Diwani Ileje anusurika kipigo cha wananchi kisa ujenzi wa kituo cha afya, mgambo akatwa Mapanga

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,802
11,961
DIWANI ILEJE ANUSURIKA KIPIGO CHA WANANCHI KISA UJENZI WA KITUO CHA AFYA,DC AFIKA NA KUZOMEWA, MGAMBO Akatwa MAPANGA.

Diwani wa kata ya Ndola Mhe Bahati Kyomo amenusurika kupigwa na Wananchi wa Kijiji cha Ishenta kilichopo kata ya Ndola Wilayani Ileje kutokana na Wananchi kutaka kituo cha Afya kijengwe ndani ya Kijiji chao cha Ishenta na si Kijiji kingine.

Inadaiwa kuwa Diwani Mhe Kyomo alifika Kijijini hapo kwa lengo la kuwapa maelekezo ya Serikali Wananchi hao kuwa wemeletewa fedha katika kata yao ya Ndola kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha afya hata hivyo mapokeo ya Wananchi hao hayakuwa mazuri ndipo walipoanza kumzonga kwa vitisho na kumtoa maneno makali Diwani huyo na Vitisho dhidi yake.

Tulipo mtafuta Diwani Mhe Kyomo alikiri kutokea kwa kutukio hilo na alidai kuwa tukio hilo linaonyesha wazi kulikuwa na shinikizo la baadhi ya Wataalamu waliopo Kijiji hapo na baadhi ya wanasiasa wapinzani wake katika siasa na alikwenda mbali zaidi kuwa tukio kama hilo alilofanyiwa yeye baada ya siku chache pia Mkuu wa Wilaya ya Ileja Anna Gidarya nae alifanyia hivyo hivyo na Wananchi wa Kijiji hicho cha Ishenta na cha kushangaza Mtendaji wa Kijiji cha Ishenta Safia Tweve alipoambiwa apeleke muhutasari kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo baada ya tukio la kwanza kutokea hakuweza kufanya hivyo hali iliopelekea kuwa na Wasiwasi kwamba Mtendaji Safina Tweve huenda akawa nae ni miongoni mwa Viongozi wanaochochea mgogoro huo kwa Wananchi.

Alipotafutwa Mkuu wa Wilaya ya Ileje Anna Gidarya alikiri kutokea kwa tukio hilo na alisema kuwa aliposikia tukio hilo kumtokea Diwani wa Ndola alilazimika kwenda kuongea na Wananchi hao kwa lengo la kuwapa elimu lakini cha ajabu Wananchi hao walianza kumtolea kauli zisizofaa kwa jamii na kutaka kuanzisha vurugu na Mgambo aliekuwa akiwatuliza Wananchi hao wa Kijiji cha Ishenta usiku huo huo walimvamia na kumkata kata Mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake na ndipo yeye kama Mwenyekiti wa Usalama Wilaya ya Ileje aliamua kuitisha kikao na Kamati yake ya Usalama ya Wilaya ambapo walimwita Mtendaji wa Kijiji cha Ishenta Safia Tweve na akashindwa kujieleza mbela ya Kamati hiyo hali iliopelekea kumuweka ndani wakati uchunguzi zaidi ukiendelea dhidi yake na wote waliohusika na Vurugu hizo ndani ya Kijijini cha Ishenta.

IMG-20211112-WA0165.jpg
IMG-20211112-WA0164.jpg
 
kuwapa maelekezo ya Serikali Wananchi hao kuwa wemeletewa fedha katika kata yao ya Ndola kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha afya hata hivyo mapokeo ya Wananchi hao hayakuwa mazuri ndipo walipoanza kumzonga kwa vitisho na kumtoa maneno makali Diwani huyo na Vitisho dhidi yake.
Nahis hapa ndipo ulipo mzizi wa fitna. Ni maelekezo gan aliyasema had wakaanza kumzonga na kumtolea vitisho.
linaonyesha wazi kulikuwa na shinikizo la baadhi ya Wataalamu waliopo Kijiji hapo na baadhi ya wanasiasa wapinzani wake katika siasa
Hii inaweza kuwa sababu lakin sina uwakika kama inaweze kufanikiwa kwa kuwashawiahi wanakijiji wote na kama itafanikiwa inamaana ww haukubariki kwa wananchi na ushindi wako wa udiwani unatia mashaka.


Tunaomba kusikia na upande wa wananchi ni kutu gan walikuwa wanakilalamikia/kilichosababisha wakaghadhibika kiasi hicho wenda viongozi ndio wakawa source ya hayo yote.
 
Back
Top Bottom