TARIME: Diwani wa CCM kata ya Susuni auawa kikatili

Nyakarungu

JF-Expert Member
May 1, 2011
472
375
Aliyekua diwani wa kata ya Susuni wilayani Tarime, bwana Nicholous Matiko, amevamiwa na kuuawa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi usiku wa leo.

Habari hizi zinakuja ikiwa ni siku chache tu tangu mtu mmoja wilayani humo katika eneo la Sirari auawe na kuchunwa ngozi na watu amabo hawajafahaika.

Je, kanda maalum ya jeshi la polisi wilayani humo,ina ulalo wa kazi yao wilayani humo?

Mbona wizi wa mifugo unaendelea tu?

Mbona masurgeon wa asili wanaendelea kufanya upasuaji wao kama kawaida?
 
Diwani kupitia ccm wilayani tarime ameuwawa na majambazi usiku wa kuamkia jana 15july.alipigwa risasi na kukatwakatwa mapanga!cha ajabu hao majambazi hawakuiba kitu wala pikipiki aliyokua akiendesha!Jamani tarime mauji yamezidi muogopeni mungu
 
DIWANI wa CCM, Kata ya Susuni Tarafa ya Inchugu wilayani hapa mkoani Mara, Felex Horombe (45) ameuawa kwa kupigwa risasi kiunoni na mguuni na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya, Kamishna Msaidizi, Deus Kato alisema kuwa tukio hilo la mauaji lililotokea usiku wa Ijumaa saa 2 katika eneo la pori la Nyandoto wakati diwani huyo alipokuwa akitokea Tarime Mjini kuelekea nyumbani kwake Kijiji cha Kiongera.

Alisema diwani huyo alikuwa akiendesha pikipiki yake na alipofika eneo hilo, alivamiwa na kundi la watu waliokuwa na silaha aina ya bunduki na kuanza kumshambulia na kumpiga risasi kiunoni na mguuni.

Alisema baada ya kupigwa risasi walimpora bastola yake aliyokuwa akimiliki kihalali na simu yake ya mkononi na kuitelekeza pikipiki hiyo katika eneo la tukio.

Jeshi la Polisi lilifika eneo hilo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka kufanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Wilaya Tarime ambapo umehifadhiwa ukisubiri kufanyiwa mipango ya maziko kijijini kwake Kiongera.

Hata hivyo, Kamanda Kato alisema polisi wanaendelea na uchunguzi wa mauaji hayo na kwamba hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na mauaji hayo.
 
Magwanda wa huko wachunguzwe maana wao ndio "wapiganaji"!
 
Kutakuwa na ishu za kisiasa hapa! Majambazi gani wakuvamie na wakuue bila kuchukua chochete?
 
kwa kuwa umejidhihirisha mwenyewe umebeba box kichwani, ushauri wa bure, kwenye jina lako futa herufi M linalobakia ndio jina lako. POLENI WAFIWA
 
Kutakuwa na ishu za kisiasa hapa! Majambazi gani wakuvamie na wakuue bila kuchukua chochete?

DIWANI wa CCM, Kata ya Susuni Tarafa ya Inchugu wilayani hapa mkoani Mara, Felex Horombe (45) ameuawa kwa kupigwa risasi kiunoni na mguuni na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya, Kamishna Msaidizi, Deus Kato alisema kuwa tukio hilo la mauaji lililotokea usiku wa Ijumaa saa 2 katika eneo la pori la Nyandoto wakati diwani huyo alipokuwa akitokea Tarime Mjini kuelekea nyumbani kwake Kijiji cha Kiongera.

Alisema diwani huyo alikuwa akiendesha pikipiki yake na alipofika eneo hilo, alivamiwa na kundi la watu waliokuwa na silaha aina ya bunduki na kuanza kumshambulia na kumpiga risasi kiunoni na mguuni.

Alisema baada ya kupigwa risasi walimpora bastola yake aliyokuwa akimiliki kihalali na simu yake ya mkononi na kuitelekeza pikipiki hiyo katika eneo la tukio.

Jeshi la Polisi lilifika eneo hilo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka kufanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Wilaya Tarime ambapo umehifadhiwa ukisubiri kufanyiwa mipango ya maziko kijijini kwake Kiongera.

Hata hivyo, Kamanda Kato alisema polisi wanaendelea na uchunguzi wa mauaji hayo na kwamba hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na mauaji hayo.
walimpora bastola yake aliyokuwa akimiliki kihalali na simu yake ya mkononi
 
bangi na gongo zimepindisha akili zao ndo mana wanafanya mambo ya kishwain hivi

Diwani kupitia ccm wilayani tarime ameuwawa na majambazi usiku wa kuamkia jana 15july.alipigwa risasi na kukatwakatwa mapanga!cha ajabu hao majambazi hawakuiba kitu wala pikipiki aliyokua akiendesha!Jamani tarime mauji yamezidi muogopeni mungu
 
I suspect ni hizi shoddy deals gone wrong. Majambazi gani wanaua watu kisha wanasepa? Tuambieni basi kuwa alijaribu kupambana nao. RIP
 
Back
Top Bottom