Diwani wa CHADEMA aliyefukuzwa Arusha ajuta

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,326
974
*************

Habari ifuatayo unaweza kuisoma kwenye attachment niliyoweka humu ambayo ni cutting kutoka gazeti la DIRA la leo uk. 02

*************

Mmoja wa madiwani wa CHADEMA wa Jiji la Arusha waliofukuzwa kwa kukaidi amri ya Kamati Kuu, Charles Mpanda (Rasta) amekataa kushiriki vikao vya Baraza la Madiwani na kuchukua posho, licha ya Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa, George Mkuchika, kusisitiza kuwatambua na hivyo kumuumbua.

Rasta alitoa msimamo huo baada ya kudai kuwa alijikuta akiingia katika mzozo na viongozi wake wa juu, baada ya kuponzwa na wenzake bila kujijua.


Alisema kwa sasa ameamua kuachana na siasa na kushughulika zaidi na shughuli zake na kwamba hatoshiriki kwenye vikao vya baraza la madiwani.


Mpanda alisema hawezi kuchukua posho kwani atakuwa hawatendei haki wananchi wakati hawatumikii.


Aidha, diwani huo anajuta kujiingiza kwenye siasa kwani kabla ya hapo alikuwa na maisha mazuri na alikuwa akiheshimiwa na jamii tofauti na sasa ambapo jamii inamchukulia kama adui na msaliti asiyeaminika.


Alisema, awali aliamini nafasi yake ya udiwani ingempatia uzoefu mkubwa ili baadaye ndoto yake ya kuwania katika jimbo mojawapo mkoani Mwanza, lakini sasa amesitisha zoezi hilo baada ya kubaini siasa zinamletea madhara makubwa.


"Kwa sasa sina mpando kabisa na siasa, kwanza zimeniharibia mambo yangu mengi sana na wala sitegemeu kushiriki hata vikao vya madiwani, wameniletea baru kushiriki kikao tarehe 8 mwezi huu, nimewaambia sitakuwepo," alisema Mpanda.


Hata hivyo kumekuwepo taarifa kwamba diwani huyo amekuwa akizomewa mara kwa mara anapopita karibu na mshabiki wa chama hicho na kudiriki hata kutaka kumpiga wakidai msaliti.


Taarifa zimedai kwamba Mpanda alivamiwa na kundi la vijana alipokuwa akipita eneo la Makao Mapya karibu na shina la Ngome Imara la CHADEMA na kuanza kuzongwa na vijana huku baadhi yao wakimtemea kohozi la mate usoni.


"Ni kweli nimekuwa katika wakati mgumu sana kila ninapopita mitaani, hasa sehemu walipo mashabiki wa CHADEMA," alisema

Katika hatua nyingine, katibu mkuu wa CCM mkoa wa Arusha, Mary Chtanda amejikuta kwenye wakati mgumu, kufuatia kundi la vijana kuibuka mara kadhaa na kumzomea hadharani.

Matukio hao yamekuwa yakiibuka Mahakama Kuu ya Arusha, wakati umati wa watu wakitoka ama kuingia kufuatilia kesi ya kupinga matokeo ya ushindi wa mbunge wa Arusha Godbless Lemma.


Katika kesi hiyo iliyoanza kuunguruma hivi karibuni, umati mkubwa wa watu wamekuwa wakifika mahakamani hapo wakiwemo mashabiki wa CCM na CHADEMA, hatua ambayo imempelekea Chatanda kuzomewa wakidai kwamba amechangia CCM kukosa jimbo.

*************

RastawaCHADEMA.jpg
 

Attachments

  • Rasta wa CHADEMA.jpg
    Rasta wa CHADEMA.jpg
    199.3 KB · Views: 88
Jun 14, 2011
58
18
waombe wana wa Arusha msamsamaha.binafsi nilikuamini sana lakini ulichokifanya sikuamini pia sikufurahia hata kidogo. nivizuri ukajuta then wengine wajifunze kutokana na usaliti wako
 

Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,990
4,502
Counting down walifikiri CCM ina urafiki wa kudumu watakutumia then wanakuacha wamuulize aliyemwagiwa tindikali.
 

Gwallo

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
3,088
3,459
Mh! Hiyo ni trela tu, hata movie bado, ulifikiri cdm ni shamba la bibi?
<br><br>


Siasa huwa chungu endapo upo pale kwa maslahi yako lakini ukitumikia jamii iliyokuamini kwa uaminifu na uadilifu utadumu katika siasa la sivyo unaweza kuwa mashuhuri dakika leo&; na kesho ukaporomoka mpaka huamini macho yako.

Charles binafsi sikutegemea hayo uliyoyafanya. Lakini ndiyo hivyo ulidanganywa ukakubali sasa siasa ndiyo hivyo tena imekutupa mkono.[JFMP3][/JFMP3]
 

VIKWAZO

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
1,909
580
aisee,mimi ningekuwa huyu jamaa ningeitisha press conference na kumaliza ya moyomwisho kuwaomba radhi wana KATA,MORE TO COME
 

Ziltan

JF-Expert Member
Aug 20, 2011
2,332
5,900
Hafai kwani kwa umri wake anadai alidanganywa ,kama ni hivyo atapata akili lini sasa,
tamaa tu hizo alidanganywa na vicent vya hawa magamba,
 

Gagnija

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
9,764
6,126
*************

Habari ifuatayo unaweza kuisoma kwenye attachment niliyoweka humu ambayo ni cutting kutoka gazeti la DIRA la leo uk. 02

*************Rasta alitoa msimamo huo baada ya kudai kuwa alijikuta akiingia katika mzozo na viongozi wake wa juu, baada ya kuponzwa na wenzake bila kujijua.


Alisema kwa sasa ameamua kuachana na siasa na kushughulika zaidi na shughuli zake na kwamba hatoshiriki kwenye vikao vya baraza la madiwani.

"Kwa sasa sina mpando kabisa na siasa, kwanza zimeniharibia mambo yangu mengi sana na wala sitegemeu kushiriki hata vikao vya madiwani, wameniletea baru kushiriki kikao tarehe 8 mwezi huu, nimewaambia sitakuwepo," alisema Mpanda.
Huyu kakubuhu kwa unafiki. Kama ameamua kuachana na siasa, anashindwa nini kuwajulisha hivyo hao waliomletea barua ya mwaliko wa kikao cha madiwani?
 

Gwallo

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
3,088
3,459
Hafai kwani kwa umri wake anadai alidanganywa ,kama ni hivyo atapata akili lini sasa,
tamaa tu hizo alidanganywa na vicent vya hawa magamba,

Ziltan, anapaswa kuomba msamaha jamii ya wanaKaloleni kwa ujinga alioufanya kisha anatangaza hapo hapo kuachana na siasa kama anavyodai. Naamini hamaanishi kujutia aliyofanya ili apate huruma ya wananchi tena ili awe kiongozi wao.
 

Pezzonovante

JF-Expert Member
May 1, 2008
639
41
Sometimes and all mtimes politicians awelewki duu je ungeona wakati wa uchaguzi ungejua kwamba jamaa alikuwa na nia na siasa mtikisiko mdogo tu anagwaya je alipandwa kwenye jiwe au mchangani?
 

Nyunyu

JF-Expert Member
Mar 9, 2009
4,354
1,005
Hata vitabu vya dini vinaelezea wazi endapo mfuasi akipotoka na kujirudi, atapokelewa kwa amani kabisa. Cha muhimu yeye ajutie maamuzi yake hadharani na ndipo aache siasa, hvyo bado tu kivuli chake kitamsumbua!!
 

Mthuya

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
1,415
228
Namuonea huruma tatizolake alifuata mkumbo sasa wamebaki wawili tune mwishowao,people poweeeeeeeeeer
 

mwinukai

JF-Expert Member
May 3, 2011
1,448
630
Basi kwa vile sasa anjutia na anasema alifuata mkumbo bac aombe radhi na sasa Arudishwe,na wale waliokomaa kwenda huko kwenye vikao waumbukae peke yao
 

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,187
DIWANI RASTA TUNAKUOMBEA MSAMAHA CDM KWA KUONYESHA KUJUTA KWAKO
MAKOSA YA KI-MKUMBO HAPO A-TOWN


Chonde Mhe Mbowe na Dr wa Ukweli Mhe Slaa,
huyu chaliii wetu Diwani RASTA yuko REMORSEFUL kwa kutambua kosa lake dhidi ya Waheshimiwa Wapiga kura wa A-Town, chama chetu cha CDM pamoja na majirani zake kwa ujumla.

Kitendo cha huyu bwana kutoona sababu yoyote ya kuendeleza vita na chama chetu hata baada ya kuadhibiwa vikali, kuamua kuendelea na utiifu hata katika machungu ya kutumikia kifungo chake CHADEMA; nawasihi sana wakubwa wangu Prof Baregu, Dr Mkumbo, Mzee Ndesamburo, Mhe Zitto Kabwe, Halima Mdee - kateueni Kikundi Kazi kutazama upya mwenendo mzima wa baadhi ya Madiwani wa Arusha kwa ajili ya kuwatenganisha (i) kundi la wa wale Madiwani WACHUMIA TUMBO tofauti na (ii) wale ambao walijikuta tu kwenye mkumbo wa wale Watoto wa George Mkuchika.

Natumai hili litaweza kuangaliwa kwa jicho la tatu kwa ajili ya kurudisha kundini wale Madiwani wetu waliokwisha kujutia dhambi zao na kusema sala za toba kimya kimya majumbani kwao na vitendo vyao kutubainishia hilo sawa na hili la Diwani Rasta wa kule A-Town.

Kwa wale madiwani wanaoonekana kuendeleza mapambano na chama bila kujutia makosa yao shauri yao huko!!!

waombe wana wa Arusha msamsamaha.binafsi nilikuamini sana lakini ulichokifanya sikuamini pia sikufurahia hata kidogo. nivizuri ukajuta then wengine wajifunze kutokana na usaliti wako
 

Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,990
4,502
DIWANI RASTA TUNAKUOMBEA MSAMAHA CDM KWA KUONYESHA KUJUTA KWAKO
MAKOSA YA KI-MKUMBO HAPO A-TOWN


Chonde Mhe Mbowe na Dr wa Ukweli Mhe Slaa,
huyu chaliii wetu Diwani RASTA yuko REMORSEFUL kwa kutambua kosa lake dhidi ya Waheshimiwa Wapiga kura wa A-Town, chama chetu cha CDM pamoja na majirani zake kwa ujumla.
Hivi kila diwani akijitetea kuwa alifuata mkumbo itakuwaje nani atakubali kuwa ndiye alifuatwa.
 

Speaker

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
6,327
2,227
Huyo hajajutia hata kidogo.
Nakumbuka siku naangalia matokeo,akaoneshwa huyo rasi akaoneshwa star tv,...
ingawa alikua arusha,ila mdogo wangu alimfurahia kweli.
Nilianza kupatwa na wasiwasi nae siku hiyo hiyo,ila nahisi nilikosea hasa ukizingatia
leo nimejua alimaanisha nini,....

Alisema 2015 anataka agombee ubunge,nikahisi huyu anataka kuleta mzozo chadema
ila leo kasema alitaka kugombea mwanza,....okey.

Omba msamaha,ukifanyika mkutano arusha naamini utaombewa msamaha na
utaonekana shujaa,after that achana na siasa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom