani?
  Kwa kuwa ni CDM kweli watampa kibano.
   
 13. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #13
  Apr 16, 2011
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye bold jamani! Hivi mkuu wa mkoa anaruhusiwa kuhudhulia kikao cha bajeti cha baraza la madiwani? Yeye ni mjumbe kwa mtindo upi?
   
 14. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #14
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  RC ni mhimili wa kikao cha madiwani:A S 465: Hivyo kwa madaraka yake anaruhusiwa kuhudhuria vikao vya halmashauri
   
 15. m

  msaragambo Senior Member

  #15
  Apr 16, 2011
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Umesahau Edger Maokola Majogo alikamatwa nayo Airport sasa si bora aliyeisalimisha mwenyewe
   
 16. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #16
  Apr 16, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nilikuwa sijui. Hivi kumbe chadema ni majambazi. yaani mpaka viongozi. Hivi yule diwani wa chadema aliyekuwa rumande kwa tuhuma za mauaji alishatoka? Nasikia na lema naye ni member mzuri tu, du si utani.
   
 17. mwanaone

  mwanaone JF-Expert Member

  #17
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 635
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 180
  jamani hii jamiii forum sio tawi la chadema jami forum ni kwa ajili ya watanzania wenye uchungu wa nchi yao na wenye kutaka haki sawa kwa wote. sasa kama huyo diwani ni kweli kakamatwa na silaha tena AK 47 . mimi kama mwanajamii nahisi sheria ichukue mkono wake ili iwe fundisho kwa wengine ukizingatia yy ni kiongozi na vile vile chadema kama chadema ili kulinda heshima yake imlazimishe aachie ngazi mara moja kwa hii haileti picha nzuri kwa chama makini kama chadema.
   
 18. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #18
  Apr 16, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  ni kinyume cha sheria kumiliki binduki bila kibali bana!...polisi wafungue mashtaka kwa wote wawili.
   
 19. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #19
  Apr 21, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  bunduki ni ya chacha siyo ya chadema. Tofautisheni mtu na chama.
  Hii msiifananishe na ufisadi kwani hela za ufisadi zilitumika kuingiza chama na baadhi ya viongozi wake madarakani, ndiyo maana tunahusisha chama na mafisadi. Kama bunduki hiyo ingekutwa inatumika kuiingiza cdm madarakani, the tungeihusisha na cdm; vinginevyo itabaki ni ya chacha. Sheria ichukue mkondo wake.
   
Loading...