Diwani Isaya Doita aliyemtuhumu Godbless Lema afukuzwa Uanachama

Mbona huyo huyo Lema Kuna kipindi alimkosoa mhe. Lowassa kwa kutumia social network wakati lowassa yupo chama Cha chadema alipoenda kukutana na Magufuli ikulu mbona hakutumia vikao vya chama na Wala hakuchukuliwa hatua zozote na chama chake.Tusipende kutanguliza mahaba kwenye mambo ya msingi.
Ukipata jibu hapo tutashtuana basi.
 
Hakuwa na sababu ya kwenda kuongea na nyombo vya habari masuala yaliyotakiwa yajadiliwe ndani ya vikao vya chama. Huyo diwani ni kiongozi tena ni mmoja wa madiwani wanoheshimika Arusha alishindwa nini kushawishi kikao cha ndani kiitishwe?
Huyu diwani alishafika bei kimyakimya sema yeye aliona aibu kuunga juhudi hadharani badala yake kapitia njia nyingine. Haiwezekani ajifanye hajui sababu za madiwani na hata wabunge wa nyama vya upinzani kuacha nafasi zao na kuhamia upande mwingine? Lazima anajua manunuzi makubwa yanayofanywa na wenyewe kufika bei.
Kwahiyo kukosolewa hamtaki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi huyu ni wewe au ni watu wawili tofauti?

Hapa upo sahihi kabisa. Ile kutoa tu mtazamo wake haikutosha kuondolewa uanachama mara moja tena ndani ya saa 24. Ilitakiwa onyo kwanza. Huyu diwani tunamfahamu vizuri, ni mtu committed na CDM pamoja na majukumu yake ya udiwani. Si mropokaji wala mkurupukaji. Kuna wakati Komu na Kubenea walileta hitilafu la kiuongozi ndani ya chama lakini chama kikamalizia mambo yao kimyakimya na wao kuomba msamaha. Kwanini haraka haraka kwa huyu diwani? Lema na wenzake ajipime, wanapwaya mno.

Unashangaza sana!

Hujisikii aibu kuwa unaonekana hujui unachokisimamia?
 
Hivi huyu ni wewe au ni watu wawili tofauti?

Unashangaza sana!
Post ya kwanza nilikuwa namjibu mtu anayepiga propanga humu, post ya pili nilikuwa najadiliana na mtu mwenye akili timamu. Mimi na huyu wa pili tuna mtazamo unaofanana na wala siyo mwanachama wa CDM.
 
Diwani wa Kata ya Ngarenaro kwa tiketi ya CHADEMA, Isaya Doita aliyemtuhumu Godbless Lema kuwa hajui kazi na majukumu yake kama kiongozi wa juu wa CHADEMA na pia kama Mbunge amefukuzwa uanachama kwa kosa la kukiuka kanuni na misingi ya uanachama wa chama.

Kufukuzwa Uanachama kunamfanya kupoteza hata Udiwani wa Kata ya Ngarenaro kwa sababu Diwani lazima awe na udhamini kutoka chama cha siasa.

Ikumbukwe kuwa Juzi kupitia vyombo vya habari, Diwani Isaya alimtuhumu vikali Mbunge Godbless Lema kuwa hajitambui na hajui majukumu yake kama Mbunge, Mwenyekiti wa Kanda na Mjumbe wa Kamati Kuu ambapo imesababisha chama kudhoofika na kukimbiwa na baadhi ya Madiwani wa Jiji la Arusha.

Ukitaka kusoma na kuangalia video ya tuhuma unaweza kugonga Link hii:

Link > CHADEMA Arusha ‘’kwafuka moshi’’; Godbless Lema aambiwa hajitambui na hajui majukumu yake

Barua ya kumvua uanachama
EPUVdxeXUAA597w

Video ya tuhuma kwa Godbless Lema
Mkuu nisaidie, kwa mjib wa Barua katibu kata anaweza kumfukuza mwanAchama ubunge?

KatibA inasemAje(cdm) kuhusu kustishwa, kusimamishwa Au kufukuzwa uanachama?

Je mtu mmoja, kiongoz, kamati kuu au mkutAno mkuu ndo unauwezo?

Zingatia;
Mwandishi amejitambulisha kama katibu wa katA

na anamuandikiA mkurugenzi wa manicpal... hyo protocal ipoje wakuu,!! Nawaza t kwa saut

Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA, kikao cha shina/kata kina uwezo wa kumfukuza uanachama mwanachama yoyote!
 
CHADEMA hakuna njia nyingine zaidi ya kutimuana, hata vikao vya majadiliano hakuna... Kwa nini msiwe mnajipa nafasi kabla ya kutimuana.!!
 
CHADEMA tangu kuundwa kwake sijawahi kusikia mwanachama anatoa hoja kinzani na anabaki salama,

Nafikiri kwenye hili wanapaswa kubadilika, vinginevyo wanaonekana ni WAHUNI tu

Haiwezekani wahubiri demokrasia wasiyoweza kuiishi.
 
Taratibu za kukosoana ziko kikatiba na zinapaswa kufuatwa.
Hivi huko ccm kiongozi mmoja anaweza itisha press na kumtuhumu wa juu yake badala ya vikao?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe mnawaiga CCM? Mlitakiwa kuonyesha kuwa nyie ni tofauti na kuwa kwenu kuna uhuru wa kutoa mawazo kama jina leni linavyosema. Inawezekana kabisa huyu bwana ameitisha press conference baada ya kuona huko kwenye vikao hasikilizwi. Na kama anachosema ni kweli basi mwaka huu msitafute mchawi.

Amandla....
 
Diwani wa Kata ya Ngarenaro kwa tiketi ya CHADEMA, Isaya Doita aliyemtuhumu Godbless Lema kuwa hajui kazi na majukumu yake kama kiongozi wa juu wa CHADEMA na pia kama Mbunge amefukuzwa uanachama kwa kosa la kukiuka kanuni na misingi ya uanachama wa chama.

Kufukuzwa Uanachama kunamfanya kupoteza hata Udiwani wa Kata ya Ngarenaro kwa sababu Diwani lazima awe na udhamini kutoka chama cha siasa.

Ikumbukwe kuwa Juzi kupitia vyombo vya habari, Diwani Isaya alimtuhumu vikali Mbunge Godbless Lema kuwa hajitambui na hajui majukumu yake kama Mbunge, Mwenyekiti wa Kanda na Mjumbe wa Kamati Kuu ambapo imesababisha chama kudhoofika na kukimbiwa na baadhi ya Madiwani wa Jiji la Arusha.

Ukitaka kusoma na kuangalia video ya tuhuma unaweza kugonga Link hii:

Link > CHADEMA Arusha ‘’kwafuka moshi’’; Godbless Lema aambiwa hajitambui na hajui majukumu yake

Barua ya kumvua uanachama
EPUVdxeXUAA597w

Video ya tuhuma kwa Godbless Lema

hawa wahuni wanadai Demokrasia wakati hawawaruhusu kukosolewa
 
Back
Top Bottom