Diwani Isaya Doita aliyemtuhumu Godbless Lema afukuzwa Uanachama

Hivi ukimtukana mtu usiyemjua unapata faida gani? Unajisikia kama kambabe fulani au siyo? Bila shaka wewe ni mashabiki na sio mwanachama wa Chadema.
Huyu unaemshambulia amesema hadharani kinachomkera katika chama chake kwa sababu anaona kinakoelekea si kizuri. Kwa kufanya hivyo amekipa fursa ya kuchunguza yale anayodai na kujirekebisha kama inabidi. Au mlitaka azungumzie kwenye vilabu vya pombe ambako ndiko kuna wapiga kura wengi?

Amandla....
Akili maandazi sio tusi. Kuhusu kusema,yeye ni diwani anapo pa kuzungimzia yote ya moyoni hivyo kuja kusemea kwenye press ni uhuni ili ufukuzwe upate milage ya kisiasa.
Huku mtaani ni kwa wale wasio na vikao rasmi vya kuzungumzia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ajibiwe wapi? Mm nimekuuliza umeona sababu za kufukuzwa kwenye barua yake? Ni tuhuma zipi ambazo ametoa? Ni taratibu zipi za kichama ametumia kuwasilisha tuhuma, kama unavyoziita, halafu akapuuzwa? Tangu lini mhubi kwenye chama akitimuliwa inaitwa kuwa ni chama kimevurugika?
Barua ya kufukuzwa (iliyoandikwa na Katibu Kata wake) imetoka baada ya video ya yeye kuwasema vibaya viongozi wa Chadema Arusha ( hakumsema Lema peke yake) kusambaa kwenye social media. Sasa mtu yeyote ataviunganisha hivyo vitu. Kama kuna sababu nyingine basi waliomfukuza wataweza kuitoa. Mimi sio mwanachama wa Chadema kwa hiyo siwezi kujua kwa uhakika kama aliwahi kuwasilisha tuhuma zake kwenye vikao vya kilichokuwa chama chake. Labda wewe utuambie. Kufukuzana ovyo ndiko kulikoonyesha kuwa CUF kuna matatizo. Nisingependa Chadema nao watumbukie huko huko. Lakini mwenye macho haambiwi tazama.

Amandla.......
 
Mimi huwa nawambia chadema mambo ya demokrasia ni magumu sana ni rahisi kuongea mdomoni lakini kuitenda ikawa ngumu kidogo!

Yani mtu katoa tuhuma leo na kesho kafukuzwa hahaha hivi chadema mlikaa saa ngapi kumjadili huyo mtu hahahaha


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Taratibu za kukosoana ziko kikatiba na zinapaswa kufuatwa.
Hivi huko ccm kiongozi mmoja anaweza itisha press na kumtuhumu wa juu yake badala ya vikao?

Sent using Jamii Forums mobile app

Hahahaha ziko kikatiba gani hahahaha kwanini Lema hakufukuzwa alipo mkosoa Lowasa mitandaoni? Hahahaha


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Hahahaha hivi chadema kweli mgeweza kumvumilia mtu kama Membe hadi leo hahahahaha hakika CCM ni baba wa demokrasia


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Akili maandazi sio tusi. Kuhusu kusema,yeye ni diwani anapo pa kuzungimzia yote ya moyoni hivyo kuja kusemea kwenye press ni uhuni ili ufukuzwe upate milage ya kisiasa.
Huku mtaani ni kwa wale wasio na vikao rasmi vya kuzungumzia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo " akili maandazi" ni sifa nzuri?
Kwa kujua kuwa anatafuta ujiko wa siasa ndio mkaone heri mumpe ujiko huo!

Amandla.......
 
CDM yangu sijui imepatwa na nini kwani Lema ni Mungu asituhumiwe? CDM inazidi kuondoka kwenye lengo na hii ni furaha na shangwe kwa mahasimu wetu....
Walipomkaribisha Lowassa ambaye walituaminisha ni fisadi papa kwa zaidi ya miaka 8 na kuanza kumuimbia mapambio ya Lowassa Mabadiliko, wenye fikra kubwa tulijua CHADEMA imepoteza dira/malengo!

Haya yanayotokea kwa sasa ni mwendelezo wake!
 
Nimemsikia, alichosema ni ukweli mtupu na ukweli mchungu ambao kila uchao ninaendelea kuuzungumza hadi October 2020, haya maneno huyu diwani kayasema jana, leo katimuliwa na kikao gani?.

Kuna utaratibu wa mashitaka kwa mujibu wa katiba ya Chadema, umefutwa?. Hii isije kuwa ni kama kutimuliwa kwa Zitto na Shonza, ni kumpiga teke chura.. Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili Kuwatendea Haki Watanzania 2015!

Huyu jamaa tayari ameisha jitambua, yuko njia kuu.

P
Makosa ya Kangi ni yapi?
 
Huu ni ujinga uliopitiliza. Chama kilichokomaa ni lazima kikubali kukosolewa. Kwa kumfukuza, kinathibitisha alichosema kuwa Arusha kweli kuna tatizo. Walitakiwa kumshukuru kwa kuwa muwazi na kufanyia kazi tuhuma zake. Uamuzi wa kumfukuza mtu uanachama hautakiwi kufanywa kirahisi rahisi hivi.

Amandla
Viongozi wengi wa kisiasa hasa katika vyama vyetu vya upinzani hawana busara!
 
Mbona huyo huyo Lema Kuna kipindi alimkosoa mhe. Lowassa kwa kutumia social network wakati lowassa yupo chama Cha chadema alipoenda kukutana na Magufuli ikulu mbona hakutumia vikao vya chama na Wala hakuchukuliwa hatua zozote na chama chake.Tusipende kutanguliza mahaba kwenye mambo ya msingi.
Hawawezi kukuelewa kwa sababu ni kati ya kundi ambalo political blind follower!
 
CHADEMA hakuna njia nyingine zaidi ya kutimuana, hata vikao vya majadiliano hakuna... Kwa nini msiwe mnajipa nafasi kabla ya kutimuana.!!

Mkuu hii Avator yako inanikumbusha pale tulipomweka pembeni mpambanaji na kumkumbatia Fisadi...
 
Diwani wa Kata ya Ngarenaro kwa tiketi ya CHADEMA, Isaya Doita aliyemtuhumu Godbless Lema kuwa hajui kazi na majukumu yake kama kiongozi wa juu wa CHADEMA na pia kama Mbunge amefukuzwa uanachama kwa kosa la kukiuka kanuni na misingi ya uanachama wa chama.

Kufukuzwa Uanachama kunamfanya kupoteza hata Udiwani wa Kata ya Ngarenaro kwa sababu Diwani lazima awe na udhamini kutoka chama cha siasa.

Ikumbukwe kuwa Juzi kupitia vyombo vya habari, Diwani Isaya alimtuhumu vikali Mbunge Godbless Lema kuwa hajitambui na hajui majukumu yake kama Mbunge, Mwenyekiti wa Kanda na Mjumbe wa Kamati Kuu ambapo imesababisha chama kudhoofika na kukimbiwa na baadhi ya Madiwani wa Jiji la Arusha.

Kufukuzwa kwa Diwani Isaya Doita kunafanya awe Diwani wa 14 katika Jiji la Arusha kwa tiketi ya CHADEMA aliyeondoka CHADEMA baada ya Uchaguzi Mkuu 2015.

Ukitaka kusoma na kuangalia video ya tuhuma unaweza kugonga Link hii:

Link > CHADEMA Arusha ‘’kwafuka moshi’’; Godbless Lema aambiwa hajitambui na hajui majukumu yake


Barua ya kumvua uanachama
EPUVdxeXUAA597w


Video ya tuhuma kwa Godbless Lema

Jamani mbona Diwani alikuwa anawaambia ukweli viongozi wake, kumbe hawapendi kuambiwa ukweli ila wao wanapenda kuwaambia wengine ukweli, hakuna demokrasia hapo bali ni changa la macho tu. Chadema kama FIFA ukipeleka kesi Mahakamani kukishitaki chama basi wewe si mwanachama tena, kuna demokrasia hapo...!!!!
 
Back
Top Bottom