X-PASTER
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 11,610
- 1,810
Diwani Auawa Kikatili; Binti Zake Wabakwa
Diwani Huyo Alikatwa Mapanga Jumamosi Iliyopita Saa Sita Usiku Nyumbani Kwake.
Diwani Huyo Alikatwa Mapanga Jumamosi Iliyopita Saa Sita Usiku Nyumbani Kwake.
Diwani wa CCM Kata ya Bugarama, wilayani Kahama Peter Kisiminza (50) ameuawa kinyama kwa kukatwa mapanga nyumbani kwake katika Kijiji cha Buyange.
Baada ya kumkata mapanga watu hao waliokuwa wamemvamia usiku wa manane pia walifanya unyama mwingine kwa kuwabaka watoto wake wawili wa kike na kisha kuiba mali na kutoweka.
Kwa mujibu wa taarifa za awali zilizotolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Diwani Athumani, diwani huyo alikatwa mapanga Jumamosi iliyopita saa sita usiku nyumbani kwake.
Kamanda huyo alisema siku hiyo Bw. Kisiminza akiwa nyumbani kwake usiku amelala alivamiwa na watu watatu waliovunja mlango na kuanza kukata mapanga na kuchukua simu yake ya mkononi. Baada ya kutoka nyumbani kwa diwani huyo walikwenda kuvamia kwa mwananchi mwingine kijijini hapo Buyange, Bw. Mussa Robert ambaye naye walimkata mapanga na kuiba simu tano, baiskeli moja na kifaaa kifaa kimoja cha umeme wa solar vyote vikiwa na thamani ya shilingi 567,000. Baada ya kutoweka, watu wa familia hiyo walipiga yowe kuomba msaada ndipo wasamaria wema walipofika na kumchukua Kisiminza na Robert waliwakimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya Segerema mkoani Mwanza kwa matibabu.
- Kisiminza alifariki saa nane mchana juzi.
- Robart alipata matibabu na kuruhusiwa siku hiyo hiyo kutokana na kuwa na majeraha madogo.
Tukio hilo la kuuawa kwa Diwani ni la pili katika kipindi kisichozidi miezi miwili baada ya diwani mwingine wa Lagangabilili, Bariadi, Simba Sita 45 (UDP), kuuawa kwa kupigwa risasi na majambazi.
Majambazi hao baada ya mauaji, walipora pikipiki aina ya Lifan namba T 693 BCN, fedha taslimu Sh 55,000 na simu ya mkononi aina ya Nokia.
Katika uvamizi huo, Nyebu Kadundu (60), aliuawa.
Majira | HabariLeo