Patriote
JF-Expert Member
- Jul 13, 2011
- 1,718
- 1,047
Nimefuatilia kwa makini mijadala mbali mbali ya Katiba na hata ya kijamii, nimegundea suala la elimu anayopaswa kuwa nayo kiongozi halitajwi sana, hii inaweza kuwa inachangiwa na viongozi wenyewe kutokuwa na elimu ya kulidhisha, hivyo mada ya level ya elimu kwao inakosa mvuto. Lakin ndugu zangu lazma tujue kuwa elimu ina mchango mkubwa katika utendaji wa jamii mbalimbali, sisemi lazma viongozi wawe na PHD, la hasha, ila kuna umuhimu kwa kiongozi kuwa angalau na kiwango fulani cha Elimu kuliko ilivyo sasa ambapo hakuna kiwango chochote kinachotajwa zaidi ya kusema awe Raia anayejua kusoma na kuandika.
Nimepita kwenye CV mbalimbali za waheshimiwa wetu kwa kweli kwa CV zile tusitegemee ya ajabu, Wanachokifanya sasa hivi wanajitahid sana kwa CV zile. CV nyingi zimekaa kiujanjaujanja, hazina mtiririko mzuri na kwa kweli ni aibu kwa Taifa. Mara mtu kasoma hadi O-level then kaunga Degree. Utaratibu wa wapi huu???Au labda zimenakiliwa vibaya??? Kwa sasa nalazimika kuamin waliozinakili wamenakili vibaya kwenye website ya bunge, naomba wahusika wazirekebishe. Sasa hali ipo hivyo kwa Bunge, Je hali ipoje huko chini kwa madiwami na watendaji wa vijiji tunapotegemea maendeleo yafanyike???
Mimi nadhan kuna haja sasa kupose changamoto kwa kuweka kigezo cha elimu, ili anayefikiria kuomba uongozi fulani ajipange kwanza kabla ya kuamua kufanya hivyo. Hii ni sawa kabisa na mtu anayefikiria kuwa mhasibu kujipanga kwanza kwa kwenda chuoni kupata elimu ya uhasibu. Hili suala la kusema raia yeyote ili mradi awe na uwezo wa kujua kusoma na kuandika mimi nadhan kwa karne hii limeshapitwa na wakati. Katiba ya mwanzo ilikuwa na kigezo hicho maana wasomi hawakuwepo, leo miaka 50 ya uhuru bado kigezo ni hicho hicho jaman???Basi kama kigezo cha kiongozi wa nchi hii ni hicho?? basi hata kwa kazi nyingine kigezo kiwe ni hicho hicho. Kwa nini serikali inataka mfanyakazi wa kawaida kama msaidizi wa ofisi au tarishi/mesenja awe na elimu fulani wakati kiongozi wa ngazi ya juu kama Mbunge au Waziri hajawekewa kigezo cha Elimu???Mimi nadhani suala la elimu halihitaji siasa. Kama viongozi wetu hasa watunga sheria hawana elimu ya kutosha ni dhahiri hata sheria zinazotungwa zitakuwa ni za kibabaishaji. Hebu wana JF tulijadili hili.