Diwani pekee wa CHADEMA baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Geita ajiuzulu na kujiunga CCM

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
747
3,059
Diwani pekee wa Chadema kata ya Bugalama, Luponya Masalu amejivua uanachama na kutangaza kujiunga na CCM.

Alikuwa ni diwani pekee wa Chadema katika baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Geita.

Masalu amesema ameamua kurudi CCM baada ya kuona Rais John Magufuli anatekeleza mambo aliyokuwa akiyasemea akiwa Chadema.

“Sijanunuliwa wala kutishwa kama baadhi ya wananchi wanavyodai na hakuna mwenye uwezo wa kunihonga lakini nimehama kutokana na utendaji kazi nzuri ya Rais Magufuli,” amesema

Kuhusu kugombea nafasi hiyo wakati mwingine Luponya amesema kwa sasa hawezi kuzungumzia hilo na kwamba atakapotulia atafanya maamuzi kama atagombea tena.

DSC_0384.JPG
 
Back
Top Bottom