Diwani wa CHADEMA aliyefukuzwa Arusha ajuta

Mna uhakika gani kama hii habari siyo ya kutengeneza? Kama kweli amejuta mbona sijasikia tamko lolote kutoka kwa katibu mkuu?

Kweli magamba mnaishi kwa mazoea! Kwakuwa mmezoea kutengeneza habari, lazima uwe na mashaka!
Na kwakuwa mlizoea Makamba ndio msemaji wenu, hiyo nayo imekusumbua!
Pole sana!

Mna uhakika gani kama hii habari siyo ya kutengeneza? Kama kweli amejuta mbona sijasikia tamko lolote kutoka kwa katibu mkuu?

Katibu mkuu aongelee nin wakati muhusika hana chama? Au unamtindio wa ubongo wewe?
Tafakari!

Haya mambo ya kutishia kuja.... Wakati unaha.... Matokeo yake ni kuchafua ch.... Haya ss ulinywe

huyu msaliti ni kumwandama mpaka ajitundike. Hii itakuwa fundisho kwa wengine wenye uchu wa pesa na sio kuwatumikia wananchi....
NO SECOND CHANCE TO MAKE THE FIRST IMPRESSION.
Hata kama akirudishiwa huo udiwani hataaminiwa kama zamani alishaharibu huyo, aendelee kujuta milele yote

"Isamanya ila songuo!" Yaani, la kujua halitangulii. Ndio maana ningejua huwa ni nyingi sana.

habari ifuatayo unaweza kuisoma kwenye attachment niliyoweka humu ambayo ni cutting kutoka gazeti la dira la leo uk. 02

mmoja wa madiwani wa chadema wa jiji la arusha waliofukuzwa kwa kukaidi amri ya kamati kuu, charles mpanda (rasta) amekataa kushiriki vikao vya baraza la madiwani na kuchukua posho, licha ya waziri wa tawala za mikoa na serikali za mitaa, george mkuchika, kusisitiza kuwatambua na hivyo kumuumbua.

rasta alitoa msimamo huo baada ya kudai kuwa alijikuta akiingia katika mzozo na viongozi wake wa juu, baada ya kuponzwa na wenzake bila kujijua.

alisema kwa sasa ameamua kuachana na siasa na kushughulika zaidi na shughuli zake na kwamba hatoshiriki kwenye vikao vya baraza la madiwani.

mpanda alisema hawezi kuchukua posho kwani atakuwa hawatendei haki wananchi wakati hawatumikii.

aidha, diwani huo anajuta kujiingiza kwenye siasa kwani kabla ya hapo alikuwa na maisha mazuri na alikuwa akiheshimiwa na jamii tofauti na sasa ambapo jamii inamchukulia kama adui na msaliti asiyeaminika.

alisema, awali aliamini nafasi yake ya udiwani ingempatia uzoefu mkubwa ili baadaye ndoto yake ya kuwania katika jimbo mojawapo mkoani mwanza, lakini sasa amesitisha zoezi hilo baada ya kubaini siasa zinamletea madhara makubwa.

"kwa sasa sina mpando kabisa na siasa, kwanza zimeniharibia mambo yangu mengi sana na wala sitegemeu kushiriki hata vikao vya madiwani, wameniletea baru kushiriki kikao tarehe 8 mwezi huu, nimewaambia sitakuwepo," alisema mpanda.

hata hivyo kumekuwepo taarifa kwamba diwani huyo amekuwa akizomewa mara kwa mara anapopita karibu na mshabiki wa chama hicho na kudiriki hata kutaka kumpiga wakidai msaliti.

taarifa zimedai kwamba mpanda alivamiwa na kundi la vijana alipokuwa akipita eneo la makao mapya karibu na shina la ngome imara la chadema na kuanza kuzongwa na vijana huku baadhi yao wakimtemea kohozi la mate usoni.

"ni kweli nimekuwa katika wakati mgumu sana kila ninapopita mitaani, hasa sehemu walipo mashabiki wa chadema," alisema

katika hatua nyingine, katibu mkuu wa ccm mkoa wa arusha, mary chtanda amejikuta kwenye wakati mgumu, kufuatia kundi la vijana kuibuka mara kadhaa na kumzomea hadharani.

matukio hao yamekuwa yakiibuka mahakama kuu ya arusha, wakati umati wa watu wakitoka ama kuingia kufuatilia kesi ya kupinga matokeo ya ushindi wa mbunge wa arusha godbless lemma.

katika kesi hiyo iliyoanza kuunguruma hivi karibuni, umati mkubwa wa watu wamekuwa wakifika mahakamani hapo wakiwemo mashabiki wa ccm na chadema, hatua ambayo imempelekea chatanda kuzomewa wakidai kwamba amechangia ccm kukosa jimbo.

rastawachadema.jpg

ukiwa unakula ni rahaaa ila yakishageuka utajuta kuzaliwa.......ha ha ha ha ha pole sana rasta

Mna uhakika gani kama hii habari siyo ya kutengeneza? Kama kweli amejuta mbona sijasikia tamko lolote kutoka kwa katibu mkuu?

Si umkumbushe silva rweyemamu ajibu,au ulifikiri makamba kahamia cdm? Nna wasiwasi una utapiamlo wa ubongo

Back
Top Bottom