Diwani mteule aeleza jinsi wabunge walivyo vaminiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diwani mteule aeleza jinsi wabunge walivyo vaminiwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Apr 5, 2012.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Diwani mteule wa Kata ya Kirumba kwa tiketi ya Chadema, Daniel Kahungu ameelezea namna viongozi hao walivyoshambuliwa.

  Akizungumza na gazeti la Mwananchi, Kahungu ambaye aliibuka mshindi katika uchaguzi mdogo wa Kata ya Kirumba amesema alikuwapo kwenye eneo la tukio saa 8:00 usiku wa kuamkia Aprili Mosi mwaka huu, alisema walivamiwa na kundi la watu zaidi ya 50 wakiwa na silaha za jadi, 30 kati yao waliweza kuwatambua.

  Akielezea mkasa mzima alisema kuwa yeye alikuwa katika gari la mbele kati ya magari matatu waliyokuwanayo walipokuwa wakielekea Kabuhoro ambapo walikuwa wakiwasambaza mawakala wao majumbani.

  Alisema wakiwa njiani katika njia panda ya Mtaa wa Bujumbura, walikutana na gari moja aina ya Land Cruiser nyeupe ambalo walilitambua ni la nani(jina linahifadhiwa).

  Alisema gari hilo lilikuwa limeegeshwa kando ya barabara huku taa zake zikiwaka katika mwanga hafifu. "Tulipoangalia kwa makini zaidi tuliona idadi ya watu wengi wakiwa wamekaa ndani ya gari hilo, jambo ambalo lilitushtua sana," aliongeza na kusema kuwa kutokana na mazingira ya kutia shaka ya gari hilo waliamua kunakili namba zake.

  "Wastani wa kama mita 20 kutoka katika gari hilo tulikutana na gari lingine katika njia panda ya Mtaa wa Bukoba aina ya RAV4 nalo tulilitambua kuwa ni la aliyekuwa (jina linahifadhiwa). Gari hilo lilikuwa na mtazamo wa lile la kwanza likiwa na mwanga hafifu na idadi kubwa ya watu ndani yake," alisema.

  Alisema wakiwa njiani kuelekea katika uwanja wa Shule ya Msingi Bugungumuki gari hizo ziliwafuata kwa nyuma hadi katika uwanja huo wa shule ya msingi ambapo waliwashusha mawakala wao na kuanza kurudi mjini.

  Alisema kuwa baada ya kugeuza magari yao, gari zilizokuwa zikiwafuatilia kwa nyuma ziligeuza na kuanza kuwafuata walikokuwa wakielekea huku gari moja likiwapita kwa mwendo wa kasi kidogo na kuwaweka kati; gari moja likiwa mbele na moja likiwa nyuma.

  Mashambulizi

  Alisema baada ya kuzingirwa na magari hayo kundi la watu waliokuwamo ndani yake walishuka wakiwa na silaha mbalimbali za jadi na kuelekea katika gari la Mbunge wa Ilemela huku wakiwa wanapiga kelele.

  Alisema muda mfupi baadaye magari mengine matatu yaliongezeka yakiwa na watu wengi ndani yake na wao walishuka wakaungana na wenzao na kuanza kufanya mashambulizi.

  My take: Kama watu wanajulikama na gari zinajulikana kunakuwa na ugumu gani kwa watu hao kukamatwa? Nafikiri polisi wanahusika kwa namna moja ama nyingine, au kulikuwa na maagizo toka juu ya kuwadhuru wabunge hasa Mh. Kiwia.
   
 2. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,949
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  time will reveal kila kitu
   
 3. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Ukisoma vizuri, utagundua kuwa POLISI inatajwa kimizengwe.

  1. Katika maelezo haya, hakuna sehemu yoyote ambayo inaeleze na gari la polisi wenye silaha SMG kuwa walikuwepo kama alivyodai HIGHNESS, katika kulalamika kwake, alipodai polisi walikuwepo na SMG tatu, lakini walishindwa kuwasaidia.

  2. Kwa mara ya kwanza, ndo tunaambiwa kuwa walikuwa wanawarudisha mawakala wao nyumbani, walikuwa wapi na wanafanya shughuli gani hatujafunuliwa bado, wakiwa tayari watatueleza kila kitu.

  3. wakati wanashambuliwa, hawa wengine ambao hawajashambuliwa walikuwa wapi, hatujaelezwa.

  4. Hawa watu wanafahamika zaidi kwa CDM, lakini kuna uwezekano hawataki kuwataja, kwani kama uliangalia taarifa ya habari ya juzi star tv, Barlow aligomba na kumpiga stop mwandishi mmoja kutohudhuria vikao vyake, kwa madai kuwa alikuwa anawafahamu kwa majina waliohusika, lakini hataki kuwataja. Na Barlow alisema kuficha taarifa za wahalifu, na wewe ni mhalifu, unatakiwa ushitakiwe, bila shaka ni kwa mjibu wa sheria ya ushahidi

  Thus, CHADEMA wasipokuwa makini, heshima yao itashuka, kwani majambazi yanajulikana, lakini hawataki kuyataja, hata kwenye habari hii, bado yemefichwa ili wananchi tusiwafaham. kama wameweza kuaandika yote waliyoandika, majina ya majambazi na namba zao za magari yaliyotumika ndo iwe nongwa? kuna wanalolifahamu hapo CHADEMA, wanaogopa kuumbuka, lakini mda ukifika wataeleza kila kitu, tusubiri.

  na wakati haya yakiendelea, tayari CCM wamemwandia mwenyekiti wao, Rais Kikwete kuwa, POLISI wilaya ilemela, wote ni CHADEMA. Madai ya kuituhum POLISI Mwanza kuwa ni wafuasi wa CDM, yalianza kusikika mara baada ya VIGOGO wawili wa CCM kuangushwa kwenye uchaguzi wa 2010, ambapo POLISI ilisimama kulinda kura na wachaguliwa wa wananchi kushinda.

  Wanawatuhum POLISI kuchana bendera ya chama cha magamba na kuwatimua mahali walipokuwa wakifanyia mkutano wao wa kuhitimisha kampeni hizo siku ya 31.03.2012, ambapo SITA ndiye aliyekuwepo na wanataka RAIS awawajibishe kwani kwao imekuwa ni kikwazo.

  Tetesi zinasema, RC katibuana na uongozi wa polisi Ilemela, na mpaka sasa haziivi kabisaaaaaaa

  My take.

  Wananchi tukiwa watu wa kuchukua maneno ya wanasiasa bila kuyaweka kwenye mizani ya CRITICAL THINKING, watatuyumbisha halafu mwisho wa siku ni sisi tutakao umia.

   
 4. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  For sure mkuu. Maelezo ya awali ya Higness, alieleza alikuwa peke yake wakati anashambuliwa, ndo akampigia simu MACHEMLI naye akashambuliwa. Lakini diwani yeye hata jeraha la jiwe hana, na anasema alikuwepo wakati yote yanatendeka. Wamekuwa wakipingana wao kwa wao. na tayari kupitia mkutanop wa jana, wametoa siku tatu polisi kuwakamata wote waliohusika, sina hakika kama tamko hilo limeendana na kuwataja wahusika
   
 5. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  Malima aliibiwa akifanya uzinzi, jeshi la polisi lilichachamaa kuanzia kuruta hadi igp hadi wezi kukamatwa na vitu vikapatikana, inakuwaje wahalifu wanaotumia silaha wanatanua bila jeshi letu la polisi kuwasaka badala yake wapanga foleni kuchukua mishahara? sioni busara ya kulipa kodi!!!!
   
 6. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  ntamaholo

  Unaongea kama hulijui jeshi la polisi, ungekuwa mkenya ningekusimulia.

  RPC Barlow amekiri askari wake kujificha chini ya uvungu wa gari sasa wewe unaleta stori gani kwamba polisi hakuwepo. Kama ni majina tayari wanayo na siku ya tukio Zitto alimtaja suspect wa kwanza kiongozi wa UVCCM aliyejifanya ni CDM, sasa hao unaosema wamefichwa na CDM n wapi.

  Nyie endeleeni kuwatetea polisi waharifu one day you gonna pay the price.
   
 7. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Ingekuwa mbunge wa magamba paul chagonjwa angetumwa kwa wananzengo
   
 8. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  hongera jeshi la mali kwa mapinduzi matakatifu,.
   
 9. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,719
  Likes Received: 1,628
  Trophy Points: 280
  sasa tumsilize nani Highnes muusika ua polisi mletewa taarifa?
   
 10. T

  Tanzaniaist Senior Member

  #10
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mavi matupu...! Nadhani kama mama ako angekushushiwa hicho kipigo nadhani ndio ungepata akili
   
 11. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  hujui unalolisema, ukikua utaacha.
   
 12. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  mwenyewe una majibu tumsikilize nani. kumbuka mmoja lazima awe biassed
   
 13. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2012
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Maelezo yako yanaonyesha kuwa huipendi CHADEMA. Kutaja majina kwenye vyombo vya habari ni hatari zaidi ya unavyofikiria. Wale jamaa walikuwa na nia ya kuua kabisa na inawezekana walitumwa. Na kama wametumwa aliyewatuma ni mtu mzito. Kushughlika na watu wazito kunahitaji u makini wa hali ya juu kwa sababu wana uwezo wa fedha na ushawishi mkubwa wa wananchi wengi. Kwa hiyo suala hili inabidi lifanyiwe kazi kwa umakini wa hali ya juu. Sio kwa kutaja majina. Mimi sijaona kupingana kwa taarifa kati ya ile ya wabunge waliocharangwa mapanga na hii ya Diwani mteule. Kama wangeamua kuleta inayofanana kabisa wangefanya hivyo. Kinachohitajika ni details tu ambazo nadhani zitakuja hapo baadae
   
 14. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #14
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,131
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Kwenye taarifa mbalimbali kwenye vyombo vya habari tumesikia kua Muheshimiwa Kiwia wakati anapata tafrani hiyo Polisi walikuwepo na isitoshe tumesikia pia kamanda huyo wa Polisi anadai wakati wanafika kwenye tukio waliwakuta vijana wa CCM wamewaweka chini ya ulinzi waheshimiwa hao! Sasa inakuwaje tena jeshi la Polisi liseme litawashikilia waheshimiwa wabunge kwa uchunguzi zaidi? My take je wale vijana wa CCM ambao walikutwa wamewaweka chini ya ulinzi waheshimiwa hao si lazima nao waisaidie jeshi la Polisi? Kuna utata hapa.
   
 15. A

  Afghan Member

  #15
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haujatulia wewe! Kila siku majina yanatajwa, akina mohamed na wenzake wewe uko wapi? Unajidhalilisha bure kutoa maelezo marefu kumbe hakuna chochote cha maana unachoeleza. Hata polisi kwa taarifa yako wameshakamata baadhi ya watu. Acha ujinga
   
 16. Silly

  Silly JF-Expert Member

  #16
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 508
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  jeshi la polisi Tanzania tu ndo lina sifa ya kusubiri kupelekewa ushahidi -duniani - sehemu/nchi zingine majeshi yao yanasaka ushahidi kwa njia zao,
   
 17. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #17
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Childish! Kwanini msiwe mnajibu hoja badala yake mnaandika matusi humu. Mtoa hoja kaleta mambo kibao kulingana na mtizamo wake wewe unakuja na sentensi moja isiyokuwa na hata chembe ya ustaarabu. Kuweni waungwana, hata kama bado mna akili za kisekondari.
   
 18. e

  erasmi Member

  #18
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  One day Yes! Nina imani kutakuwa na mabadiliko.
   
 19. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #19
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
   
 20. a

  ambwene_ambwene Member

  #20
  Apr 5, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MUNGU KWETU SISI NI KIMBILIO NA NGUVU..........zAB.46:1
   
Loading...