Diwani Kisarawe ang'aka kuitwa mbumbumbu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diwani Kisarawe ang'aka kuitwa mbumbumbu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Feb 17, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  17 FEBRUARY 2012
  Na Peter Mwenda, Kisarawe


  MADIWANI katika halmashauri ya Kisarawe, mkoani Pwani, wameitwa mbumbumbu kwa kuidhinisha sh. milioni 500 kwa ajili ya bajeti ya maendeleo ya elimu kwa kipindi cha mwaka 2011/2012.

  Pamoja na kuidhinisha fedha hizo, madiwani hao wanadaiwa kutenga fedha nyingi zaidi ya hizo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi wa halmashauri na manunuzi ya gari.

  Madai hayo yalijitokeza juzi katika warsha ya utawala bora iliyofanyika mjini ambayo iliandaliwa na Asasi ya Mfuko wa Maendeleo Kisarawe (KIDEFO), ikihusisha wakazi wa Kata ya Msimbu, Msanga, asasi za kiraia na makundi maalumu.

  Akitoa mada katika warsha hiyo, Mwezeshaji kutoka DEFCO, Bw. Bugi Ngeseni, aliwaambia washiriki hao kuwa madiwani hao wameidhinisha sh. milioni. 500 ambazo hazitoshi kuendeleza sekta hiyo hasa kwa kuzingatia uduni wa elimu inayotolewa wilayani humo.

  "Fedha zilizotengwa katika sekta ya elimu ni chache sana wakati zile zilizoidhinishwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi na manunuzi ya gari ni kubwa, ujenzi wa nyumba imetengwa milioni 180, ununuzi wa gari milioni 120, na lingine la ukaguzi milioni 140.

  "Mimi nimesoma Sekondari ya Mwaneromango, ambayo imesomesha viongozi wengi na wataalamu katika sekta mbalimbali akiwemo mbunge wa Kisarawe, Bw. Suleiman Jafo, shule hii imeshika nafasi ya pili kutoka mwisho katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2011," alisema Bw. Ngeseni.

  Aliongeza kuwa, Wakurugenzi wamekuwa wakiunda kikundi cha madiwani wao ambao wanawaburuza katika vikao vya halmashauri kwa sababu ya elimu zao ni darasa la saba.

  Bw. Ngeseni alisema elimu hiyo haiwawezeshi kuwa na uwezo wa kujenga hoja katika vikao vya halmashauri ambavyo taarifa zake zinaandikwa kwa lugha ya kiingereza.

  Mshiriki wa warsha hiyo, Bi. Monica Mahoza, alisema tatizo la elimu kwa madiwani wa Kisarawe ni kubwa hivyo ni vigumu kuchanganua bajeti ya halmashauri.

  Kauli ya madiwani hao kuitwa mbumbumbu, ilimfanya Diwani wa Vikumburu Bw. Juma Dihonga kwa tiketi ya CUF, kucharuka na kupinga hatua ya mtoa mada kuwaita mbumbumbu.

  Hata hivyo, Bw. Dihonga alilazimika kutulia baada ya washiriki kuungana na watoa mada wakisisitiza kuwa, madiwani hao hawakutumia busara ya kutenga fedha chache kwa maendeleo ya elimu na kutenga fedha nyingi kwa mambo yasiyo ya msingi.

  "Nimekubali maoni ya wananchi wa Kisarawe, naahidi sitakuwa tayari kupitisha bajeti ambayo haina manufaa kwa wananchi," alisema.

  Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Jinsia wilayani humo, Bi. Gretude Mwanakadudu, alisema amewahi kusikia wenyeji wa Kisarawe walikataa ujenzi wa hospitali ambayo hivi sasa imejengwa mkoani Kilimanjaro ya KCMC, kutokana na msimamo wa udini
  .
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Madiwani mbumbumbu watoke nje...

  Sababu tunasikia kuna walioweka udini wakazuia hospitali isijengwe...
   
 3. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tatizo ni CCM!
   
 4. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Umbumbumbu mbona umetapakaa kwenye serikali nzima! chunguza kama hutaamini hili
   
 5. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145

  Mimi natambaa na paragraph ya mwisho tu!

   
 6. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  wakaseme kwa baba mwanaasha
   
 7. b

  braza makaptula Member

  #7
  Feb 18, 2012
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tatizo la madiwani mbumbumbu lipo sana Tanzania hasa maeneo ya vijijini, kwa kweli wengi wao wamekuwa wasumbufu, kazi yao ni kuwaazimia wakurugenzi na wataalam mbalimbali, we mtu wa la saba hata balance sheet huijui unataka umkague DT unaanzia wapi?
  kwa kweli hakuna sehemu sensitive kwa maendeleo kwa sasa kama kwenye halmashauri, tunatakiwa tuwe na strong team wilayani ili ziweze ku produce plan zinazoeleweka badala ya kukwamisha miradi bila kuwa na utaalamu wowote, wamesomea majungu tu kwa watumishi
  I hate madiwani wasioenda shule, Serikali ibadilishe vigezo vya kugombea, tuanze na ngazi za diploma, na hata kwa wabunge pia
   
 8. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,663
  Likes Received: 3,317
  Trophy Points: 280
  Mkoa wa pwani ndio shamba la ujinga tanzania kuanzia msomi hadi kilaza,yoooote iko jinga tu,
   
 9. D

  DOMA JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Me narudia kama vp poa tu maana najua yote ni magamba maana pwani ni daraja la magamba"MADIWANI WA KISARAWE NI MBUMBUMBU"
   
 10. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Umehudhuria Mikutano ya CCM? Umeona Jinsi Watu wanavyoongea walio kwenye Mashina ya CCM? Wanavyojua kupeperusha hizo bendera za CCM? na kuongea hatua na Malengo ya Chama blila kijitabu cha CCM? Sasa hao watu wakitaka kugombea Uongozi ni lazima utawapab BY ANY MEANS necessary hautawauliza CV yako iko wapi?

  Kwahiyo ni kawaida hao ndio waliokuwa na ndio viongozi wa chama chetu tawala hawaandiki chochote kitabuni ni kuongea kwa CAPITAL LETTERS. unaondoka unajua CCM imakuangukia....
   
 11. w

  wimbi la mbele JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2012
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 647
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  .................
   
Loading...