Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,883
- 6,883
DIWANI wa Kata ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, Dotto Mtawa (CCM), anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma za wizi wa gari.
Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima imezipata zilisema diwani huyo alikamatwa juzi jioni, katika viwanja vya Tuamoyo katika eneo la Kigamboni kwenye sherehe za mkesha wa Mwenge wa Uhuru na kwenda kuhojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam kabla ya kupelekwa mkoani Morogoro.....
Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile, alikiri kupata taarifa hizo na kusema kwamba wanalishughulikia kujua sababu zilizomfanya diwani huyo achukuliwe na polisi.....
Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Adolphina Chialo, alizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu ya kiganjani na kukiri kufikishwa kwa mtuhumiwa huyo kutoka jijini Dar es Salaam, akisema anahusishwa na wizi wa gari aina ya Toyota Coaster lenye namba T 615 BUL.
Chialo alisema tukio hilo lilitokea Agosti 18 mwaka huu, katika eneo la Msamvu Nane Nane mkoani Morogoro kwa watuhumiwa kumnywesha dawa za kulevya dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo. Aliwataja watuhumiwa wengine wanaoshikiliwa kuwa ni Christopher Nyakiaga na mwingine aliyemtaja kwa jina moja la Kileo, na kwamba Mtawa anashikiliwa kwa kuwa inadaiwa kulinunua gari hilo.
Source: Tanzania daima