Diwani CCM Dotto Mtawa ashikiliwa na polisi kwa wizi wa gari

Huyu jamaa ni mwizi kweli na wakati wa kura za maoni wakina mzee kiwia walimkaa hadharani kwakuwa hiki chama hakisikii wakalazimisha na kumpa nguvu jamaa akamvunjia mzee bar yake pale msikitini ferry. Sasa wainuke tena kumtetea utafikiri kigamboni hapakuwa na watu wengine
 
Kosa lake ni ndogo tu. Anatakiwa kudhibitisha tu kuwa hakujua kwamba gari hilo ni mali ya wizi. Sana sana yeye atakuwa ni shahidi namba moja dhidi ya hao wezi.
hakujuaje ni la wizi?? alifuata taratibu za ununuzi wa gari pamoja na registration au alitumia njia za panya ili kukwepa kodi??
 
Huyu jamaa ni mwizi na huo ndo ukweli. Niliwahi kuambiwa na wakazi wa kibada hata kabla jamaa hajaanza harakati za kuwa diwani.
 
Kigamboni Nzima wanamjua,ukifika usiulizie Dotto diwani unaweza ukamkosa,ukiulizia dotto jambazi watakupeleka hadi kwake,ujambazi alianza zamani sana huyu jamaa,kwa tunaomjua ni Jambazi Sugu,alitaka kunipiga kiwanja changu maeneo ya mikadi beach huyu jamaa
Hii kali!
 
Jamani msipende kupotosha, huyo alinunua gari ya wizi bila kujua. kwani siku hizi si hata blue kadi zinagushiwa!
 
Ni Dotto Masawani, diwani wa kata ya Kigamboni, hata kabla ya kugombea kuliwahi kuibuka tuhuma za yeye kushiriki katika wizi wa gari la mkuu wa majeshi katika moja ya nchi za eac,

yote kwa yote, kaipendezesha kigamboni hasa eneo la ferry

Amependezesha kigamboni eneo la ferry??!!! kweli maajabu ya mussa.
 
Dotoo anajitahidi sana katika kazi za maendeleao kigamboni, anatumia pesa yake kuchimba mifereji na kusafisha barabara, kiasi mpaka Mbunge wake kweli amemfunika na hili linamuumba Mbunge kwanini doot amekuwa anapendwa sana na watu, ni wazi kutokana na utendaji wake wa kazi, tuombe Mungu aache ili aje awe Mbunge na aling'arishe jiji la Kigamboni
 
oooohhhhh hili jamaa ni hatari....ukimwona huwa hacheki sura yake tu ukiiona ni ya kijambazi jambazi, ni kweli kabisa kigamboni mzima hakuna hasiye mjua' ishu zake ndio hizo hizo za ujambazi, anajifanya kusistiza usafi wa mazingira kutengeneza mifereji ili aonekane bora, utajiuliza pesa anapata wapi¿ kazi yake kubwa ndio hiyo.. Duh salamu kwa mwana ccm'' oneni sasa, tusije laumiana hapo baadae....
 
bado yupo mahabusu' hukohuko alikofanya tukio, si unajua tena jela wanaenda wenzangu na mimi¿ ukiwa na pesa mambo yanamalizwa juu kwa juu...dahhhh
 
Haaaa Kashatoka siku ile ile jamani,alikamatwa na watu wa usalama wa taifa,dr faustine ndugulile(mb wa k/mboni) hana time ashageuka mfanyabiashara sasa,kaambiwa achangie pesa kidogo kwa ujenzi wa kituo cha polisi kibada kashindwa kweli mb wana kgmboni hawana,ila dotto kama akiacha ujambazi itakua poa ila inaonekana ameingia sisiemu ili kufacilitate ujambazi wake
 
kumbe yule diwani wa ccm kigamboni anayepingana na mbunge wake ni kwa sababu ana kesi ya wizi wa magari huko morogoro hivyo serikari ya ccm imemtumia kuzima kesi yake au walimwambia kesi itafufuliwa upya ndio maana wizara ilimsafirisha na wenzake kuzima hija ya mbunge wao sasa maendeleo yatoke wapi kuwa na mbunge jambazi na mwizi wa magari naomba mnijuze zaidi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom