Elections 2010 Diwani huyu alitetea kiti chake akiwa Jela na bado akasinda

Hassan J. Mosoka

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
682
323
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, Diwani wa Kata ya Bumera kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tengera Marwa jana alitolewa gerezani kwa muda na kwenda kuapishwa wakati wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na baadaye alirudishwa gerezani.

Diwani huyo yuko rumande tangu mwanzoni mwa mwaka huu akituhumiwa kwa mauaji na hata fomu za kugombea udiwani alipelekewa rumande na kufanikiwa kumshinda Katibu Uenezi na Siasa wa CCM wilaya ya Tarime, James Nokwe katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 31 mwaka huu.
 
Watu wamechoka jamani.Waungwe mkono kuondoa udhalimu unaoendelezwa na wanaojiona kuwa mungu watu
 
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, Diwani wa Kata ya Bumera kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tengera Marwa jana alitolewa gerezani kwa muda na kwenda kuapishwa wakati wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na baadaye alirudishwa gerezani.

Diwani huyo yuko rumande tangu mwanzoni mwa mwaka huu akituhumiwa kwa mauaji na hata fomu za kugombea udiwani alipelekewa rumande na kufanikiwa kumshinda Katibu Uenezi na Siasa wa CCM wilaya ya Tarime, James Nokwe katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 31 mwaka huu.

Hiyo nayo sifa?
 
Sifa ni nini? r u crazy baada ya kunywa maji ya kijani?
Mkuu angalia pale nilipohailiti kwa red. wewe umekimbilia kunitukana tu. yaani mtu anatuhumiwa kwa mauaji lakini mleta thread anaona kama sifa vile kwa kuwa na tuhuma nzito hivyo. Any way, huenda ndo sera za chama chetu!, hata mtu akiua bado anaonekana shujaa.
 
Ufalme wa mafisadi siku zenu zinahesabika.
Ngoja tuanze na katiba, baada ya hapo tunashusha pumzi kwa majambazi weusi
 
Mkuu angalia pale nilipohailiti kwa red. wewe umekimbilia kunitukana tu. yaani mtu anatuhumiwa kwa mauaji lakini mleta thread anaona kama sifa vile kwa kuwa na tuhuma nzito hivyo. Any way, huenda ndo sera za chama chetu!, hata mtu akiua bado anaonekana shujaa.

Hayo niliyopigia mstari kama ukiyatilia maanani utagundua ni kwanini wananchi waliamua kumchagua. Lakini usipoyaelewa hayo itakuwa ni kazi bure hata kama utapewa darasa la bure na jaji mkuu!!
 
Waambieni mafisadi wazidi kuwanyanyasa watu huku wakijua zamu yao imewadia.
 
Back
Top Bottom