Uchaguzi 2020 Diwani wa CCM Martini Munisi, akimbilia Mahakamani kupinga Uchaguzi Mkuu ujao

Kampeni ya CCM 2020 bila hawa watu itakuaje watakao vyaa viatu vya hawa .Nape,Mwigulu,January,Bernard,Kinana naona kama wamewatenga na awawamini tena lisha ya baadhi kujipendekeza
 
Diwani wa ccm Martin Munisi kutoka Kata ya Machame Wilayani Hai ,Mkoa wa Kilimanjaro amejipanga kukimbilia Mahakamani kufungua shauri Mahakama Kuu kanda ya Kilimanjaro kutaka ahirisho la uchaguzi mkuu ujao sababu ya presha ya Corona.

======

View attachment 1394783
Diwani wa Machame Martin Munisi amekusudia kuwasilisha kesi Mahakama kuu ya Tanzania Moshi kuitaka serikali kusitisha maandalizi ya uchaguzi mkuu mwaka huu na kuzuia mikusanyiko ya kampeni pesa hizo zielekezwe Wizara ya Afya ilikuendeleza kampeni ya kujikinga na COVID-19

Sent using Jamii Forums mobile app
Atakuwa "shogaa"
 
Diwani wa ccm Martin Munisi kutoka Kata ya Machame Wilayani Hai ,Mkoa wa Kilimanjaro amejipanga kukimbilia Mahakamani kufungua shauri Mahakama Kuu kanda ya Kilimanjaro kutaka ahirisho la uchaguzi mkuu ujao sababu ya presha ya Corona.

======

View attachment 1394783
Diwani wa Machame Martin Munisi amekusudia kuwasilisha kesi Mahakama kuu ya Tanzania Moshi kuitaka serikali kusitisha maandalizi ya uchaguzi mkuu mwaka huu na kuzuia mikusanyiko ya kampeni pesa hizo zielekezwe Wizara ya Afya ilikuendeleza kampeni ya kujikinga na COVID-19

Sent using Jamii Forums mobile app
Ki ukweli inakera ccm inajinadi kuwa yenyewe ndio Srkl halafu hao hao ndio wanaoona ipo haja ya kukataa ya srkl... yaani ccm kuipinga ccm mahakamani .... yaani hofu ya mafua ya COVID-19 serikali ndio imetaharuki... wananchi hawana shida na uchaguzi....kwanza tumeona namna ulivyoendeshwa mwaka 2019.... eti tatizo ilikua kujaza fomu eti Watanzania waliokuwa wagombea wa upinzani hawakujua kuzijaza ilhali ni wajibu wa wasiamamizi kuhakikisha fomu zinajazwa kirahisi na kwa usahihi kushindwa kujazwa fomu za uchaguzi ni kushindwa kwa shughuli nzima ya uchaguzi yaani Tume ya Uchaguzi ... manake haiwezekani 95% ya wagombea wa upinzani wameshindwa kujaza halafu bado uchaguzi ukaendelea huu ndio ulikua ushahidi wa tume kuwa ni kitengo cha ccm.

Katika hili Mahakama itajidhihirisha je ipo huru kwa ccm au la? Manake Srkl tayari ipo kitanzini kwa kauli ya wanaccm wenyewe na wala hakuna pingamizi kutoka srkl kuwa ndio ccm
 
Mzaha mzaha ,ccm ndo hilla zao hizo,wanajuwa uchaguzi ujao wataambulia majanga,na hassa kukiwa na tume huru.
sasa unaweza kuona kama vile huyo jamaa kakurupuka vile,kumbe ni mpangokamili wa Polepole
 
MTIKILA AIBUKIA MACHAME

Jana tarehe 26.03.2020 Diwani wa Machame Martini Munisi amewasilisha rasmi maombi maalumu ya notisi ya siku 90 kwa mwanasheria mkuu wa serikali akitaka uchaguzi mkuu wa mwezi October uhairishwe kutokana na tishio la maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Diwani huyo wa chama cha mapinduzi amedai kwamba lengo lake kuu ni kujali afya za watanzania na sio vinginevyo,Munisi amedai kuwa Bado wanaImani kwa kuwa Rais Magufuli hajayumba sehemu yeyote basi ni heri kuhairisha uchaguzi ili kushugulikia suala la corona na fedha zilizopangwa kwajili ya uchaguzi zielekezwe katika kada nyingine ama katika kada ya afya ili kuwaokoa watanzania katika janga hilo.

Munisi ameenda mbali kudai wananchi ndio waliompa msukumo wa kuwasilisha shauri hilo na sio katumwa na mtu binafsi kama wengi walivyoanza kutafsiri hatua yake hiyo.


Hatua hii ya Munisi imepelekea Wanasheria,mawakili na wananchi kumfananaisha na Marehemu Christopher Mtikila na wengi wakidai Walitamani kesi za namna hii zirejee maana zilikuwa na mantiki kubwa na zilipotea toka kufariki kwa Mtikila.

Kwa upande wa Mshauri Mkuu wa Diwani huyo kwenye kesi ambae pia ni Diwani wa Manispaa ya Moshi Ndugu Juma Raibu amedai shauli lao lina mantiki sana na wako tayari kufika mpaka mahakama ya Afrika mashariki endapo shauli lao litakataliwa na mahakama za nyumbani.


Mwanasheria Mkuu amepokea kusudio hilo na atatolea maamuzi hivi karibuni.





IMG_20200326_131944.jpeg
IMG_20200326_131148.jpeg
IMG_20200326_131509.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom